My brother sikuelewi msimamo wako kuhusu viongozi wa dini kuingia kwenye siasa. Je ni sawa au si sawa?? katiba inawaruhusu au haiwaruhusu? kwa jinsi ulivyojibu swali langu la kwanza ni kana kwamba hausupport viongozi wa dini kuingia kwenye siasa. lakini swali la 2 unaonyesha unasupport waingie ila kwa sababu wameingia zaidi CHADEMA kwako ni issue, zaidi umewaita wanaigana.
Lakini yakupasa kutambua, kwa mtu yeyote makini, ambae hakuwepo kabisa kwenye nyanja za siasa ni nadra sana kujiunga chama kingine hasa CCM. Hii ni kutokana na performance ya CHADEMA kwa siasa za hapa kwetu Tanzania. huu ndio ukweli!!
Imani yako juu ya waraka huu inafanana kabisa na yangu, kwamba waraka huu ni FEKI!! Zaidi ya hapo naamini kabisa waraka huu unaandaliwa na CCM ili kuivuruga CHADEMA ama vikundi vinavyosaka uraisi 2015 kwa ajili ya kupunguza nguvu ya Dr. Slaa kama ataamua kugombea uraisi 2015. nisichokuelewa hapa ni kwa nn unaamini chokochoko hizi zinaletwa na CHADEMA?
Mkuu Mkandara, Si dhani kwamba wakristo walimsupport Dr. Slaa kwa ukristo wake. Wala Dr. Slaa hana support ya wakristo peke yake, bali pia kwa waislam na wasiokuwa waislam wapenda mabadiliko ya kweli. Kwani ni nani asiyeujua uwezo na uadilifu wa Dr. Slaa? Nani asiyejua kwamba alimzidi kwa kila kitu mpinzani wake Dr. Kikwete 2015 (kama uwezo ingekuwa kigezo pekee kuchagua mtu)?
Mwisho lazima tuwe wakweli, udini ni propaganda ya CCM kusambaratisha vyama pinzani. Propaganda hizi zilifanikisha kwa kiasi kikubwa kuidhoofisha CUF, na sasa unatumika kwa CHADEMA! Tusipokuwa makini Watanzania UPUMBAVU WETU utatumaliza!