Rafiki yangu ni mapenzi kwa mkewe yalimzidia au ulimbukeni?

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
10,561
19,059
George au "Big" kama tunavomuita kutokana na umbo lake kubwa ni rafiki yangu japo sio tena kama ule urafiki wa miaka kadhaa iliyopita ambapo hata familia zetu kwa maana ya wake zetu walikua karibu na ukaribu wa kutembeleana na hata kufanya mitoko na safari za pamoja za kwenda kula mema ya nchi

Big hakua mtu wa totoz au hakua macho juu kiviile, na pale alipojaribu kuchepuka kwa ku date na dada mmoja mfanyakazi mwenzie akajikuta kabobea na kazama kichwa na miguu! Mkewe(walikua wanaishi pamoja tu walikua hawajaona) akimjua huyo dada kua ni workmate wa mumewe na mwanzoni hakua na wasiwasi nae hata chembe

Mimi alikuja kuniambia wife wangu kua mama P(mke wa Big tulimuita kwa jina la mtoto wa dada yake yeye hakua na mtoto) amegundua kua Big ana cheat na huyo mfanyakazi mwenzie. Ameambiwa na watu (maana alikua na connection na wafanyakazi wengine wa ofisi ya kina George) na kwamba ameshafanya uchunguzi wa kutosha na sasa na yeye ana lipa kisasi kwa kuondoka kabisa hapo kwake na kashafanya maandalizi

Licha ya kuonywa na wife wangu kua nisije nikamwambia rafiki yangu kuhusu habari hiyo mimi nikaona bora nimtonye mwanaume mwenzangu achukue hatua za kujirekebisha fasta ili mambo yasiharibike. Nikamweleza kila kitu, akanishukuru sana na aka ahidi kufanyia kazi kimya kimya na kujirudi

Ilikua siku ya Jumamosi jioni siku kama nne baada ya kumueleza ile issue Big, akanipigia simu kunialika tukapate Ice cream pale Snow Cream na atakua na mama P kama sitojali niende na wife, wazo ambalo tulilikubali maramoja na baada ya kujiandaa kidogo tukaelekea hapo kujiunga na marafiki zetu
Ice cream zilikua tamu sana maana jamaa wa Snow Cream wanajua hasa kuzitengeneza. Katikati ya utamu wa Banana Boat Ice Cream, na mazungumzo na utani wa hapa na pale, Big akanigeukia na kuniambia, "Sesten hebu sema sasa yale maneno uliyoniambia juzi"

Kwanza sikumuelewa ila aliposisitiza na kunikumbusha nikaanza kumsihi kwa kumwambia "George hebu kausha bana. Acha mambo ya kitoto" Lakini jamaa akashikilia niongee na alipoona nimekataa akaimwaga ile stori yoote niliyomwambia ambayo mimi pia niliambiwa na wife kwa sharti la kutomwambia rafiki yangu

Ilikua ni kipindi kigumu sana sana kwangu na nilijisikia vibaya mno. Mke wangu alikua kimya muda wote huku akionekana mwenye kufadhaishwa na hali ile. Mama P alikua kakunja mikono kifuani nae anaangalia tu hali ilivokua

Mwishoe wife wangu akasema anamajukumu mengine anataka kuondoka na mimi nikaunga mkono hoja na licha ya Big kuendelea kusisitiza lazima nielezee yale niliyomwambia tuliondoka eneo lile na njia nzima hatukusemeshana

Usiku ule tayari uliharibiwa na jitihada zangu zoote za kuomba "chakula cha usiku" hazikufanikiwa maana wife alikua anang'ang'ania hajisikii vizuri nimuache. Asubuhi kulipokucha ikabidi nitumie mbinu za hali ya juu kama vile namtongoza upya ndipo nikafanikiwa kupata 'Amka na BBC'

Baada ya pale wife ndio akafunguka kuanza kunisema kwa kitendo changu cha kumweleza rafiki yangu Big mambo tuliyokubaliana tukae kimya. Nilifurahi jambo moja na ndio maana nikataka kwanza nipate haki yangu ya ndoa ili nimlainishe. Wife wangu alikua akikasirika hasemi kitu ananuna tu. Akiaanza kukueleza kosa lako ujue hapo hasira zinapungua, mtafikia muafaka na ndivyo ilivyokua

Baada ya miezi mitano tangia siku nilivyo aibishwa mbele ya wife, mwanamke wa George alikua anavalishwa pete na mwanaume mwingine. Na habari yoote hiyo nilikua naijua hata kabda haijawa critical. Nilikuja kumueleza Big baadae kua nilikua najua kila kitu kupitia wife wangu ila nisengethubutu kufungua mdomo kukwambia, akawa anantumbulia mimacho yake mikubwa tu

Kwa ufupi yule mchepuko wake kumbe ulikua mchumba wa mtu na keshaolewa. Aliyekua wife wake (walikua wanaishi pamoja tu hawakua wamefunga ndoa) keshaolewa na mwanaume mwingine na yeye alikuja kuoa kibinti flani kidogo sana kwake kikawa kinampeleka speed hasa maana kila wakati yupo na company ya vivulana
 
