Rais wa SMZ aweka wazi mikataba iliyokuwa siri kubwa, Je Rais wa Muungano ataweza?

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,287
24,161
03 Julai 2022
Unguja, Zanzibar.

Rais wa SMZ awamu ya nane Mh. Dr. Hussein Ali Mwinyi ameweka historia kwa kuweka hadharani mikataba iliyokuwa ya siri kwa zaidi ya miaka 30.

Imekuwa kawaida kwa serikali zetu kudai mikataba ni siri kubwa baina ya mwekezaji kwa upande mmoja na serikali iliyopo madarakani kwa upande mwingine. Na kuwaacha wananchi na hata wawakilishi wao kama wabunge au wajumbe ktk baraza la wawakilishi bila ufahamu wa nini kinaendelea baina ya nchi yao na wawekezaji.

Lakini rais wa awamu ya nane wa serikali ya Mapinduzi na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi ameamua kuvunja mwiko wa kuweka siri kuu ambazo zilisababisha kuwepo na uvumi pia gumzo ktk vibaraza na mitaa ya visiwa vya Zanzibar kuwa nchi imeshatiwa mnadani mfano kuwepo ukodishaji wa visiwa kwa siri kwa wageni, kandarasi za majenzi kubwa kupewa wageni n.k n.k

Rais Dr. Hussein Ali Mwinyi katika mazungumzo na waandishi wa habari ameamua kutokaa kimya na vitu kubakia sirini huku vikijadiliwa kama 'uvumi' kutokana na serikali zilizopita za awamu za nyuma kuwa na utamaduni wa kunyamaa kimya bila kutoa maelezo ya kina kile wananchi wanachokiona kinaendelea ktk miji, vijiji na visiwa vya nchi hii ya Zanzibar.

Itakubukwa hivi karibuni matamshi ya Mzee wa CCM Mzee Shamte mwana wa waziri mkuu wa kwanza wa Zanzibar huru kuwa nchi inapigwa mnada huku wao wanaiona ilileta mjadala mkubwa na mpana sio tu Zanzibar bali ulitapakaa mpaka bara Tanganyika.
 
Mwinyi Hana kifua wazanzibar watampasua kichwa sana maana hawajazoea kuhishi anavyotaka yeye, anatakiwa awe mvumilivu kweli kweli
 
Declassified hazina impact tena. Mikatana yenye manufaa kwao binafsi huwezi kuisikia
 
Aanze na waarabu wa Loliondo kama ana uthubutu na uzalendo wa kweli.

Serikali ya SMZ awamu ya 8 imeonesha mfano, ni wakati wa serikali ya Muungano ya Tanzania awamu ya sita na kuendelea kuanza kuitoa hadharani mikataba iliyo sirini toka enzi hizo hadi awamu ya JPM.

ili tujue hii miradi ya migodi, mchanga wa thamani Kigamboni bandari, gesi kusini, zao la korosho kitapeliwa na mkenya n.k nani ni mhusika pande zote yaani aliyesaini kwa niaba ya serikali na mwekezaji ni nani, muda wa mkataba kuisha, magawanyo ya mapato n.k

US$ 190 bilion kuwezesha kila mtanzania kupewa gari ya Noah
 
Mwinyi aache propaganda kakodisha visiwa kwa miaka 99, aweke hiyo mikataba wazi ili ijulikane Kama kakodisha au kauza
 
Back
Top Bottom