Rais Kikwete, mbegu uliyoipanda italitafuna taifa letu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete, mbegu uliyoipanda italitafuna taifa letu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DOUGLAS SALLU, Nov 15, 2010.

 1. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,611
  Likes Received: 4,719
  Trophy Points: 280
  Siyo siri kuwa muasisi wa siasa za maji taka hapa Tanzania ni JK na genge lake la wanamtandao. Mbinu hii aliizanza mapema kabla ya uchaguzi wa mwaka 2005, na wahanga wakubwa wa siasa hizi za kishenzi ni Fredrick Sumaye, Salim A. Salim, Prof.Mark Mwadosya na wengineo, na wahanga hawa walilengwa kwani walionekana kuwa tishio kwa malengo ya JK kuukwaa urais hivyo ilikuwa lazima wachafuliwe kiasi cha kutosha ili wanuke na wakati huo magazeti yakimpamba JK kwa sifa asizostahili, na kweli mbinu hii ya kishenzi ilifanikiwa na JK akawa rais.

  Mwaka huu kwa vile kanuni za CCM zilikuwa zinamlinda JK asipate mpinzani toka ndani ya chama hicho hakuwa na haja ya kutumia mbinu hiyo na akawa anajiandaa kushinda kwa kishindo, lakini ghafla upepo ukabadilika baada ya mzalendo wa kweli Dr Slaa kuteuliwa na Chadema kugombea nafasi ya urais, JK baada ya kuona kuwa maji ni marefu kwake na chama chake akarudia tena mbinu yake ya maji taka na ndipo zikasikika habari za Dr Slaa kuchukuwa mke wa mtu, lakini kwa vile watanzania wa leo siyo wale wa mwaka 47, waliimpuuza JK na siasa zake hizo chafu wakaendelea kumuunga mkono Dr Slaa.

  Baada ya JK na genge lake kuona kuwa mbini hii haifanyi kazi akaamua kutumia SILAHA YA MAANGAMIZI -
  UDINI.

  Ukazushwa uvumi kuwa Dr Slaa ametumwa na Kanisa Katoliki, mbinu hii ilikolezwa na magazeti ya fisadi Rostam Aziz na mengine kama Habari Leo, AL HUDA, AL NUR, na kama haitoshi zikatumwa sms kwa mamilion ya wapiga kura kumchafua Dr Slaa na kuhusisha na udini.

  Siyo siri kuwa silaha hii imeacha majeraha mengi miongoni mwa Watanzania na mfano hai ni hata hapa jamvini hangover ya siasa hizi za udini zilizo asisiwa na Kikkwete mwenyew e ipo. Dini ni jambo nyeti sana na likitumiwa vibaya linaweza kuilipua nchi nzima na hiki ndicho alichokifanya JK.


  NATOA MWITO KWA WACHA MUNGU WOTE TUOMBEE NCHI YETU IONDOKANE NA SUMU ILIYOMWAGWA NA JAKAYA MRISHO KIKWETE
   
 2. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Umesema yote. Nilipomsikia anaongea siku ya kutangazwa matokeo kuwa inabidi tutib majeraha yaliyosababishwa na kampeni hasa udini nikjiuliza huyu mtu ana akili kweli? Kama alikuwa na akili asingetumia hizi mbinu chafu ili uje utibu baadaye, hajui kuwa tiba inaweza kukubali au kugoma?

  Kwa yeye nadhani lengo ilikuwa kurudi ikulu at whatever cost nchi itakayoingia na matokeo yake yeye na genge lake wameanzisha mbegu mbaya sana kwa taifa hili. Sumu hii inaweza kuendelea kututafuna miaka hata miaka kwa sababu wanasiasa uchwara wataona ndio njia rahisi na nyepesi ya kuingia madarakani. Ubaya ni kuwa hakuna sheria ya kuwazuia ni kama mtu una moral authority ndio ujuzuie kutumia mbinu chafu kama hizi.
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Dhambi hii JK itamtafuna yeye na chama chake hadi kisambaratike.Leo kammaliza sitta.Na yeye tunamsubiri miaka mitano si mingi tuone ataishije atakaposhuhudia ubaguzi wa kidini alioasisi.NIKUKUMBUSHE Douglas, KIKWETE ALIAHIDI KUWA ANATAKA AKITOKA MADARAKANI WATANZANIA WAMKUMBUKE.Na sasa watanzania wamepata kitu cha kumbukumbu toka kwa JK, MUASISI WA UBAGUZI KWA DHANA YA KIDINI

  JK TUTAKUKUMBUKA KWA UASISI WA UDINI
   
 4. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hakika hili la UDINI limeniumiza kuliko mambo yote niliyowahi kukutana nayo kitaifa. Hakika tusisahau kamwe yale maneno ya Mwl J K Nyerere aliyosema "watanzania wote ni ndugu... bila kujali rangi, kabila wala dini zao..."

  Turudishe uhusiano wetu uliotukuka wa kuheshimu imani na dini za watu wengine. Kwa sasa si muda wa kulaumu nani ni nani na nani alifanya nini, Nadhani sasa ni muda wa kujega mahusiano yaliyohitilafiwa na watu wachache wanaopenda madaraka. Ni wajibu wangu mimi, wewe na yule katika kuhakikisha tunalitokomeza hili jambo kabisa.

  Ee mwenye enzi Mungu utusaidie sisi waja wako

  Amen
   
 5. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  DOUGLAS SALLU

  Mods wa JF hii posti haisomeki, tafadhali badilisheni maandishi yawe ya kawaida na makubwa ya kusomeka.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hata ukiandika nini, Kikwete hasomi na wala hayatilii maanani maoni ya wana jf
   
 7. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Udini ni uislam tu? Mbona nyerere na mkapa waliwabagua waislam na hatukusikia kilele? Huyo kikwete hana uislamu jambo musijidanganye kwani kikwete kawasaidia nini waislam tanzania?
   
 8. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hakuna jinsi sasa udini umeiva na mhasisi wake ni JK.Huyu jamaa ni hatari sana na kinachofuata hivi sana ni kuzaliwa kwa makundi ya wafia dini na ndipo hapo tanzania haitakalika tena!!
   
 9. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,065
  Trophy Points: 280
  Siyo italitafuna Taifa tu bali itamtafuna yeye na ukoo wake.
   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Douglas umeniongezea hasira. Namchukia sana Kikwete kutokana na sera hii ya hovyo ya udini. I real hate this guy. Mwaka huu ameianzisha, mwaka 2015 itakua na mwisho wa siku tutafikia kuuana. Na hakuna vita mbaya na ngumu kama vita ya udini. Hii ni vita hatari mno. Inaboa sana kuwa na Rais mwenye akili kama hizi.
   
 11. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,065
  Trophy Points: 280
  Hujaielewa thread tatizo siyo kuwasaidia hawa ama wale ni mbegu ya chuki aliyoipanda.
   
 12. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #12
  Nov 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nani kaandika uislamu hapa? Hivi uliona akina Mkapa na Nyerere au Mwinyi wamepiga kampeni kwa misingi ya udini? Uliwahi kuona wakikataa kuwapa nafasi waislam kutokana na udini wao. Sema waislamu kilichokuwa kinagomba ni elimu. Mbona akina Dk Salim A Salimu na akina Rashidi kawawa walipewa nafasi kubwa sana za kitaifa? Unasemaje kwamba Nyerere aliwabagua waislam. By the way hatujadili uislam, tunajadili mkakati wa kampeni wa kikwete wa kuamua kuwagawa watanzania kwa misingi ya udini. Na huu ni mkakati wa hovyo kuwahi kutokea katika jamii ya watanzania.
   
 13. J

  Jafar JF-Expert Member

  #13
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Congrats
   
 14. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #14
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Tusipokemea haya mambo yatajirudia huko mbeleni
   
 15. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #15
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,611
  Likes Received: 4,719
  Trophy Points: 280
  Hebu toa ushahidi wa Nyerere na Mkapa walivyowbagua waislamu. Na hoja yako kuwa JK kawasaidia nini waislamu ni kuwa Kikwete hajawasaidia chochote waislamu wala hana uwezo huo yeye yuko kuwasaidia mafisadi wazidi kuwafukarisha Watanzania wote wakristo na waislamu kwani athari za ufisadi zinawaumiza wote, na zaidi alichokifanya kwa waisalamu ni kuwafitinisha na ndugu zao wakristo.

  MTU YEYOTE MWENYE MAWAZO YA UDINI AMEFILISIKA KWANI HAKUNA MTU ANAPATA SHIBE YAKE KWA KUWA KIONGOZI ALIYEPO MADARAKANI NI WA DINI YAKE, ILASHIBE YAKO INAWEZA KUKOSEKANA KWA KUWA NA KIONGOZI FISADI HATA KAMA NI WA DINI YAKO
   
 16. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #16
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,611
  Likes Received: 4,719
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo Baba Mwana asha ni wa kwenda The Hague. Huyu JK tabasamu lake la kinafiki linaficha uovu mwingi kuliko wa ibilisi
   
 17. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #17
  Nov 16, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wewe hujaelewa nini kinajadiliwa hapa. Hapa hatuzungumzii Uislamu au Ukristo. Tunachosema ni kwamba JK amewapotosha Watanzania kwa kuzusha kwamba kumekuwa na udini kwenye kampeni za uchaguzi na kupandikiza mbegu hiyo kwa Watanzania. Ni mtu mjinga tu unaweza kubisha ukweli huu. JK kama kiongozi wa nchi alipaswa kuwa wa kwanza kutambua hili. Kamwe hatutamsamehe kwa KOSA hili kubwa alilolifanya.
   
 18. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #18
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  maskini sisi..tatizo la umaskini halitutoshi tunasaka na mengine ya kutagawa katikati ya njaa zetu...hili ni balaaa kubwa
  mix with yours
   
 19. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #19
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  Utajirudia? Kwani hii mbegu ya udini iliyopandwa na Jk ishaondoka ama kutibiwa hata uanze kutoa tahadhari za kutokujirudia. Hakuna kitu kilichowahi kuuchoma mtima wangu na kunisababishia sononeko kama siasa chafu za kidini zilizoruhusiwa na jk kuhubiriwa hadharani wakati wa campaign. Ilikuwa ukipita maeneo ya DSM kile unachoshuhudia kwenye magazeti kama ya alhuuda sijui alnur, huthubutu kuridish macho kwa mara ya pili.

  Yaani ilikuwa ni kama umekutana na mwanamke aliyevaa kikahaba hivyo kulazimika kuyaondoa macho yako haraka usijeingia majaribuni. Na radio kama kheri nk au sipika za baadhi ya misikiti zilikuwa zikinadi mtu ambae waumini wanapaswa kuchagua na waliweza kumtaja kwa jina bila kuhofu. Wangehofu nini wakati serikali iliyopo madarakani ndio iliyowapo muongozo wa yale wanayofanya?

  EEH MUUMBA UTUEPUSHE KWA KUTUCHOMOA KWENYE HII MBEGU YA KIDINI ILIYOASISIWA NA SERIKALI YA JK. TUNAUONA UGUMU WA KUNG'OKA KWAKE KATIKA MIOYO YA WATZ NA NDIO MAANA TUNAOMBA MSAADA WAKO EEH MUNGU. SISI NI JAMAA MOJA TULIOJENGWA KATIKA MSINGI WA KUHESHIMIANA NA KUTHAMINIANA KATIKA USAWA WA KUSHIRIKI FURSA ZA TAIFA LETU, NI KWANINI TUKUBALI MSINGI HUO UNG'OLEWE KWA SASA?

  MTU YULE AJITAKIAE MADARAKA KWA GHARAMA YA KUUSUKUMIA MBALI UTU UMKEMEE KWA NGUVU ZA UWEZA WAKO EEH MUNGU. TUNAOMBA HAYA KWA IMANI KWAMBA HAKUNA JAMBO GUMU LA KUKUSHINDA MUNGU. AAAMEN!
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Nov 16, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,710
  Trophy Points: 280
  Hivi JK kiakili ni okay kweli?.........................maana naona hivi ni vituko hivyo....................na hakuna chembe ya hekima au utashi tunaotarajia kwa kiongzi wa kutumainiwa.................
   
Loading...