Rafiki yangu kampenda dada mwenye Sickle Cell

Ukumbuke ugonjwa huu mtu anazaliwa nao ila HIV mtu anaupata duniani...
Unaweza kufuru ukamkwepa mtu huyu ila wewe ukaja ukazaa mtoto mwenye nao...

UGONJWA WA SELI MUNDU
(SICKLE CELL)


Wapendwa wasomaji katika mada ya leo na kwa faida ya wasomaji wengine nitapenda kujibu baadhi ya maswali mbalimbali kutoka kwa wasomaji wa makala hii ya Daktari kwa kuuelezea ugonjwa wa Seli Mundu ambao ni ugonjwa wa kawaida katika jamii yetu ambayo imekuwa na dhana tofauti kuhusu ugonjwa huu.

Kabla ya kuanza kuuelezea ugonjwa wenyewe ni vyema basi mpendwa msomaji ukafahamu jinsi gani damu husafirishwa katika mwili wa damu.

Himoglobini (haemoglobin) ni molekyuli ambayo ni sehemu ya chembe hai nyekundu zilizoko mwilini.Himoglobini hufanya kazi ya kuzisaidia chembe hai nyekundu kubeba hewa ya oksijenu kutoka kwenye mapafu kwenda sehemu nyingine za mwili.

Kwa kawaida binadamu anapozaliwa huwa na himoglobini ya kawaida ambayo huitwa himoglobini A (Haemoglobin A) au kwa kifupi HbA na Himoglobini ya kichanga ambayo huitwa Himoglobini F (HbF).Himoglobini A ambayo hutengeneza takriban asilimia tisini na saba ya Himoglobini za mtu mzima imeundwa na jozi mbili za minyororo (chains) za alfa (alpha) na beta (beta).

Chembe hai nyekundu za damu za kawaida huwa laini,za duara na huweza kujipenyeza katika mishipa ya damu kirahisi.Pia huweza kuishi kwa takriban siku mia moja na ishirini (120) kabla chembe hai nyekendu za damu mpya hazijatengenezwa.

Watu wenye ugonjwa wa sickle cell wao huwa na chembe hai nyekundu ngumu, zenye umbo la mundu au mwezi mchanga ambazo hupita kwa shida kwenye mishipa ya damu haswa ile midogo.Aina hii ya himoglobini huitwa Himoglobini S (HbS).Tofauti na chembe hai nyekundu za damu za kawaida,zenyewe huishi kwa siku chache zaidi, kwa kawaida takribani siku kumi na sita (16) tu.

Kwa hiyo ugonjwa wa sickle cell ni ugonjwa wa kurithi ambapo mwathirika huwa na himoglobini S ambayo hupelekea chembe hai nyekundu za damu zisizo za kawaida kushindwa kupita kwenye mishipa ya damu kirahisi.Hali hii hupelekea kuwa na upungufu wa damu kwenye baadhi ya sehemu mwilini.

Hata hivyo iwapo chembe hai nyekundu za damu HbA ni zaidi ya HbS huweza kutengeneza HbAS.Hali hii hujulikana kitaalamu kama Sickle cell isiyo na dalili (Sickle Cell Trait).Watu wenye aina hii ya sickle cell huwa na afya nzuri ya kawaida.

Ugonjwa wa sickle cell ni ugonjwa sugu na wa kudumu.Waathirika waweza kuwa wenye afya njema lakini maisha yao huandamwa na vipindi vya mashambulizi ya maumivu.Umri wa kuishi hupungua na baadhi ya tafiti za nyuma zinaonyesha kwamba waweza kuishi kwa wastani wa miaka arobaini (40) mpaka hamsini (50).Ugonjwa huu ni wa kawaida kwa watu wenye asili ya kiafrika haswa walioko chini ya Jangwa la Sahara lakini waweza athiri watu wa mataifa mengine pia.

Jinsi ugonjwa unavyorithiwa

Ugonjwa wa sickle cell waweza kurithiwa kama ilivyo kwa makundi ya damu, rangi ya ngozi, rangi ya macho na tabia ua vitu vingione vinavyoweza kurithiwa.

Kwa mfano kama mzazi mmoja ana himoglobini AS,amabyo huashiria kuwepo kwa sickle cell bila kuonyesha dalili na mzazi akiwa mzima, basi wana uwezekano wa kupata watoto wenye sickle cell ambao hawataonyesha dalili.

Pia kama mzazi mmoja ana sickle cell na mwingine ana sickle cell bila dalili, kuna uwezekano wa asilimia hamsini ya kupata mtoto mwenye sickle cell au sickle cell bila dalili katika kila mimba itakayotungwa.

Na kuna takriban asilimia ishirini na tano ya kupata sickle cell yenye dalili katika kila mimba.

Jinsi Sickle Cell inavyotokea
Ugonjwa wa sickle cell hutokea kutokana na mabadiliko (mutations) katika mnyororo wa beta (beta chain) ambapo amaino asidi (amino acid) aina ya glutameti (glutamate) huitoa amaino asidi ya Valini (Valine) kutoka kwenye nafasi ya sita ya mnyororo wa beta.

Katika mazingira yenye kiwango kidogo cha oksijeni, chembe hai nyekundu za damu zenye umbo la kawaida (mviringo) huharibiwa na kupoteza uwezo wa kutanuka na kusinyaa (elasticity) zipitapo kwenye mishipa ya damu.Hali hii hupelekea chembe hai hizo nyekundu za damu kuharibiwa na mfumo wa damu kwenye bandama (spleen) uitwao kwa kitaalamu reticuloendothelial system.

Pia hupelekea kuziba kwa mishipa midogo ya damu (infarction) kutokana na chembe hai nyekundu za damu zenye umbo la mundu.Hali hii yaweza kupelekea kukosekana kwa damu na oksijeni ya kutosha katika baadhi ya viungo.

Dalili za sickle cell

Ni mara chache kwa dallili za sickle cell kuonekana katika miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa.Hii inatokana na kuwepo kwa wingi kwa himoglobini ya kichanga, himoglobini F, ambayo huzilinda chembe hai nyekundu za damu zisibadilike umbo.
Ikumbukwe kwambamabadiliko ya kiumbo ya chembe hai nyekundu za damu ndiyo chanzo cha dalili tutakazoziona hivi punde.

Dalili utotoni
-Maumivu ya pingili (dactylitis) za mikono na miguu
-Kushambuliwa na maradhi kama uti wa mgongo,
nimonia,mafua,kikohozi n.k
-Kuvimba kwa bandam (splenomegally) kutokana na kujaa ghafla
kwa damukwenye bandama
-Kusinyaa kwa bandama(autosplenectomy)

Dalili ukubwani

-Upungufu wa damu
-Maumivu ya tumbo
-Maumivu ya mifupa (viungo)
-Kupooza
-Maumivu ya kifua yafananayo na nimonia (acute chest syndrome)
-Kubana kwa kifua
-Kukojoa damu
-Vidonda sugu miguuni
-Kusimaama kwa uume kuambatanako na maumivu makali (priapism)
-Kuvimba kwa paji la uso au fuvu

Vipimo na Uchunguzi

Vipimo vifuatavyo ni muhimu katika kugundua sickle cell na magonjwa yaambatanayo na sickle cell
-Kipimo cha Sickling (Sickling Test)
-Kipimo cha damu kama kuna Malaria
-Kipimo cha mkojo kuchunguza uwepo wa chembe hai nyekendu za damu katika mkojo
-Picha ya kifua (x-ray) kuangalia iwapo kuna athari katika kifua
-Kipimo cha wingi wa damu (Hb level)
-Kipimo cha kundi la damu (Blood grouping and cross matching)

Matibabu

Aina ya matibabu anayohitaji mgonjwa hutegemeana na aina ya mgonjwa na tatizo linalomsumbua kwa wakati huo. Ni vyema kuchukua hatua mapema iwapo una mtoto mwenye dalili zilizotajwa hapo juu.

Ushauri

Ugonjwa wa Sickle cell ni ugonjwa sugu na wa kudumu.Watu wenye ugonjwa huu huambukizwa kirahisi magonjwa mengine kama vile nimonia, malaria n.k

Wagonjwa wenyewe wanatakiwa kujilinda dhidi ya baridi, magonjwa ya kuambukiza kama nimonia, malaria, magonjwa ya mifupa n.k

Pia ni vizuri kwa mgonjwa wa nimonia kuoa au kuolewa na mwenza ambaye hana sickle cell ili kupunguza uwezekano wa kupata mtoto mwenye sickle cell.

Kwa wakina mama wenye sickle cell na wenye mpango wa kubeba ujauzito ni vema wakafahamu kwamba upo uwezekano wa mtoto kudumaa kiakili akiwa tumboni, kutoka ghafla kwa mimba na kupata kifafa cha mimba. Pia ni vizuri kwa wagonjwa wa aina hii kutiwa moyo.


