Rais Hussein Mwinyi: Zanzibar inakabiliwa na ugonjwa wa Corona

Ni lini mzee alisema hakuna korona? Kwa siku za hivi karibuni? Acheni ushabiki maandazi..nashangaa MTU anakazana kusema hakuna Corona wakati imeshatangazwa tuchukue tahadhari labda mzee awe anakuja kuwavalisha barakoa na kunawa mikono asubuhi na mchana ndio mtaridhika...
What are you trying to defending?
 
Hussein Ally Mwinyi alistahili kuwa Rais wa Tanzania, sio huyu.
Tanzania haina bahati,imagine angekuwa raisi wa tzbara kila mtu angekuwa na mapenzi na nchi yake..for the first time in my whole life nampenda na kumshabikia kiongozi wa ccm...akigombea huku nitatumia damu sio wino kumpigia kura.. Otherwise mpinzani wake awe Tundulisu hapo labda...
 
Kapewa mamlaka huyu na jiwe ya kutoa kauli hii kwamba corona iko nchini?
1614973438648.jpeg
 
Ni lini mzee alisema hakuna korona? Kwa siku za hivi karibuni? Acheni ushabiki maandazi..nashangaa MTU anakazana kusema hakuna Corona wakati imeshatangazwa tuchukue tahadhari labda mzee awe anakuja kuwavalisha barakoa na kunawa mikono asubuhi na mchana ndio mtaridhika...

Acha uzandiki!! Alifikia kusema Mungu “katulinda na janga” la korona. Hivi unadhani wanapoita vifo vya corona “changamoto ya upumuaji” ni bahati mbaya?? Sasa hivi anasema “mwaka jana Mungu alituondolea korona”. Vipi mwaka huu??

Lugha za fitna huwa hazina uwazi, sijui ni kipi usichokijua huku viongozi wa serikali wakishutumu viongozi wa dini na wanasiasa kuwa hawana mamlaka ya kutangaza magonjwa. Kaa hapo usubiri wakwambie “kuna korona”!!
 
Rais wa Zanzibar leo ametangaza rasmi kuwa Zanzibar inakabiliwa na ugonjwa wa korona na ametaka taadhari za lazima sasa zichukuliwe.

Kauli hii ni ya kwanza kutolewa na kiongozi wa juu wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na pia ni tofauti kabisa na kauli zinazotolewa na Rais Magufuli.

======

Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi akiwa katika ibada ya Ijumaa katika msikiti wa Mfereji wa Wima amedokeza kuhusu kuwapo kwa gonjwa la Corona katika Kisiwa hicho.

Akiongea na Waumini baada ya swala ya ijumaa Dkt. Mwinyi amesema "Ndugu zangu tumekabiliwa na tatizo hili la ugonjwa wa Covid ulioathiri afya lakini pia umeathiri uchumi wa nchi yetu. Lakini Alhamudulillah muelekeo unaonekana ugonjwa huu unapungua na Insha Allah kwa dua zetu sote utakwisha na In Shaa Allah uchumi wetu utarudi katika hali ya kawaida na utaongezeka zaidi."

Zaidi ya hayo, Dkt. Mwinyi ameshukuru Viongozi wa msikiti kumpa nafasi ya kuongea
Ukiisikiliza clip aliyosema na uliyoandika wewe ni vitu viwili tofauti. Hakuna mahali amesema tahadhari za lazima sasa zichukuliwe. Acha upotoshaji
 
Kila mtu duniani anafahamu kwamba huu ugonjwa wa Covid-19 upo. JPM alisema mtoto wake mwenyewe aliugua sasa hii habari ya sijui Tanzania hakuna Covid-19 etc ni ujinga ambao unashikiliwa na Mlevi wa Konyagi, Zito pamoja na wajinga wengine kama Lisu et al.

Swala ni kwamba Wanaokufa na ugonjwa huu ni wachache sana ukilinganisha na nchi jirani ambazo zilijifungua nk. Ukweli utabaki pale pale, Tanzania have managed to control this disease at its best possible situation. Wacheni wivu Tanzania ndio gunzo hivi sasa ulimwenguni.
 
Haujielewi wewe.
Kwani chanjo ndo dawa ya corona?
Kuna watu wame chanjwa na bado wamekufa kwa covid, niko kwenye sekta ya utalii Zanzibar toka mwaka jana mwezi wa nane mpaka leo, siamin kama sijawahi kupata corona, nahisi nimepata zaidi ya mara moja sema sijui tu ila naishi na wenzangu wanaugua na wanapona na wengine tunalala room moja, juzi hapa mmoja amepata mafua makali na hewa kubana amejifukiza sana mpaka mwisho ameenda kununua ugoro ili apige chafya apate unafuu, siku hizi mbili anaonekana ana nafuu, mwingine niko nae mpaka sasa kalala kitanda cha pili, anasema anajisikia ovyo sana anatafuna tangawizi na malimao kama hana akili nzuri, namwombea awe poa, Mungu atulinde sio siri corona ipo, tujilinde
 
Ni lini mzee alisema hakuna korona? Kwa siku za hivi karibuni? Acheni ushabiki maandazi..nashangaa MTU anakazana kusema hakuna Corona wakati imeshatangazwa tuchukue tahadhari labda mzee awe anakuja kuwavalisha barakoa na kunawa mikono asubuhi na mchana ndio mtaridhika...
Watu wengine wanashida sana, nashangaa mpaka watu wenye akili zao kama Maria Sarungi wanasema eti Rais hajatangaza, sijui wanataka afanye ziara majumbani kwao awaambie wao na familia zao tu.
 
Wewe acha uwongo, leo msemaji wa serikali amtangaza rasmi kuwa Tanzania imeweza kuidhibiti corona, sasa wewe na msemaji wa serikali nani mkweli
Sasa kama wameweza idhibiti, wanadhibitije kitu kisichokuwepo?? Mfano unasema umedhibiti samaki jangwani lazima watu wakuone punguani maana jangwani hakai samaki.
 
Kuna watu wame chanjwa na bado wamekufa kwa covid, niko kwenye sekta ya utalii Zanzibar toka mwaka jana mwezi wa nane mpaka leo, siamin kama sijawahi kupata corona, nahisi nimepata zaidi ya mara moja sema sijui tu ila naishi na wenzangu wanaugua na wanapona na wengine tunalala room moja, juzi hapa mmoja amepata mafua makali na hewa kubana amejifukiza sana mpaka mwisho ameenda kununua ugoro ili apige chafya apate unafuu, siku hizi mbili anaonekana ana nafuu, mwingine niko nae mpaka sasa kalala kitanda cha pili, anasema anajisikia ovyo sana anatafuna tangawizi na malimao kama hana akili nzuri, namwombea awe poa, Mungu atulinde sio siri corona ipo, tujilinde
Duuh hii ngumu kumeza japo sishangai maana Norway kuna mtu alipigwa chanjo ndani ya nusu saa kakata moto.

Mkuu hao waliopigwa chanjo na wakakata unaowwzungumzia ni watanzania wenzetu??
 
Back
Top Bottom