Rais hakusema havunji baraza!

Nimewawekea mahojiano ya Rais Kikwete na Waandishi nusu saa ya mwanzo hewani. Unaweza kusikiliza kupitia KLH NEWS INTERNATIONAL na angalia kwenye menu yajuu panaposema "Podcasts". Labda itawapa mwanga kwanini sikuweza kuendelea kusikiliza hadi mwisho..!
 
me nijuavyo baraza hilo liliundwa ki ushkaji tuu sasa ka sie tumekaa busy kusubiri jama avunje ushikaji huoo basi tunajidanganyaaa..sana sana wat he will do ni ku badilishia sehemu za ulaji tuu which wont b kuvunja baraza hilo or kuondoa mawaziri flani
 
Hii habari ya kuvunja baraza la mawaziri, sasa inafanana na hadithi ya fisi na mkono wa binadamu.
 
Hii habari ya kuvunja baraza la mawaziri, sasa inafanana na hadithi ya fisi na mkono wa binadamu.

Kweli kabisa, nadhani ndivyo "wafaidika" wa baraza hilo wanavyoiona na wanatamani iendelee kuwa hivyo. Siye kina kuku tunamwomba Mwenyezi Mungu atukubalie dua letu limpate mwewe inshaallah.
 
Mheshimiwa MoD unaweza kuunganisha hii na ile ya "keil" hapo juu kuhusu Rais kutovunja Baraza? at your discretion.
 
Kweli nimesikiliza mahojiano hayo, sikumsikia akitamka kuwa havunji baraza la mawaziri. Alisema waliunda baraza lililopo kutokana na mahitaji, na wataliangalia "mbele ya safari" wakiona kuna haja ya kurekebisha watafanya marekebisho. Sasa mie sijajua kama hapo "mbele ya safari" tushafika ama bado!
 
niseme nini ndugu zangu? nanyenyekea kwa fahari kuwa wenu mtiifu once again my record still stands!

Sijui baadhi ya waandishi walipata wapi maneno kuwa "Rais Havunji Baraza"...

Next time read between the lines na usiweke maneno midomoni mwa viongozi. It is all politics.

Msikose makala yangu ya reaction ya kujiuzulu kwa Lowassa kesho kwenye Tanzania Daima.
 
Back
Top Bottom