Huyu pasipo kutia shaka ni Dr ksb haya yote aliyoyaandika hapa, ndiyo yaliyozungumzwa na kushauriwa na Ma Dr pale MNH kipindi nahudhuria clinic ya wagonjwa Wa sickle cell kabla hatujaambiwa kimefungwa. Ila nashukuru Dr Wa mtoto wangu bado anaendelea kunisaidia kila ninapohitaji msaada Wa ushauri au matibabu.
Asante Dr ,naona sasa watakuwa wameelewa vizuri wale wote ambao walikuwa hawana uelewa juu ya ugonjwa huu, asante sana.

Hiyo ya udumavu Wa akili, namshukuru sana Mungu ksb Mwanangu ameepukana nayo.
 
Tu


Tunaugua malaria, tena sisi tukiugua tunaumwa kweli kweli na kibaya zaidi hata damu inapungua.
Tunashauriwa sana tujilinde kila tuwezavyo tusiumwe malaria.
Sickle cell ukifuata masharti yake wala haisumbui sana, utajikuta unaishi kama waishivyo wengine.

Hivyo ukiniona Mimi naangalia TV, au najisomea nikiwa ndani ya neti usinishangae...natania tu ha ha ha ha
Mkuu wewe umefanikiwa kuishinda hofu..! Mungu wetu ni mwema hongera kwa kuwa na furaha.
 
Haku
Napenda wataalamu na watu wenye uzoefu mniambie ni vipi mtu anaweza kumhandle mtu mwenye sickle cell. Huyu rafiki yangu ameambiwa baada ya kuwa tayari kazama kwenye bwawa la mahaba anampenda sana msichana, isitoshe ni kitu matata kichwani, umbo, upole kiufupi wife materials shida hiyo sasa sicklecell, nasikia kuishi kwao siyo garantee jamaa anamwogopa tangu aambiwe hilo tatizo, mtujuze life span yao pia.

Nitanguliza shukrani.

Mkuu hakuna maisha yenye guarantee, tuakufa za kuzaliwa randomly.
 
Mm ningempenda sana. Nilikua kuwa na mahusiano na binti mwenye hiv. Alininyima penz mpaka nikajilaumu, akaja kuniambia ukwel, nilimpenda sana mpka mwenyewe akaniacha.
Duuh! Kuna watu mna mapenzi yenu aisei..!
 
Napenda wataalamu na watu wenye uzoefu mniambie ni vipi mtu anaweza kumhandle mtu mwenye sickle cell. Huyu rafiki yangu ameambiwa baada ya kuwa tayari kazama kwenye bwawa la mahaba anampenda sana msichana, isitoshe ni kitu matata kichwani, umbo, upole kiufupi wife materials shida hiyo sasa sicklecell, nasikia kuishi kwao siyo garantee jamaa anamwogopa tangu aambiwe hilo tatizo, mtujuze life span yao pia.

Nitanguliza shukrani.
Ni ugonjwa hatar sana unarithishwa pia binafc ukoo wetu wote upande wa mama una sickle cell kila kila familia ina watoto au mtoto mwenye sickle cell ila anatakiwa ajue ana sickle cell trait or sickle cell desease ( Anaemia) trait anakuwa anabeba single sickle cell from only one parent huyu anakuwa hana shida sana anazaa na anaishi kikawaida labda kuumwa umw kidg kukauka damu barid viungo kuuma ila sio hatari sana but mwenye sickle cell desease yeye anabeba sickle cell from all parents so anakuwa na desease yenyew wengi wanakuwa wembamba kukauka damu mara kwa mara vingo kuuma baridi na desease inakuja pale if mother have sickle cell desease and father ana sickle cell desease or mzaz mmoja ana sickle cell desease mmoja ana trait or wote wazaz wawil wana trait sickle cell na kila watoto watakaozaa kwenye wa3 japo mmoja atakuwa na Desease wengine watapata japo trait yani wanabeba gense kwa mzaz mmoj tu wanaobeba kw wazaz wote ndo wanapata desease na hapo ujiandae kuuguza mara kwa mara ila wanaish japo kwa tabu naongea haya nn experience nayo mtoa mada mke wa rafki yako anaish wapi
 
Isitoshe haujawah kutokea msiba wa mtu kwetu aliekufa kwa sickle cell japo wanaish kwa tabu wenye sickle cell desease
 
Hamisi almaarufu FA anadunda kama kawa na kaoa zake na kabinti Mungu kawajaalia kama jamaa ako kampenda uyo binti asonge nae tu huo uoga wake sio kinga maana Mungu fundi unaweza kumuoa mwenye afya zake ila baada ya ndoa akateleza tu bafuni na akapooza mazima aya mambo ukijifanya uko makini kuliko umakini wenyewe utajikuta umefika mwisho wa safari kabla haujaianza.
 