Hahaha sipat picha ulivyokua mdogo ulopoambiwa useme yote


Huyo g naye kama s mwanaume hana kifua, angejirekebisha tu, hata sio mapenzi ni ulimbukeni tu
Kweli kabisa Madame S huo ni zaidi ya ulimbukeni, maana najua hata wewe na shemeji hua mwaongea meengi na mnapeana na ubuyu wa huko duniani lakini naamini yanaishia kwenu tu wala hamyatoi nje
 
Sijui alipewa mambo gani adimu mpaka akaamua kunitosa na kuniuza rafiki yake, labda ni huo ulimbukeni wa mapenzi
Hizo tabia achilia mbali Big kwenye mapenzi yake, hata viongozi waandamizi kwenye taasisi zetu wana hizo tabia.
Mfanyakazi akimletea majungu, badala ya kuyapokea na kuyafanyia kazi kimya kimya, anachokifanya anawaita wote wawili, mleta taarifa ya huyo aliyekuwa anasemwa halafu anaanza "EHE SESTEN ZAKAZAKA NIAMBIE SASA YALE MANENO ULIYOKUWA UMENIAMBIA KUHUSU NAHUJA...."
Ni tabia mbaya kwa kiongozi, yeye anadhani anakomesha majungu kazini kumbe anaharibu. Bora upokee hayo majungu halafu ukauke nayo usiyafanyie kazi
 
Sio kila mtu anakubali ushauri na sometimes ukitoa ushauri kwa wakati usio sahihi ni sawa na bure hivyo basi mkeo ameonyesha anaupeo mkubwa wa kuona mbali kuliko wewe jipange next time utakuja kuiweka familia yako sehemu mbaya
Nakubaliana nawe mia kwa mia mkuu
 
Hizo tabia achilia mbali Big kwenye mapenzi yake, hata viongozi waandamizi kwenye taasisi zetu wana hizo tabia.
Mfanyakazi akimletea majungu, badala ya kuyapokea na kuyafanyia kazi kimya kimya, anachokifanya waita wote wawili, mleta taarifa ya huyo aliyekuwa anasemwa halafu anaanza "EHE SESTEN ZAKAZAKA NIAMBIE SASA YALE MANANEO ULIYOKUWA UMENIAMBIA KUHUSU NAHUJA...."
Ni tabia mbaya kwa kiongozi, yeye anadhani anakomesha majungu kazini kumbe anaharibu. Bora upokee hayo majungu halafua ukauke nayo usiyafanyie kazi
Kweli kabisa maana hapo unajiweka katika wakati mgumu watu watakua wanaogopa kukuletea taarifa ambazo nyingine ni za kujenga na za manufaa kwa taasisi lakini lazima uzipokee kwa namna ya kumlinda mleta taarifa
 
Da! Ilinitokea, niliaibika sana, tangu siku hiyo niliapa kutokuwa na rafiki serious na hadi sasa naaproch mid Forty sijawahi kuwa na rafiki serious
 
Kweli kabisa maana hapo unajiweka katika wakati mgumu watu watakua wanaogopa kukuletea taarifa ambazo nyingine ni za kujenga na za manufaa kwa taasisi lakini lazima uzipokee kwa namna ya kumlinda mleta taarifa
Ni kweli kabisa, marehemu bibi yangu alikuwa anatuasa kuwa, mtu mmbeya tusimdharau, anaweza kukupa siri hata kama kuna watu wanataka kukudhuru, alisisitiza kuwa watu wakimya hata kama anakuona unapita barabarani na huko mbele kuna simba anaweza asikuambie!!!
Pia watumishi wa umma, wanaweza kuwa na taarifa kuwa kuna mgomo unaandaliwa, au hata kuna mpango mbaya wa kuchoma majengo ya ofisi wakakupa taarifa mapema kiongozi wao na ukachakua tahadhari.
 
Hizo tabia achilia mbali Big kwenye mapenzi yake, hata viongozi waandamizi kwenye taasisi zetu wana hizo tabia.
Mfanyakazi akimletea majungu, badala ya kuyapokea na kuyafanyia kazi kimya kimya, anachokifanya anawaita wote wawili, mleta taarifa ya huyo aliyekuwa anasemwa halafu anaanza "EHE SESTEN ZAKAZAKA NIAMBIE SASA YALE MANANO ULIYOKUWA UMENIAMBIA KUHUSU NAHUJA...."
Ni tabia mbaya kwa kiongozi, yeye anadhani anakomesha majungu kazini kumbe anaharibu. Bora upokee hayo majungu halafu ukauke nayo usiyafanyie kazi
Wakati niko o level
Msaidizi wa headmaster,alimpigia simu mwenye shule kumlalamikia kuhusu maovu ya manager na mkuu wa shule

Yule boss alichofanya aliwaita waalimu wote afu anamwambia yule mleta mada HONGEA ULIYONIAMBIA

Jamaa alipata aibu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom