Rais Hussein Mwinyi: Zanzibar inakabiliwa na ugonjwa wa Corona

bne

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,618
2,000
Rais wa Zanzibar leo ametangaza rasmi kuwa Zanzibar inakabiliwa na ugonjwa wa korona na ametaka taadhari za lazima sasa zichukuliwe.

Kauli hii ni ya kwanza kutolewa na kiongozi wa juu wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na pia ni tofauti kabisa na kauli zinazotolewa na Rais Magufuli.

======

Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi akiwa katika ibada ya Ijumaa katika msikiti wa Mfereji wa Wima amedokeza kuhusu kuwapo kwa gonjwa la Corona katika Kisiwa hicho.

Akiongea na Waumini baada ya swala ya ijumaa Dkt. Mwinyi amesema "Ndugu zangu tumekabiliwa na tatizo hili la ugonjwa wa Covid ulioathiri afya lakini pia umeathiri uchumi wa nchi yetu. Lakini Alhamudulillah muelekeo unaonekana ugonjwa huu unapungua na Insha Allah kwa dua zetu sote utakwisha na In Shaa Allah uchumi wetu utarudi katika hali ya kawaida na utaongezeka zaidi."

Zaidi ya hayo, Dkt. Mwinyi ameshukuru Viongozi wa msikiti kumpa nafasi ya kuongea
 
lulu za uru

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
1,344
2,000
Ni lini mzee alisema hakuna korona? Kwa siku za hivi karibuni? Acheni ushabiki maandazi..nashangaa MTU anakazana kusema hakuna Corona wakati imeshatangazwa tuchukue tahadhari labda mzee awe anakuja kuwavalisha barakoa na kunawa mikono asubuhi na mchana ndio mtaridhika...
 
bne

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,618
2,000
Ni lini mzee alisema hakuna korona?kwa siku za hivi karibuni? A cheni ushabiki maandazi..nashangaa MTU anakazana kusema hakuna Corona wakati imeshatangazwa tuchukue tahadhari labda mzee awe anakuja kuwavalisha barakoa na kunawa mikono asubuhi na mchana ndio mtaridhika...
Wewe acha uwongo, leo msemaji wa serikali amtangaza rasmi kuwa Tanzania imeweza kuidhibiti corona, sasa wewe na msemaji wa serikali nani mkweli
 
Thebroker

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
1,032
2,000
Mkuu umeandika haraka kama upo UCHI. Pili Mwinyi sio kiongozi wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, tatu inabid umtafute Honi Sigara ujifunze kiswahili kidogo.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
6,782
2,000
Ni lini mzee alisema hakuna korona?kwa siku za hivi karibuni? A cheni ushabiki maandazi..nashangaa MTU anakazana kusema hakuna Corona wakati imeshatangazwa tuchukue tahadhari labda mzee awe anakuja kuwavalisha barakoa na kunawa mikono asubuhi na mchana ndio mtaridhika...
Unavyo jitahidi kumtetea huyo Mzee wako, utadhani ana faida yoyote ile!!🤔
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
82,140
2,000
raisi wa Zanzibar Leo amtangaza rasmi kuwa Zanzibar inakabiliwa na ugonjwa wa korona na ametaka taadhari za lazima sasa zichukuliwe

Kauri hii ni yakwanza kutolewa na Kiongozi wa juu wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na pia ni tofauti kabisa na kauri zinazotolewa Na raisi magufuli.

SASA KWA WALE MATAGA WA JOKA KUU CCM AMBAO WAO KILA KITU NI NDIO, JE NA MWINYI KATUMWA NA MABEBERU?
Zanzibar ni nchi
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
42,113
2,000
raisi wa Zanzibar Leo amtangaza rasmi kuwa Zanzibar inakabiliwa na ugonjwa wa korona na ametaka taadhari za lazima sasa zichukuliwe

Kauri hii ni yakwanza kutolewa na Kiongozi wa juu wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na pia ni tofauti kabisa na kauri zinazotolewa Na raisi magufuli.

SASA KWA WALE MATAGA WA JOKA KUU CCM AMBAO WAO KILA KITU NI NDIO, JE NA MWINYI KATUMWA NA MABEBERU?
Tupe chanzo cha habari!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom