Raia Mwema: Wanawake 40 wajitokeza TAKUKURU kutoa ushahidi wa unyanyasaji wa kingono na ubakaji wa Ole Sabaya

Moja kati ya tuhuma zinazomkabili aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ni unyanyasaji wa kingono. Sabaya anadaiwa kulazimisha ngono wanawake mbalimbali, kuwachukua kwa nguvu anapokutana nao kwenye klabu za usiku, na kuwapeleka hotelini kufanya nao ngono kwa lazima. Jumla ya wanawake 40 wamejitokeza kutoa ushahidi, limeripoti gazeti la Raia Mwema.

Kati ya wanawake hao wapo wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika mikoa ya Arusha na Kilimnjaro. Kati ya wanafunzi hao wawili wanadai kulawitiwa baada ya kutekwa na walinzi wa Sabaya walipokutana nae night club. Mmoja kati ya walinzi amekiri kuwapeleka wasichana hao kwa Sabaya lakini amekanusha tuhuma za ulawiti.

"Tuliagizwa kuwachukua lakini sikujua mahusiano yao na Mhe.Sabaya wala sikujua kama walikubaliana kukutana. Nakiri kuwapeleka kwake lakini kuhusu kulawiti siwezi kutoa ushahidi maana sikuwa naye ndani" mmoja wa walinzi wa Sabaya ameieleza timu maalumu (task force) inayochunguza suala hilo kwa kushirikiana na TAKUKURU.

Sabaya anadaiwa kufanya vitendo hivyo katika hoteli mbalimbali za kifahari jijini Arusha na amekuwa akiondoka bila kulipa. Baadhi ya hoteli zimekiri kumdai Sabaya baada ya kupata huduma mbalimbali ikiwemo malazi na chakula lakini amekua akindoka bila kulipa. CG Hotel wanamdai 8.7M, Grand Melia 14.8M, Marves Hotel 3.4M, na Massai Land 9M.

Sabaya ambaye yupo mahabusu tangu May 25 mwaka huu, anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote ikiwa ataonekana ana kesi ya kujibu.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni jana alisema "Ni kweli tunamshikilia tangu jumanne ya wiki iliyopita kwa mahojiano ya tuhuma mbalimbali za matumizi mabaya ya madaraka na rushwa. Akionekana ana kesi ya kujibu atafikishwa mahakamani"
Hao ndio watoto wa magufuli aliokuwa akiwapa kichwa wafanye wanavyotaka bila kuulizwa hoja tu kwamba walikuwa wakiwanyanyasa wapinzani halafu ati utasikia watu bado wanamsifu magufuli la kufanya tumshukuru mungu kwa kumuondosha mapema kabla ya nchi kuingia kwenye matatizo makubwa. Nasema tenaahsante mungu.
 
Kumshikilia mtu zaidi ya siku 5 bila kumpeleka mahakamani sio tu ni uonevu bali ni kinyume cha sheria.
Charge him or release him immidietly

Huna uzoefu na hizi kesi, kesi isiyo na dhamana hata ukipelekwa mahakamani kama ushahidi haujakamilika bado utarudishwa rumande, na utakuwa umejiweka mtegoni maana info zako zimefika mahakamani. Ni bora ukae ndani siku kadhaa ujiweke sawa kwenye ushahidi wako.. labda kama kesi ni ya kuiba kuku
 
Mimi sio mwanasheria, ilakama anafanya ukatili wa kijinsia kingono, akiwa amelewa, sabaya atashinda mcha kweupe manake utetezi utakuja kuwa ni akili ya pombe sio akili yake, je akiwa katika akili ambayo haina pombe huwa anabaka na kufanya ukatili wa kijinsia?

Ingekua mara moja na kwa mtu mmoja sawa, lakini watu wote hao 40 na bado wengine hawajajitokeza aseme aliwabaka sababu ya pombe? Hamna wakili wala hakimu atakayekubali utetezi wa kindezi namna hii
 
Moja kati ya tuhuma zinazomkabili aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ni unyanyasaji wa kingono. Sabaya anadaiwa kulazimisha ngono wanawake mbalimbali...
Why investigating the obvious?

The man was obviously showing every picture of the law breaking leader, where were the government machineries to deal with him.
Let us be a country that abides with the laws govern itself.

Let us abscond the laws are implemented by the virtue of personalities of Leaders.
 
Hao ndio watoto wa magufuli aliokuwa akiwapa kichwa wafanye wanavyotaka bila kuulizwa hoja tu kwamba walikuwa wakiwanyanyasa wapinzani halafu ati utasikia watu bado wanamsifu magufuli la kufanya tumshukuru mungu kwa kumuondosha mapema kabla ya nchi kuingia kwenye matatizo makubwa. Nasema tenaahsante mungu.
Yani asante Mungu
 
Hivi mwendazake alikuwa anatumia vigezo gani kuteua hawa vichaa?
Spika Ndugai naye akamatwe aunganishwe, alishabikia mateso T Lisu na Mbowe Hadi kumvua ubunge na ubunge .
Kusheherekea kupigwa kwa Mbowe.
Bila Shaka alijua wahusika.
Akamatwe asaidie Polisi kupeleleza hayo matukio!!
 
Moja kati ya tuhuma zinazomkabili aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ni unyanyasaji wa kingono. Sabaya anadaiwa kulazimisha ngono wanawake mbalimbali, kuwachukua kwa nguvu anapokutana nao kwenye klabu za usiku, na kuwapeleka hotelini kufanya nao ngono kwa lazima. Jumla ya wanawake 40 wamejitokeza kutoa ushahidi, limeripoti gazeti la Raia Mwema.

Kati ya wanawake hao wapo wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika mikoa ya Arusha na Kilimnjaro. Kati ya wanafunzi hao wawili wanadai kulawitiwa baada ya kutekwa na walinzi wa Sabaya walipokutana nae night club. Mmoja kati ya walinzi amekiri kuwapeleka wasichana hao kwa Sabaya lakini amekanusha tuhuma za ulawiti.

"Tuliagizwa kuwachukua lakini sikujua mahusiano yao na Mhe.Sabaya wala sikujua kama walikubaliana kukutana. Nakiri kuwapeleka kwake lakini kuhusu kulawiti siwezi kutoa ushahidi maana sikuwa naye ndani" mmoja wa walinzi wa Sabaya ameieleza timu maalumu (task force) inayochunguza suala hilo kwa kushirikiana na TAKUKURU.

Sabaya anadaiwa kufanya vitendo hivyo katika hoteli mbalimbali za kifahari jijini Arusha na amekuwa akiondoka bila kulipa. Baadhi ya hoteli zimekiri kumdai Sabaya baada ya kupata huduma mbalimbali ikiwemo malazi na chakula lakini amekua akindoka bila kulipa. CG Hotel wanamdai 8.7M, Grand Melia 14.8M, Marves Hotel 3.4M, na Massai Land 9M.

Sabaya ambaye yupo mahabusu tangu May 25 mwaka huu, anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote ikiwa ataonekana ana kesi ya kujibu.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni jana alisema "Ni kweli tunamshikilia tangu jumanne ya wiki iliyopita kwa mahojiano ya tuhuma mbalimbali za matumizi mabaya ya madaraka na rushwa. Akionekana ana kesi ya kujibu atafikishwa mahakamani"

My Take
Chanzo cha haya yote ni John Magufuli. Yeye alidhani anamkomoa Mbowe kumbe anagongewa watanzania wanyonge
 
Back
Top Bottom