Rafiki yangu kampenda dada mwenye Sickle Cell

KATASAN'KAZA

JF-Expert Member
Jul 24, 2013
3,097
1,352
Napenda wataalamu na watu wenye uzoefu mniambie ni vipi mtu anaweza kumhandle mtu mwenye sickle cell. Huyu rafiki yangu ameambiwa baada ya kuwa tayari kazama kwenye bwawa la mahaba anampenda sana msichana, isitoshe ni kitu matata kichwani, umbo, upole kiufupi wife materials shida hiyo sasa sicklecell, nasikia kuishi kwao siyo garantee jamaa anamwogopa tangu aambiwe hilo tatizo, mtujuze life span yao pia.

Nitanguliza shukrani.
 
Mbona mi namjua MTU ana sickle ni MTU mzima na ana watoto,..sema labda kwa sababu ni ugonjwa wa asili,na wengi nayo wapo prone sana na disease hasa malaria,

Unaweza ishi naye tu,maisha yenyew hayak guaranteed,..
 
Mkuu huyo jamaa mwambie asithubutu kumnyanyapaa kisa ana Sickle Cell.. magonjwa ni mengi skuhizi mwambie hata yeye anaweza pata Heart attack at anytime na akaondoka au akapata Cancer,Ebola, Kisukari au hata ugonjwa mwingine wowote.

Mtaani watu wanawadiss watu wenye HIV alafu wao wanaondoka na pressure daily.
 
Kama huyo shemeji yako ameshavuka miaka 22 basi life expectancy yake ni sawa na ya mtu mwingine wa kawaidia. Kawaida wanasema mtu mwenye sickle cell akivuka miaka 18 basi huwa anakuwa na life span ya kawaida. Lakini mimi napinga hili kwa sababu nilimpoteza rafiki yangu kwa sickle cell akiwa na miaka 22.

Kitu ambacho rafiki yako anatakiwa afahamu ni kwamba sickle cell ni ugonjwa wa kurithi hivyo watakapojaliwa watoto kuna uwezekano mkubwa mmoja wa watoto akawa na sickle cell. Mungu akawabariki na wajukuu, uwezekano wa mjukuu mwenye sickle cell upo pia.

Shemeji yako nahitaji matunzo mazuri na care ya hali ya juu, hatakiwi kuwa stressed maana stress huwa zinawaletea matatizo ya pumzi.
 
Hatumkatishi tamaa lakini anything can happen any time. Pia kuna uwezekano mkubwa wa kuzaa watoto wenye hilo tatizo kwa sababu huo ni ugonjwa wa kurithi.

Umenikumbusha msiba wa rafiki yangu kipenzi aliyekuwa na hilo tatizo.
 
Hakuna MTU mwenye guarantee ya kuishi milele. Kila MTU atakufa. Usimuogopeshe rafiki yako. Kuwa na MTU mwenye seli mundu sio kitu kibaya. Na kuna uwezekano wa kuzaa watoto ambao hawana seli mundu.
 
Dah!! umenikumbusha mkuu kuna mdada nilitokea kumpenda mwaka 2013 nikiwa bariadi na alikuwa na huo ugonjwa wa sell mundu jamani mapenzi upofu niliambiwa kila kitu kuhusu huo ugonjwa kuhusu huyo mdada lakini sikusikia hata kidogo.

Ila baadaye nilihamia mkoa mwingine kutokana na umbali wa mkoa niliokuwa na yeye alikuwa shule sijawahi kupata mawasiliano.
 
Mkuu huyo jamaa mwambie asithubutu kumnyanyapaa kisa ana Sickle Cell.. magonjwa ni mengi skuhizi mwambie hata yeye anaweza pata Heart attack at anytime na akaondoka au akapata Cancer,Ebola, Kisukari au hata ugonjwa mwingine wowote.

Mtaani watu wanawadiss watu wenye HIV alafu wao wanaondoka na pressure daily.
Sawa, ila sasa ndiyo hivyo huu ugonjwa ni kurithi watoto pia wanaweza athirika, inakuwaje hapa??
 
MwanaFA nasikia pia ana sickle cell
Sidhani kama ni ugonjwa wa kuuogopa sana

Ila tatizo linakuja kuwa nasikia unaweza kurithishwa kwa mtoto
Hapo sasa watoto, ingawa lazima wote muwe carriers.
 
Kama huyo shemeji yako ameshavuka miaka 22 basi life expectancy yake ni sawa na ya mtu mwingine wa kawaidia. Kawaida wanasema mtu mwenye sickle cell akivuka miaka 18 basi huwa anakuwa na life span ya kawaida. Lakini mimi napinga hili kwa sababu nilimpoteza rafiki yangu kwa sickle cell akiwa na miaka 22.

Kitu ambacho rafiki yako anatakiwa afahamu ni kwamba sickle cell ni ugonjwa wa kurithi hivyo watakapojaliwa watoto kuna uwezekano mkubwa mmoja wa watoto akawa na sickle cell. Mungu akawabariki na wajukuu, uwezekano wa mjukuu mwenye sickle cell upo pia.

Shemeji yako nahitaji matunzo mazuri na care ya hali ya juu, hatakiwi kuwa stressed maana stress huwa zinawaletea matatizo ya pumzi.
Duuuh! Jamani mbona jamaa nikimwambia haya atamwacha ni mkubwa yuko 22 sasa hivi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom