Rais Kikwete, mbegu uliyoipanda italitafuna taifa letu...

Rais Kikwete, mbegu uliyoipanda italitafuna taifa letu...

Nazani ni kheri ajitoe maana itaonekana nae anasupport haya maushenzi
 
Nadhani unajua kuwa yeye ni mkubwa kwako na unatambua maneno unayopendekeza sio mazuri.Zingatia anakuheshimu sana mkuu!
 
Ngoja nitoe mifano hai labda wenye ufinyu wa mawazo watanielewa vizuri. Mungu ametuumba na kutupa akili ya kufikiri na kufanya ya maana ili tujikomboe kimaendeleo. Mfano, kuna computer, television, magari, pikipiki, baiskeli, vyoo vya kukalia, ndege na vitu vingi tu ambavyo tumejipatia ama kuvimbua baada ya kupata elimu shuleni si Madrasat. Kuna sababu watu wanaenda shule, utaajiriwa na nani kwa elimu ya madrasat? Tumshukuru Nyerere kwani aliona mbali kwa kuleta free education Tanzania. Nyerere alifanya chini juu kupeleka shule hata sehemu za hajabu ili tu watu wasome waondokane na ujinga lakini bado tu baadhi ya watu wakaona kupeleka watoto wao shule ni mwiko eti watalishwa nguruwe na wakristo. Ukienda madrasat bila kupata elimu lazima tu utakuwa mnafiki, wenzako wanaendelea kwa kupiga hatua wewe unaona unaonewa tu kila kukicha. Tuachane na udini, turudishe watoto mashuleni. Madrasat haina maana kwa maendeleo ya mtoto. Angalieni muislam yeyote ambaye amesoma na anaijua dini/imani...kamwe huwezi muona anakashifu dini ama imani za wenzake kwani anaelewa nini anakifanya.
 
Jambo alifanya mtoto mdogo, hajui hata maana ya dini ni nini!!? Watu wazima na akili zao wanatoka kwenda kuchoma makanisa! Inasikitisha, naamini tz imeingiliwa na wendawazimu huku watawala wakiendelea kula bata kiulaini!!
 
ha ha ha,umenikumbusha saini za Zitto

Mkuu watawala wanaogopa kuwa nje ya bodigad,wangependa waendelee kulindwa na kuwa kwenye motorcade muda wote,so wazo la kujiuzulu kwa Mh.Pinda sio wazo zuri.
 
Ukishakuwa ndani ya CCM dhamila inakufa. Pinda kashaonja asali, dhamila imeshakufa. Pale hatuna mwakilishi wa Ukristo tena.
 
Kama hakuna ufisadi, umasikini ungepungua. Mafisadi wamevuruga nchi, wameweka Viongozi dhaifu madarakani. Wezi na mchwa wanatafuna nchi kila kona kuanzia halmashauri, wizara, bandari na mikataba. Nchi kwisha hii.

bado kitim tim cha fao la kujitoa - NSSF, ppf... Maandamano mengine yaja. serikali inatafuna hela za walalahoi

Mafisadi wametamalaki, umasikini umeenea kwa watanzania
.

Pia kama umasikini ukipungua ugumu wa maisha hakuna.

Elimu Dunia ingetolewa kwa vijana hawa, wasingetumiwa.

Hawa vijana wana njaa, hawana kazi ni rahisi kutumiwa

Lile bomu la Ajira alisema lowasa ndo linalipuka sasa.

Country is so delicate now.

Mafisadi wameteka nchi.

Muungano pia ni kichocheo kingine.

Source: BBC now. Listen
 
Mkuu hili la Pinda kujiuzuru Utasubiri sana lakini siyo Tanzania.:A S embarassed:
 
Wakati huo huo DINI nazo ni mbeleko ya UVIVU WA KUFIKIRI mama wa UTUMWA WA KIFIKRA msingi mkuu wa UKOLONI MAMBOLEO rafiki yao njaa, magonjwa, vita, machafuko, umasikini, wizi, ufisadi, umamluki, uvivu, unafiki, usaliti, .....(unaweza kuendelea mwenyewe kila aina ya uovu) kwa mtu mweusi.
Mungu wetu anaita sasa!
 
Tukemee kwa nguvu zote bila kujali Dini zetu ,makabila yetu ,uwezo wetu kiamaisha na hata upagani wetu, swala hili la UDINI!!! Nalaani vikali WAPANDAJI WA MBEGU HII YA UDINI wasiojua misingi mikuu ya UTAWALA BORA UTU NA HAKI YA MTANZANIA!! Mmetumia nguvu nyingi kuizuia HAKI YA MYONGE MLIYO IPORA na haya ndiyo matunda ya sumu mliyo pandikiza kwa jamii.

HAKI inapigania HAKI!! haki ya myonge iliyopotea…. wanainchi wameilewa vizuri HAKI YAO , nyinyi mkaja na hii mbegu ya udini kuwapandikiza hawa wanainchi masikini ili muendeleee kuwanyonya zaidi…nasema mlaaniwe nyinyi pamoja na vizazi vyenu!!!

Hitimisho: watanzania wote tunawajibu kwa sasa kuhakikisha haki ,AMANI na utu wetu vinarudishwa mikononi mwetu na KAMWE SI MBEGU HII CHAFU YA UDINI!!! Mlipora HAKI NA UTU WETU na kamwe si huu UDINI mliopandikiza …TURUDISHIENI HAKI NA UTU WETU!!

TANZANIA BILA UDINI ILIWEZEKANA INAWEZEKANA NA ITAWEZEKANA!!!
 
Upo usemi katika Biblia usemao kuwa. Kuna baadhi ya vitendo vya wanadamu huwa ni sawa na kupanda upepo ili kuvuna tufani. Vurugu za waislam zinazofanywa leo, serikali hii inavuna tufani.
Tumeshuhudia rais mstaafu, Alhaji Ali Hassan Mwinyi akipigwa kofi hadharani na mwislam. Usisahau wakati ule wa vurugu za mwembechai huyu ndie alikuwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kwa kuwakumbusha, wakati ule waislam hawakuchoma makanisa. Lakini walivunjavunja bucha za kitomoto. (nyama ya nguruwe). Mmoja wa viongozi wa vurugu zile alikuwa huyuhuyu Issa Ponda. Baadhi ya waislam walipigwa risasi na kufa wakati wa kutuliza ghasia. Lakini akina Ponda hawakupata adhabu yoyote yenye maana.
Tumeshuhudia waislam wakilazimisha mahakama ya kadhi iingizwe kwenye mfumo wa serikali. Bila kujali kuwa ni kinyume cha katiba. Kama haitoshi tumewashudia wakilazimisha kuingiza kipengele cha dini kwenye zoezi la sensa. Aidha tumeshuhudia waislam wakivuruga zoezi la sensa lenyewe akina issa ponda wakiwa viongozi wa uhalifu huo. Si hivyo tu, bali pia wakaandamana bila kibali ili kuishinikiza serikali iwaachie wahalifu wa kiislam waliovuruga zoezi la sensa. Na kweli wahalifu wakaachiwa. Maandamanao yale situ yalikuwa haram kwa kuwa hayakuwa na kibali, bali pia walifanya wakati wa zoezi la sensa. Wakavunja sheria ile polisi wanayodai chadema waliivunja walipofanya mikutano wakati wa sense. Wakati chadema walipigwa mabomu na kuuawa kikatili, hawa hawakupigwa wala risasi wala rungu halikurushwa. Kwa nini? Labda kwa kuwa rais ni mwislam. Aidha wakati huohuo CCM walikuwa wanafanya mkutano wa kampeni huko Bububu. Hawa nao hawakupigwa. Kwa nini? Labda kwa kuwa rais ni mwenyekiti wa CCM. Kwanini sheria hizi zinabagua watu. Kosa moja wengine wanauawa lakini wengine wakaa salama. Sijaisahau hotuba ya mwisho wa mwezi wa tisa ya rais.
Tumeshudia waislam wakiandamana kwa mara ya pili bila kibali wakiongozwa na Ponda. Polisi wakaweka uzio wa utepe na kutoa ilani yakutovuka utepe ule. Lakini waislam wale wakakata utepe ule na kuvuka na kufanya yote waliyokusudia. Najiuliza kama Chadema wangefanya hivyo sijui ingekuwaje. WANGEKUFA KWA RISASI ZA POLISI KAMA KUKU. Hakuna aliefumuliwa utumbo wala kupigwa kwa kitu kizito chenye ncha kali. Hakuna kisingizio cha taarifa za kiinterijensia. Sina maana waislam nao walipaswa kuuwa. Nachosema kwa nini sheria hizo zina iona chadema peke yake?
Tumeshudia waislam wakiandamana tena nakuteka eneo ambalo Bakwata walishaliuza kwa madai ya kuokoa mali za waislam. Kiongozi akiwa issa Ponda. Na hatimae tumeshuhudia kile kilichotokea Mbagala. Makanisa yakichomwa moto na wizi ukifanyika. Najiuliza, kwa nini serikali hii intumia sheria kibaguzi wakiwapendelea waislam na CCM na kuwakandamiza wapinzani. Je kwa nini waisalam wanafanya haya kwa kujiamini kiasi hiki? Je ni kwasababu Rais ni mwislam? Makamu wa rais Mwislam. IGP mwislam, kamanda wa kanda maalum ya DSM ni mwislam? Kwa nini?
Najiuliza vipi wakristo hawa watu wenye amani wakiishiwa uvumilivu. “PATACHIBIKA”
Ni wazi sasa serikali inavuna tufani. Imewalea watu hawa kwa muda mrefu sana. Wanavuna walichopanda. Lakini jamaa, aaaaaaaaah! Yuko Oman. Mtajiju. Tanzania tuiendeayo yenye legacy ya udini wa serikali ya awamu ya nne itakuwa Tanzania isiyofaa kwa matumizi ya binadamu kama matokeo ya udini huu uliopandwa na CCM.
 
Acha ujinga wewe. wakati wa uhuru waislam walikuwa wamejenga shule ngapi. hebu zitaje kwa majina katika mikoa mingapi. unajua kwamba nyerere alinyang'anya shule zote za wakristo na kuzifanya za taifa ili waislam ambao hawakuwa na shule nao wasome? hivi hujui Mkapa alichukua majengo ya serikali (chuo cha Tanesco morogoro akawapa waislam. nitajie chuo kikuu walichajenga waislam wenyewe. acha izo.
 
Nasikitishwa sana na hali inayoendelea Tanzania, nawaonea huruma wananchi wa Tanzania kwa maana tunachokitaka hatuna uzoefu nacho wala mahala pa kukimbilia, lakini zaidi nawaonea huruma wakina mama na watoto. Nimekua nikiiangalia hii hali nasikitika sana, matusi yanayotolewa humu jamii forum kwa dini zote mbili naapa sikuwahi kusikia wala kuona kwa umri wangu wa miaka 37 niliyoishi hapa duniani na tanzania in particular. Kiukweli nimekata tamaa na nchi yangu na nimeshaona vita ya kidini hapo mbele.....tuliyopandikiziwa si sawa hata kidogo.
 
amani inatoweka,utulivu unakimbia,furaha inamezwa,raha inakimbia.
jamani watanzania turudishe amani, viongozi wa dini wajenge umoja wa dini zote. nawapenda sana wakiristo na ninawapenda sana waislam.
 
Back
Top Bottom