Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Moja ya changamoto kubwa sana tuliyokuwa nayo Tanzania, ni kuona kila kitu tulichokuwa nacho hakifai.
Wakati nchini Tanzania hadi tume ya kupitia mfumo wa Haki Jinai ikiwa imeundwa na tayari ipo kazini, raia wa Afrika Kusini wameonyeshwa kuvutiwa sana na utendaji kazi wa Jeshi la Polisi la Tanzania katika kupambana na uhalifu hadi kufanikisha kukamatwa kwa wahalifu waliotikisi taifa lao siku za hivi karibuni.
Katika tweets zao, raia hawa wa Afrika Kusini wamefikia hatua ya kuomba Jeshi letu la Polisi kwenda kufanya kazi ya kuzuia uhalifu nchini mwao!
Sasa nimeamini nabii hatambuliki kwao. Heko kwa Jeshi letu la Polisi, pamoja na changamoto kweli mmetuheshimisha.