Binafsi nashangazwa sana na watu si watanzania tu ila watu wote wanaondekeza dini hususan hapa Afrika. Dini is there for the taking na hakuna dini iliyo bora zaidi ya nyingine. Hindu atajiona yeye bora shinda muislam na ndiyo maana walishindana kule India mpaka waislam wakajitenga na kuunda Pakistan. Ukiwa budha utajiona wewe ni bora shinda yeyote asiyeamini dini yako. Wayahudi same thing....kwa kifupi kila mmoja anajiona dini yake ndiyo bora zaidi ya nyigine wakati Mungu ni yule yule. Kwa huku kwetu Afrika (watumwa wa dini), tunauana kwa ajili ya hizi dini mbili Waarab (waislam) na wakristo (wazungu) wakati hizi dini hazituhusu tuliletewa tu kwa njia ya kurubuniwa ili wakoloni waibe mali zetu na kuchukua mababu zetu kuwafanya watumwa hapa na huko kwao. Eti leo hii sisi ndo tumekuwa waumini zaidi shinda ya wenyewe walioturubuni, jamani inakuja kichwani kweli hii? Practice whatever pleases YOU kwani Mungu ni yule yule. Simama chini ya mwembe au piga magoti chini ya mbuyu....I swear to YOU GOD listens. Kwenda kanisani ama msikitini kupeleka unafiki ni dhambi kwani Mungu alisema pendaneni kama mnavyojipenda wenyewe na muwe na amani. Sasa hapa amani na upendo ambao Mungu alitangaza kupitia kwa Yesu na Mohammad pamoja na dini zingine zote duniani viko wapi? Kuendekeza dini ni ujinga na inaonyesha kuishiwa kwa mawazo kwani dini ain't nothing but faith na faith hailazimishwi. Unaamini kile unachoona kinakufaa wewe binafsi na si the mass! Kwanza ni unafki na kosa kwa yeyote anajitolea kuhubiria watu hadharani kuwa Yesu kasema hivi ama Mohammad anataka hivi, tuna makanisa na misikiti for this. Kwani misikiti na makanisa yamejengwa si ili watu wahubiri au? Imani yako ni personal belief keep it to yourself. Wewe kama unaona Mohammad ama Yesu anakufaa hiyo ni shida yako kwani at the end of the day ni Mungu ndiye anayekuhukumu si Yesu wala Mohammad. Binafsi, ni mkristo ambaye nina damu zote uislam na ukristo lakini sishabikii kwenda kanisani kila Jumapili ama siku kuu. Ninakwenda kanisani tu pale ninapojisikia kwani nikijisikia ndipo ninasali kwa imani yangu yote. Utashangaa watu wanakwenda kanisani kila Jumapili kuangalia fulani kavaa nini ama kuambiana mke wa fulani anatembea na nani...this is stupid na ni dhambi kubwa sana ya kuhukumu watu wakati wewe mwenyewe ni mchafu rohoni. Msikitini ni vile vile, tena siku hizi wanaendekeza unafiki na kupandikiza chuki bila sababu, tena ukichukulia vijana wengi wa kiislam hawajajikomboa kwa kusoma kisha utilie unafki juu yake basi ndo kabisaaaaa, balaa. Maana illiteracy ukichanganya na ujinga pamoja na unafki unavuna ya Mbagala watu kuandamana na kuleta vurugu bila ya kujuwa sababu za msingi, ukiuliza oh si wakristo wamefanya hivi wakati hawana uhakika wanahisi tu. Cha kushangaza wenyewe wazungu na waarab wametulia sie tulioletewa hizi dini balaa tunauana kwa kupigania dini za watu. Waachieni wenyewe dini zao sie tujirudie kwenye imani zetu za mababu. Mbona waliishi kwa amani tu kabla ya Abou Bakari na Johnson kuja?