Hungary: Rais ajiuzulu kwa kumpa msamaha mtu aliyehusishwa na kesi ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,463
2,289
Rais wa Hungary, Katalin Novak ametangaza kujiuzulu baada ya kutoa msamaha kwa mtu aliyeficha taarifa katika kesi ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya Watoto

Mtu huyo alitiwa hatiani kwa kuwalazimisha watoto kubadili kauli zao kuhusu ukatili wa kingono uliodaiwa kufanywa na msimamizi wa kituo cha serikali cha kulea watoto

Novak ameomba radhi kwa vitendo vyake pamoja na kukiri kuwa alifanya makosa kutoa msamaha kwa mtu aliyehukumiwa kwa Ukatili.

--

BUDAPEST, Hungary (AP) — Hungary’s conservative president has resigned amid public outcry over a pardon she granted to a man convicted as an accomplice in a child sexual abuse case, a decision that unleashed an unprecedented political scandal for the long-serving nationalist government.

Katalin Novák, 46, announced in a televised message on Saturday that she would step down from the presidency, an office she has held since 2022. Her decision came after more than a week of public outrage after it was revealed that she issued a presidential pardon in April 2023 to a man convicted of hiding a string of child sexual abuses in a state-run children’s home.

Hungary's president resigns over a pardon to a man convicted in a child sexual abuse case

======

Kwa kikosa kidoooogo! That is, kwa vipimo vya Afrika. Eti alitoa msamaha kwa mfungwa ambae alikuwa anabaka Witoto.

Rais anasema alikosea. Anapisha kiti cha Urais.

Kwa sheria ya Hungary, kama ya Tanzania, Rais ana mamlaka ya kusamehe li mfungwa lolote lile. Lakini bado anaingia matatizoni, kwa sababu hawategemei utoe msamaha kwa kila jangili na kila uhabithi wa binadamu. Kuna wakati msamaha hau make sense, wanategemea utumie akili!

Sasa huku kwetu viongozi huwa hawakiri hapa nilichemka, ngoja nisogee pembeni, wananchi wanisamehe, nijipange upya. Kama ambavyo Mzee Mwinyi alivyojiuzulu uwaziri baada ya polisi kuua watu Shinyanga, baadae akarudi kwenye siasa na akawa Rais wa awamu ya pili.

We unadhani Ulaya, nchi iko gizani miezi miwili hawa mawaziri na wakurugenzi wa TANESCO wangekuwa hawajajiuzulu ?
 
Rais wa Hungary, Katalin Novak ametangaza kujiuzulu baada ya kutoa msamaha kwa mtu aliyeficha taarifa katika kesi ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya Watoto

Mtu huyo alitiwa hatiani kwa kuwalazimisha watoto kubadili kauli zao kuhusu ukatili wa kingono uliodaiwa kufanywa na msimamizi wa kituo cha serikali cha kulea watoto

Novak ameomba radhi kwa vitendo vyake pamoja na kukiri kuwa alifanya makosa kutoa msamaha kwa mtu aliyehukumiwa kwa Ukatili.
 
novak.jpg

Rais wa Hungary, Katalin Novak, mshirika wa karibu wa Waziri Mkuu, Viktor Orban, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na hasira ya umma juu ya msamaha uliotolewa kwa mtu aliyehusishwa na kesi ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto.

Muda mfupi baadaye mfuasi mwingine wa Orban, waziri wa zamani wa sheria, Judit Varga naye alitangaza kuwa anajiondoa kwenye utumishi wa umma kutokana na jambo hilo.

Uamuzi wa Novak kujiuzulu umetokana na shinikizo kubwa kutoka kwa wanasiasa wa upinzani na maandamano ya wananchi nje ya Ikulu ya Rais Ijumaa jioni.

“Ninajiuzulu wadhifa wangu,” alisema Novak (46), akikiri kwamba alifanya makosa.

“Ninaomba msamaha kwa wale niliowaumiza na waathiriwa wote wanaoweza kuwa na maoni kwamba sikuwaunga mkono,” alisema Waziri wa zamani wa Sera za Familia.

“Mimi niko, nilikuwa na nitabaki katika neema ya kulinda watoto na familia.”

Novak alikuwa mwanamke wa kwanza kushikilia nafasi ya urais katika taifa hilo Machi 2022.

Mzozo huo ulichochewa na msamaha aliopewa aliyekuwa naibu mkurugenzi wa makazi ya watoto. Alikuwa amesaidia kuficha tuhuma za unyanyasaji wa kingono za bosi wake kwa watoto waliowasimamia.

Mwananchi
 
Haa Wenzetu Hawana Jambo Dogo Isipokuwa Kuwajibika
Tanzania Hiyo Haipo Haitatokea Na Kamwe Kamwe Haliwezekani
 
Maamuzi ni makubwa kuliko kosa ila watu wasio na uelewa wataona kafanya sahihi,, jifunzeni kuona nje ya box kama hujui chochote kuhusu undani wa taarifa hii tulia tu utajua ukweli uliopo.
 
Huku kwetu babu seya aliachiwa huru baada ya miaka kadhaa gwajima anachaguliwa pamoja na Ile aibu kubwa ya kujirekodi na video ya ngono bado anaendelea kuchunga kondoo
 
Huku kwetu babu seya aliachiwa huru baada ya miaka kadhaa gwajima anachaguliwa pamoja na Ile aibu kubwa ya kujirekodi na video ya ngono bado anaendelea kuchunga kondoo
Hata huyo wa Hungary atakaa pembeni na kosa lake hilo haliwezi kuwa la milele kumfanya asiwe na nafasi yoyote tena

Kawaida ya Maisha, mtu akisha kosea akifungwa, anakuwa kwenye sehemu ya mafunzo na isipokuwa mambo yasiyosameheka Kisheria na ingawa kwa Mungu hana hizi sheria za kuhukumiwa tu hata kama katubu
 
Back
Top Bottom