Seli mundu au sickle sell kama mnavyoita wenye wazungu ni ugonjwa usio na shida hasa kwa wale ambo wamevuka 18 yrs.

Naomba umwambie rafiki yako ajitahidi sana kama moyo haupo tayari kumuoa kwa sababu ya hiyo seli mundu amuache bila kumsababishia jeraha.

Mwaka huu kuna binti tumezika huko kasulu kisa jamaa alimuacha kwa sababu ya huo ugonjwa mbaya zaidi walikuwa wameshatambulishana na shughuli za ndoa zilikuwa moto moto. Binti alikuwa anajiandaa kwa ajili ya send off ndio mashilawadu wakamwambia mwanaume kuwa binti ana ugonjwa wa seli mundu na tayari binti alikuwa na mimba ya watoto mapacha tumboni.

Jamaa alipopewa zile taarifa alienda kuomba ushauri kwa wazazi wake ambao waliona ule ugonjwa ni kama nuksi vile ikabidi wamzuie kijana wao kumuoa yule binti. Binti alikuwa mwalimu wa sekondari huko Mwanza kwa msongo wa mawazo alioupata ukizingatia alishachangisha watu michanganyo ya send off na harusi leo hii aje kuwaambia ndio imeota mbawa kama ya Vicky Kamata. Binti akaiaga dunia akiwa mapacha wake tumboni.

Chonde chonde kijana naomba umuombe rafiki yako amuache kwa tahadhari kubwa sana huyo binti ili asije akafariki kwa upweke na mawazo.

Ila sickle sell sio ugonjwa wa kumuogopa mtu ispokuwa watoto au wajukuu wa huyo mama au mwenye hayo maradhi lazima wataurithi tu.
Hakutakiwa kumuacha kawaida mwenye desease anakuwa na doctor maalum anaemguide n maisha yanaenda murua
 
Hatumkatishi tamaa lakini anything can happen any time. Pia kuna uwezekano mkubwa wa kuzaa watoto wenye hilo tatizo kwa sababu huo ni ugonjwa wa kurithi.

Umenikumbusha msiba wa rafiki yangu kipenzi aliyekuwa na hilo tatizo.

Ni kweli ugonjwa sickle cell ni wa kurithi. Lakini mtoto anaweza kuurithi ugonjwa huo kutoka kwa wazazi wake endapo wazazi wa pande zote mbili watakuwa wamebeba vina 7 (genes) za sickle cell.

Mtoto hawezi kurithi huo ugonjwa endapo mzazi 1 ndio amebeba vina 7 (genes).
 
  • Thanks
Reactions: VSM
Mwambie huyo jamaa yako kama kazoea bao 3 kwa mchepuko hapo nibao mojatu. akizidisha anamuua
 
Huyu pasipo kutia shaka ni Dr ksb haya yote aliyoyaandika hapa, ndiyo yaliyozungumzwa na kushauriwa na Ma Dr pale MNH kipindi nahudhuria clinic ya wagonjwa Wa sickle cell kabla hatujaambiwa kimefungwa. Ila nashukuru Dr Wa mtoto wangu bado anaendelea kunisaidia kila ninapohitaji msaada Wa ushauri au matibabu.
Asante Dr ,naona sasa watakuwa wameelewa vizuri wale wote ambao walikuwa hawana uelewa juu ya ugonjwa huu, asante sana.

Hiyo ya udumavu Wa akili, namshukuru sana Mungu ksb Mwanangu ameepukana nayo.
Hiyo ya udumavu wa akili sio kweli. Mm nimesoma na mtu mwenye shida kama hiyo alikuwa very bright. Na saiv ni Daktar wa binadam na yuko above 30yrs now na afya yake iko njema kbsa
 
Mtu mwenye sickle cell akishavuka 22yrs haina complication sana. Sema kwenye ujauzito atahitaji uangalizi wa hali ya juu coz tatizo kubwa kwao ni kupungukiwa damu kunapoweza kuleta kifo cha ghafla.
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom