Rais hakusema havunji baraza!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Nimepata nafasi ya kusikiliza mahojiano ya Rais na waandishi wa habari wiki iliyopita. Cha kushangaza ni kuwa magazeti yaliandika kuwa Rais kasema "silivunji baraza" au "havunji Baraza" n.k Ukweli ni kuwa Rais hakusema maneno hayo! Na pale aliposema "Uvumi" siyo maneno ya Rais. Ni mwandishi aliyesema kuwa je "uvumi tu unaoendelea mtaani?" na Rais akaashiria kukubaliana lakini hayakuwa maneno yake originally. Na zaidi ya yote kuna mwandishi mmoja alisema ati wamekuja kwa "mfalme" kupata majibu ya masuali mbalimbali. Halafu kitu kingine ni kucheka, kwanini Rais anacheka sana hata anapoulizwa maswali ya msingi? Kuna mahali alicheka hadi waandishi wanatazamana! Jamani waandishi msituangushe namna hii.
 
Ninavyofahamu mimi kama unaulizwa swali lenye umuhimu halafu ukatoa kicheko ni dalili ya kudharau swali hilo.
 
Ninavyofahamu mimi kama unaulizwa swali lenye umuhimu halafu ukatoa kicheko ni dalili ya kudharau swali hilo.

Nyerere alikuwa anacheka sana kisha anakuja na jibu mzinga. Wakati anaanzisha kicheko, wengine munaitikia, yeye anapanga points zake vizuri.

Sijui JK lakini wakati mwingine kicheko sio lazima iwe dharau, huenda ni ujanja wa kupata nafasi ya kupanga points vizuri.
 
The more I follow events at home the more I am convinced we do not hold attention to detail in high regard.

Kwa msingi huo Mwanakijiji unaweza kuonekana "mlalamishi" tu wakati inabidi kujifunza kwenda na detail.

Huyo rais mwenyewe qualification yake kubwa kuchaguliwa ni "kuchekacheka" sasa unategemea nini?

Waliomchagua wamelikoroga, sasa sadly wanalinywa wapende wasipende. My fear ni kuwa anaweza kwenda "Paris Club" or such highfalluting places kama Davos etc halafu akaulizwa either a simple or trick question akabaki kucheka cheka watu wakamfanya yeye laughingstock.
 
LOL!...Rais wetu qualification yake kubwa ni kucheka cheka. Maybe next time we should elect a president with qualification ya kununa nuna...because kucheka cheka so far has been a big flop...of course with a light touch...:)
 
Hakuna rais anayeweza kukubali mbele ya waandishi wa habari kuwa eti ni kweli nitavunja baraza karibuni, according to dataz inasubiriwa tu ripoti ya Mwakyembe na maneno ya mabadiliko yanakuja, maana tusiwape moyo hawa mawaziri wakafikiri hayaji,

Nyie mawaziri ni ku-fasten your belts, they are coming and I belive this dataz!
 
Kwa jinsi hali ilivyo hivi sasa inakuwa rahisi kwangu kuamini "uvumi" wa mitaani kuliko matamshi ya viongozi wa serikali.
 
Nimepata nafasi ya kusikiliza mahojiano ya Rais na waandishi wa habari wiki iliyopita. Cha kushangaza ni kuwa magazeti yaliandika kuwa Rais kasema "silivunji baraza" au "havunji Baraza" n.k Ukweli ni kuwa Rais hakusema maneno hayo! Na pale aliposema "Uvumi" siyo maneno ya Rais. Ni mwandishi aliyesema kuwa je "uvumi tu unaoendelea mtaani?" na Rais akaashiria kukubaliana lakini hayakuwa maneno yake originally. Na zaidi ya yote kuna mwandishi mmoja alisema ati wamekuja kwa "mfalme" kupata majibu ya masuali mbalimbali. Halafu kitu kingine ni kucheka, kwanini Rais anacheka sana hata anapoulizwa maswali ya msingi? Kuna mahali alicheka hadi waandishi wanatazamana! Jamani waandishi msituangushe namna hii.

