Rafiki yangu kampenda dada mwenye Sickle Cell

Rafiki yangu kampenda dada mwenye Sickle Cell

Siyo ugonjwa wa kuogopa? haupo sirious..... Huo ugonjwa ni mbaya sana Mungu aepushie mbali..... Unatakiwa uwe unahudhuria clin mara kwa mara sana kuna dawa unapewa...... Wanasema siyo rahisi sana kuvuka miaka 30...... Kama unao ukifikisha miaka 60 na kuendelea viungo vya mwili vinakuwa havina nguvu tena..... Wengi wanakufa kuanzia miaka 6 kurudi chini
Mmhh
 
Wataalamu wanadai mtu mwenye sickle cell hususani mwanamke akipata mimba before 20's anapoteza maisha mara nyingi watu hawa wanakuwa dhaifu sana kwa sababu Oxygen haiwi ya kutosha ndani ya redi blood cells kutokana na Cell zenyewe kuwa incomplete hawaishi muda mrefu mmoja nilisoma nae olevel at the age of 20 to 24 alipoteza uhai wake lakini maisha yake yalikuwa dhaifu mno
 
Mbona mi namjua MTU ana sickle ni MTU mzima na ana watoto,..sema labda kwa sababu ni ugonjwa wa asili,na wengi nayo wapo prone sana na disease hasa malaria,

Unaweza ishi naye tu,maisha yenyew hayak guaranteed,..

Kabisa mkuu hawana shida ni namna yao kuishi tu ndio inakuwa na masharti kidogo ila hakuna tofauti na mtu mwingine wa kawaida .

Kufa kupo tu.
 
Ajilinde kila awezavyo asiwe anaugua malaria Mara kwa Mara, ale balanced diet, anywe Maji ya kutosha kila siku, afanye mazoezi , akienda hospital aonane na Dr wa huu ugongwa anaweza kushauriwa kunywa folic acid, ale vyakula vingi /matunda yanayoongeza damu. Apate muda Wa kupumzika. Asifanye kazi ngumu sana, mfano za kuchimba barabara kwa sululu.
Kuna kipindi namtania mwanangu, namwambia kuwa huu ugonjwa tulionao tunatakiwa tuishi maisha mazuri hivyo azingatie sana elimu ksb kazi ngumu sana Mungu kampa upendeleo Wa kutokufanya.
Ukimpenda mtu mwenye sickle cell wala usimwache eti ksb ana ugonjwa au ana vimelea vya ugonjwa huo, labda umwache ksb zingine. Kikubwa muonane na wataalam ili awape ushauri Wa kitaalam ili muishi kwa furaha ,amani na upendo.
Na huo ndio ukweli halisi. Hongera sana mkuu
 
Ndio... Yaani carrier akizaa na carrier mwenzake wana chance kubwa ya kupata mtoto mwenye sickle cell...
Sijui kwanini watu hatupimagi hii kitu kabla ya kuoa/kuolewa.
Kwa hiyo wenye nao watakuwa hawaoi au hawaolewi?

Nadhani elimu ni ndogo juu ya huu ugonjwa hiyo ndio sababu.
 
Kwa hiyo wenye nao watakuwa hawaoi au hawaolewi?

Nadhani elimu ni ndogo juu ya huu ugonjwa hiyo ndio sababu.
Sio kua hawaoi/hawaolewi ila wanaangalia kutooana wenye chance kubwa ya kuzaa watoto wenye sickle cell. Na atakama watu wakiendelea kuoana wajiandane na kuhudumia mtoto mwenye sickle cell anaemia.... Isije kama mshtuko
Mimi chuo nilichoenda wote tulipimwa hiyo genotype... Kwa Tanzania Elimu ya huu ugonjwa kweli ingeenea.
 
Kutooana wenye chance kubwa ya kupata watoto wenye sicke cell ukimaanisha nini sio mbaya ukafunguka ili asiyejua akajua.
 
No ni kawaida mapenz upofu cha msingi ni kumhandle kutoka na na hari yake na mpende kwa dhati update dhawabu sio kwa tamaa zenu
 
Sio kua hawaoi/hawaolewi ila wanaangalia kutooana wenye chance kubwa ya kuzaa watoto wenye sickle cell. Na atakama watu wakiendelea kuoana wajiandane na kuhudumia mtoto mwenye sickle cell anaemia.... Isije kama mshtuko
Mimi chuo nilichoenda wote tulipimwa hiyo genotype... Kwa Tanzania Elimu ya huu ugonjwa kweli ingeenea.
Ni probability wanaweza kuza watoto wasio na huo ugonjwa ila lazima kizazi cha hao watoto wao wanaweza pata,ila kuna mtu yuko ivyo na watoto wake hawana ila wajukuu zake ndio wanao
 
Kutooana wenye chance kubwa ya kupata watoto wenye sicke cell ukimaanisha nini sio mbaya ukafunguka ili asiyejua akajua.
Oook!
Ukipima genotype kuna za aina tatu.
AA, AS au SS
AA- huyu hana kabisa ata chembechembe za sickle cell
AS - huyu haugui sickle cell anaemia ila amebeba chembechembe za sickle cell
SS - huyu ndo anaumwa sickle cell Anaemia.

Sasa
1. AA + AA = AA (watapata watoto wazima wote)
2. AA + AS = AA, AS (Wana chance ya kupata watoto wazima na waliobeba chembechembe za huo ugonjwa)
3. AA+ SS = AS ( Watapata watoto wote waliobeba chembechembe za huo ugonjwa)
4. AS + AS = AA, AS, SS (watapata watoto wazima, waliobeba chembechembe za huo ugonjwa na mgonjwa)
5. AS + SS = AS, SS (Watapata mtoto aliebeba chembechembe za ugonjwa na mtoto mwenye huo ugonjwa)
6. SS + SS = SS (Yaani hawa kila mtoto watakaepata atakua na huu ugonjwa)

(Nimeelezea kwa nilivyofundishwa, sina background ya udaktari... Madaktari wataweza elezea vizuri zaidi)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom