Ole Sabaya afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na kufunguliwa kesi mpya. Amkataa Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU

Ngarob

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
584
1,921
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kufunguliwa mashitaka mengine yanayomkabili, leo Jumatano Juni Mosi, 2022

Sabaya amefikishwa Mahakamani hapo Sa 11:40 Asubuhi.

===========================

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya amemkataa Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Tumaniel Kweka kwa kuwa anatokea Wilaya ya Hai.

Aliwasilisha hoja hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Salome Mshasha, Sabaya alisema hana imani na mwendesha mashitaka huyo kwa kuwa anatokea katika wilaya hiyo na kwamba ni mtu aliyedai ni wa visasi na anatumika kisiasa.

Sabaya na washtakiwa wenzake wanne wanaokabiliwa na mashitaka saba ambapo alienda mbali na kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati kesi hiyo.

Mbali na hoja hiyo lakini kulijitokeza hoja nyingine kupitia kwa wakili Hellen Mahuna, aliyedai washitakiwa hao hawakupelekwa mahakamani hapo kwa kufuata taratibu za kisheria na kwamba mawakili wao hawakupewa taarifa.

Kutokana na malumbano hayo, Hakimu Mshasha ameahirisha kesi hiyo kwa muda wa dakika 10 hadi 15 ili kupitia hoja hizo ili kutoa uamuzi mdogo.


--UPDATES--
 
Screenshot_20220601-121949_Twitter.jpg
 
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kufunguliwa kesi mpya.

Sabaya amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Juni Mosi saa 11:40 asubuhi.

--UPDATES--
 
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kufunguliwa kesi mpya.

Sabaya amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Juni Mosi saa 11:40 asubuhi.

--UPDATES--
Ndiyo tatizo la kumtegemea binadamu, badala ya kumtegemea Mungu aliyekuumba.

Matokeo yake ndiyo haya, yanayomkumba Ole Sabaya🥺
 
Back
Top Bottom