Mimi binafsi Nina sickle cell, Ila naishi maisha ya kawaida kama waishivyo wengine. Tena najiona Nina bahati ya kuwa ugonjwa mzuri sana ksb ni ugonjwa unaonitaka Nile balance diet muda wote, ninywe Maji ya kutosha, niyale na kuyathamini sana matunda. Kiufupi Nina afya bora. Sickle cell imenifanya nithamini sana kuwa na afya bora kuliko kitu chochote kile.
Ni MTU mzima mwenye watoto wawili, mtoto mmoja karithi anao kama Mimi, Ila mwingine hana. Kupitia ugonjwa huu tumejikuta family nzima tunathamini na ukizingatia sana mlo kamili, mazoezi,Maji, kwa ufupi afya bora. Tunaishi kwa furaha kabisa, changamoto nilizonazo ni za kawaida tu ,ukizingatia kuwa maisha hayakosi changamoto.
Angalia tabia za MTU, Ila kuhusu magonjwa ya kurithi mengine yana changamoto kubwa kikubwa ni kuzingatia masharti ya wataalam na kumwomba Mungu zaidi. Zaidi sana Jikubali ,jipende, jithamini, jilinde, jiombee ili uyafurahie maisha.