bernadina
Senior Member
- Jan 22, 2017
- 156
- 64
Sikujua ilo Dada imekaa pouwOook!
Ukipima genotype kuna za aina tatu.
AA, AS au SS
AA- huyu hana kabisa ata chembechembe za sickle cell
AS - huyu haugui sickle cell anaemia ila amebeba chembechembe za sickle cell
SS - huyu ndo anaumwa sickle cell Anaemia.
Sasa
1. AA + AA = AA (watapata watoto wazima wote)
2. AA + AS = AA, AS (Wana chance ya kupata watoto wazima na waliobeba chembechembe za huo ugonjwa)
3. AA+ SS = AS ( Watapata watoto wote waliobeba chembechembe za huo ugonjwa)
4. AS + AS = AA, AS, SS (watapata watoto wazima, waliobeba chembechembe za huo ugonjwa na mgonjwa)
5. AS + SS = AS, SS (Watapata mtoto aliebeba chembechembe za ugonjwa na mtoto mwenye huo ugonjwa)
6. SS + SS = SS (Yaani hawa kila mtoto watakaepata atakua na huu ugonjwa)
(Nimeelezea kwa nilivyofundishwa, sina background ya udaktari... Madaktari wataweza elezea vizuri zaidi)