Mwanakijiji,

Nakubali maandishi yako mengi lakini katika hili ngoja tu tutofautiane kidogo. Waandishi wetu wana haki ya kutafsiri maneno, vitendo na hali ya rais (au chanzo chochote cha habari). Kama wao waliona ni uvumi na wakamwambia kuwa wamesikia uvumi, naye akajibu bila kukosoa kauli yao kuwa ni 'uvumi' kwa nini nao wasichukulie kuwa naye amekubali ni uvumi? Maneno mengine, labda kama yamewekwa katika alama za kufungua na kufunga usemi (") si lazima yawe yametamkwa na chanzo cha habari kuleta maana ile ile. Kama waandishi walikosea mbona Ikulu haijajitokeza kuwakosoa? Twende mbali zaidi, nimesoma gazeti moja juzi Jumapili limetafisiri zaidi kauli ya Rais (nadhani ni Tanzania Daima) limesema "ameficha siri..." Tuwalaumu waandishi wetu katika mambo mengine lakini hili wamejitahidi. Mwanakijiji nawe fanya tafsiri bwana!
 
Kauli mkanganyiko humsaidia JK kuiongoza Nchi kiujanja ujanja na huamua kufanya kitu anapo hisi sifa zake zinaelekea kubaya .Kauli tata normally humpa nafuu JK na kwa msingi huo naamini naye pamoja Ikulu wanapenda ili wapate mahala pa kukwepea kwa muda .
 
By the way, jamani samahani kitu kimoja hapa. Hivi kweli tunasubiri JK abadilishe baraza la mawaziri?.. ili iweje!

Just thinking!
 
By the way, jamani samahani kitu kimoja hapa. Hivi kweli tunasubiri JK abadilishe baraza la mawaziri?.. ili iweje!

Just thinking!

Mkuu Bob, tulipofikia na hili taifa, anything is something hata kama ni nothing! Wananchi tumechoka sana, mabadiliko ni lazima na yanakuja maana kuna mawaziri kama Kapuya, according to the dataz physically, hana tena uwezo wa function as a human 100%, licha ya kuendelea kuwa waziri, ndio maana ninasema kuwa mabadiliko yanakuja, hata kama hayana faida kwetu wananchi, lakini for sure kuna watakao achwa, no way Karamagi ataendelea tena na hata yeye mwenyewe anaziona alama za nyakati tayari, ndio maana siku hizi haishi kwenye makontena yake kule bandarini,

Majuzi aliitwa na kamati ya bunge ya Miundo Mbinu, akakulizwa aliwezaje kupewa tenda ya makontena bandarini na serikali ya awaamu ya tatu, tena ya miaka 25, bila zabuni kutangazwa hadharani, katika dalili zinazoonyesha ku-resign kwake to his fate, aliwajibu wabunge kwa unyonge mkubwa kuwa alipewa na Mkapa mwenyewe kama rais, wajumbe wa bodi ya bandari walipoulizwa walisema exactly hivyo hivyo kuwa walipewa order na Mkapa, kama rais wapitishe na kumpa kampuni ya Karamagi,

Kwa hiyo huyu akitoka uwaziri, inatosha tu mkuu kwetu wananchi, kama ni roho mbaya on our part kumuombea atoke na iwe!
 
FieldmarshallEs,
Sawa mkuu wangu lakini on Karamagi nipo radhi kuweka bet!.. sidhani kabisa kama hili linaweza tokea ktk utawala wa JK..sababu unazijua na wazi hata kwa kipofu.
 
FMES,
Kwa Karamagi kutoka tu haitatosha. Lazima arudishe ile miaka 25 aliyopewa tenda ya kiupendeleo na Mkapa ili haki ionekane kuwa inatendeka.
 
........ no way Karamagi ataendelea tena na hata yeye mwenyewe anaziona alama za nyakati tayari, ndio maana siku hizi haishi kwenye makontena yake kule bandarini,

Majuzi aliitwa na kamati ya bunge ya Miundo Mbinu, akakulizwa aliwezaje kupewa tenda ya makontena bandarini na serikali ya awaamu ya tatu, tena ya miaka 25, bila zabuni kutangazwa hadharani, katika dalili zinazoonyesha ku-resign kwake to his fate, aliwajibu wabunge kwa unyonge mkubwa kuwa alipewa na Mkapa mwenyewe kama rais, wajumbe wa bodi ya bandari walipoulizwa walisema exactly hivyo hivyo kuwa walipewa order na Mkapa, kama rais wapitishe na kumpa kampuni ya Karamagi,

Kwa hiyo huyu akitoka uwaziri, inatosha tu mkuu kwetu wananchi, kama ni roho mbaya on our part kumuombea atoke na iwe!

Vijana siku hizi wanasema "kama noma na iwe noma!"
Orodha yangu ya "kama noma na iwe noma":
1. Karamagi
2. Kapuya
3. Chenge
4. Mramba
5. Mungai (nisamehe tu mzee wangu!)
6. Msola
7.

Wengine pia tajeni mwungwana aone kina nani hawatakiwi humo ndani.
 
Mimi nadhani kuwa Rais ametengeneza mazingira ya kuibuka shujaa. Habari za kificho toka ndani ya "mbuga" ambako anakula mapumziko ya Krismasi ni kuwa ameenda huko na wasaidizi kushinda kawaida ni kama Ikulu imehamia mbugani. Sasa akitoka huko na siku chacha baadaye akafanya mabadiliko makubwa ya Baraza (hata kulivunja) waandishi wataonekana wameongopa na kufikiri Rais aliwaambia uongo kuwa havunji Bunge.

Hapo ndipo Salva na wenzake watakapotoka na kusema "hivi mlisikia Rais alichosema?". Unapoweka maneno ya kunukuu ina maana hayo maneno fulani kayasema kweli siyo tafsiri yako ya nini alimaanisha.

Ni kweli tunaweza kuendelea kusubiri tuone Rais atafanya nini. Nitajaribu kuwakea sehemu ya mahojiano hayo ya Rais muamue wenyewe.
 
Kithuku,

Nafikiri wazo lako zuri sana na itakuwa vema kama tutaweza orodhesha hapa viongozi (Mawaziri) ambao inabidi waondoke tena ikiwezekana wengine kuchukuliwa hatua kutokana na Ufisadi wao. Muhimu ni kuorodhesha pia Udhaifu wao mathlan unaposema Karamagi unganisha na mabaya yake ama uzembe wake kazini.
 
Lazima tukubali kuwa waandishi wa habari hapa nyumbani wanatuangusha sana, naona wengine wanakuwa kama ni wa kupandikizwa. Rais anaitisha kitimoto mwenye badala ya kumuuliza maswali yenye manufaa na maslahi kwa taifa mtu unaanza kuuliza swali kama atafanya reshufle, tena unasema kabisa kuwa uvumi, what a crap. There are a lot of burning issue that The President needs to address lakini hakuna hata mwandishi wa habari aliye dare kugusa hizo issue, sijui ni kuwa wanakatazwa kuuliza maswali ya maana ndiyo wanauliza maswali ya kijinga. Au sijui ni kuwa ni short sighted wanashindwa kuuliza maswali ya maana? Kweli inasikitisha sana, sijui kama hii ni observation yangu peke yangu au wengine mna observe vitu kama hivyo hivyo.
 
LOL!...Rais wetu qualification yake kubwa ni kucheka cheka. Maybe next time we should elect a president with qualification ya kununa nuna...because kucheka cheka so far has been a big flop...of course with a light touch...:)
We had BWM! Kucheka kwa JK ni maumbile ninavyoona mimi na makuzi maana kuwa katibu mkuu wa chama, Masasi ukinuna mambo yataenda?
 
Back
Top Bottom