Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,675
- 40,555
Nimepata nafasi ya kusikiliza mahojiano ya Rais na waandishi wa habari wiki iliyopita. Cha kushangaza ni kuwa magazeti yaliandika kuwa Rais kasema "silivunji baraza" au "havunji Baraza" n.k Ukweli ni kuwa Rais hakusema maneno hayo! Na pale aliposema "Uvumi" siyo maneno ya Rais. Ni mwandishi aliyesema kuwa je "uvumi tu unaoendelea mtaani?" na Rais akaashiria kukubaliana lakini hayakuwa maneno yake originally. Na zaidi ya yote kuna mwandishi mmoja alisema ati wamekuja kwa "mfalme" kupata majibu ya masuali mbalimbali. Halafu kitu kingine ni kucheka, kwanini Rais anacheka sana hata anapoulizwa maswali ya msingi? Kuna mahali alicheka hadi waandishi wanatazamana! Jamani waandishi msituangushe namna hii.