Rais Kikwete anaipenda CHADEMA!

Rais Kikwete anaipenda CHADEMA!

Kikwete anajua kuwa ni rais wa Tanzania nzima;
Anajua wajibu wake kwa Watanzania wote;
Anajua hata maeneo ya Tanzania yanayoongozwa na viongozi wa vyama vya
upinzani maendeleo yake yanatokana na serikali ya Tanzania chini ya ccm.
 
Wakati mwingine tuwe waungwana! Kama asingesifia akina Wenje ingekua kelele, amewasifia imekua tabu. Mnataka nini?
Kuwa CDM haimaanishi usiongelee mazuri yanayofanywa na CCM hali kadhalika kuwa CCM haimaanishi usiipongeze CDM pale inapofanya vizuri.
 
Alikuja mwanza kama Rais wa nchi na hakuja mwanza kama mwenyekiti wa CCM, ndo maana hakufanya kama Mkuu wa mkoa alivyotaka iwe.Tatizo ni kwa hawa wenzake na JK wao wanajua kila mahali ni chuki za kipumbavu tu,,ndo maana huwa inafikia sehemu JK anatofautiana nao mbali sana.CCM wenye uelewa wa chini huwa hawajui hata ITIFAKI kila kitu wao wanajua ni sisiemu,sisiemu,sisiemu.Big up JK umewaonesha na wao wafuate, SIASA SIYO UADUI.

Yale mashati ya nepii aah sorry nape hayakuwepo maana yale ndo kiashirio kaja kiccm au kiserekare
 
Mkuu nimepita mitaa ya Lumumba nimewaona wako kwenye foleni naona walikuwa wanakinga ila walikuwa wanapiga makelele sana! inaonekana project inasuasua na walikuwa wanazinguliwa malipo.

Ha haaa haaaa uwiii mkuu umenichekesha
 
CDM ndio chama kitakachoongoza nchi baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2015.hivyo JK ni lazima ausome upepo mapema.
 
Kikwete anajua kuwa ni rais wa Tanzania nzima;
Anajua wajibu wake kwa Watanzania wote;
Anajua hata maeneo ya Tanzania yanayoongozwa na viongozi wa vyama vya
upinzani maendeleo yake yanatokana na serikali ya Tanzania chini ya ccm.

Teh teh hata huku upo!!
Twenzetu MMU,huku mi huwa nakimbia mada zake nyingi kichwa huwa kinaniuma
 
Jk ni mlezi wa vyama vyote vya siasa ndio mana hata kipindi kile aliwakaribisha akina slaa, mbowe na genge lake walipoomba kwenda kunywa juice ikulu

Mahali CCM huwa wananiacha hoi ni hapo kwenye kusema viongozi wa Chadema walikwenda kunywa juice ikulu. Hapo ndio utajua watu wa CCM wanajali kula tu na sio issues. Wakati Chadema walikwenda kujadili mambo ya katiba,CCM wao hawajali katiba wanajali chakula. Watanzania amkeni mjue watu wanaojadili maslahi yenu na wale wanajali matumbo.
 
Jk siyo kama SLAA, na wala wananchi hawawezi kuthubutu kumzomea
Nakupa taarifa tu wewe lumumba project,licha ya kuzomewa alishawahi kupopolewa mawe kama maembe kule mbeya,kama unabisha kamuulize.
 
Rais pia aliwaambia Wanaccm wajiandae Kisaikolojia mwaka 2015, maana kitakacho tokea hawataamini.....
 
kama Mungu angeiweka Tanzania iwe maskini kama nchi nyingne na wakatumia akili zao kujiendeleza sijui ingekuwaje? ukweli ni kwamba Mungu amjalia nchi hii sana ukilinganisha na nchi nyingine, lakini matokeo yake ukifuatilia unaona ni kma nchi lenye kundi la watu wasio na vichwa tuamkeni, bado tuko nyuma sana! JK haache kujisifia wengine wana tucheka badala ya kuanza kujibishan utumbo na kusifia ujinga, tutumie muda mwingi kuangalia wapi tuko nyuma na tungeweza kuparekebisha ili tujikomboe kati hali hii tete ya kujitakia. ushabiki haututoi, bado tunajidanganya...
 
Hilo halina ubishi. Mimi siyo shabiki wa JK wala CCM lakini kwenye uungwana,nakubali kwa 100%. Na siyo uungwana tu bali hata hekima pia, na ndiyo maana atamaliza kipindi chake bila rabsha kubwa. Anapigana vita ngumu, anapigwa vita na madikteta ndani ya CCM, na huku nje anasakamwa na wapinzani na baadhi ya wananchi pia. Muda mwingi badala ya kuwaza juu ya maendeleo ya nchi kwanza inabidi utumie muda wake kuvishinda vita vya ndani ya chama.

Linapokuja suala la kiuongozi jk siku zote ni muungwana
 
WENYEWE WAMEANZA KUMKUBALI.
nilishawaambia, siku JK akiondoka madarakani watu watamkumbuka na kumlilia kwani kwa zama hizi za viongozi wavuta bangi kama akina MBOWE nadra kupata kiongozi mwenye uungwana, mwanademokrasia,mzalendo,mfuata sheria na mjenga nchi kama JK.
AFTER ALL, HATA CHADEMA WANAMKUBALI SANA JK japo hawataki kulisema hili hadharani
 
Jk ni mwerevu wenzake CCM hawamuelewi, watakuja kumwelewa baadaye wakati anakabidhi nchi ka makamanda
 
CHADEMA nikama maji usipoyanywa utayaoga tu,people powerr
 
Nimekuwa kwenye msafara wa ziara ya mh.rais kanda ya ziwa,ziara ambaya imemalizika jana na leo rais anarejea jijini dar.
Katika ziara hiyo tumeshuhudia mambo mengi yaliyofanywa na rais lkn mimi nimeibuka na moja kuwa RAIS WETU KIKWETE anaipenda Chadema.Dalili zipo nyingi nitataja chache🙁1) Mkuu wa mkoa Ndikiro alimnyima Wenje(CDM) nafasi ya kuwasalimia wananchi wake wa nyamagana lkn JK alimsimamisha naye Wenje akiwa jukwaa kuu alisalimia waliokuwepo kwa salaam ya makamanda nao wakajb(na jk akiwemo)poweeeeer...(2)JK alitumia muda mwingi kuwasifu HIGHNESS na WENJE (wote wa CDM)kwa jitihada zao kuwaletea maendeleo wapiga kura wao.Kwa sbb hizo na nyinginezo nyingi nashawishika kuamini JK YUPO CCM KIMWILI lkn ROHO YAKE IPO CHADEMA.Wapi Ritz,Zemacopolo,Lizaboni na buk 7 wote? njoo huku haraka nafasi zimebaki chache.
Khaa!! kumbe hata kwenye msafara wa rais kuna mambumbumbu wa siasa. Wewe ulitegemea afanye nini kama mwanasiasa kwa hao waheshimiwa wakati hao ndiyo wanao wawakilisha wananchi wa eneo hilo? Kama hujui hali hii ndiyo ilimpata Mheshimiwa Mbowe kule jimboni kwake na akamsifia Mheshimiwa JK huku mijinga mingine isiyojua siasa za kistaarabu ikidhani Mh. Mbowe alichemka. Tuache ujinga wa kuleta upinzani kwenye maendeleo yetu wenyewe. Tuwe na upinzani kwenye sanduku la kura tu.:whistle:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom