Radio Free wakatisha matangazo ya BBC baada ya Padre kufunguka ukweli kuhusu Corona

Kama ni msikilizaji mzuri, basi kukatwa kwa matangazo au maoni hasa yanayokinzana na Serikali ya Magufuli ni jambo lilozoeleka.

Media zimebinywa korodani.
Kweli mkuu yanakatwa sana baadhi ya habari zinazokinzana na serikali yetu, nakumbuka baada ya matokeo ya urais zanzibar kesho yake asubuhi BBC kupitia redio one walikata matangazo baada ya kufika zamu ya maalim seif kutoa maoni yake jinsi uchaguzi ulivyokua wakarudi baada ya yeye kumaliza kuzungumza
 
Corona kweli ipo. Mnataka lockdown au? Huko walikofanya hivyo nini kimebadilika?
 
Muda haujawahi danganya mkuu kuna mtu ataabika dunia itamcheka soon
Mimi nasubiri hao mawaziri wake watakapoanza kuanguka 1 baada ya mwingine, si wanaogopa kuvaa barakoa eti mkuu asije akakasirika wee subiri.
 
Nchi haiongozwi kwa maneno ya media na mitandao.Corona ni ugonjwa kama magonjwa mengine.
 
Lakini tumpe Raisi haki yake:

Angefunga nchi mngelalamika maisha magumu na serikai ni ya ki- dictator

Angetangaza vifo kila siku mngesema anatangaza uongo ili awaonee (au awanyankue nguvu)

Polisi wangekuwa wanagawa kipigo ku-enforce lockdown si mngelalamika

Uchumi ungesimama ni yeye ndo angekuwa analalamikiwa.

Kiukweli Corona haina jinsi:
1. Lockdown imewekwa nchi nyingine lakini bado watu wanakufa (tena strain mpya zimeanza kutokea).

3. Matangazo ya vifo yamefanya watu wapanick na kuua uchumi

Tanzania na Afrika tumezika wengi:
Ukimwi,Malaria, TB, cancer

Kifo hakizookeki ila kama huna jinsi utafanya nini?

Namuunga mkono raisi sema kweli;

Uchumi ndo kinga yetu kwani tukijifungia tutakufa na njaa na magonjwa mengine kabla ya Corona.
 
Kwahiyo unataka tuweke lockdown au tuagize chanjo ulaya?
Sio lazima lockdown ni serikali kukiri janga lipo ili watoe miongozo kama kuepuka misongamano isiyo ya lazima na nje watu wavae barakoa ni kutoa miongozo ya kisheria kuzuia kwa kiasi ila sio lockdown. Kama wakati ule wa kwanza sherehe zilizuiwa wakaambiwa sio wakati wake huu zuia hizi club za ndani za usiku, zuia matamasha makubwa yenye msongamano, unaweza kuruhusu club za wazi za nje ni mambo ya wataalamu kutoa muongozo. Lakini unakuta viongozi imekuwa kusema corona ipo kama crime lakini hata wao wanajuwa ipo sasa makanisani wameanza kusema wazi ipo kama viongozi wa dini ila kumbuka kuna sisi waislamu hatuna viongozi wenye uthubutu wanajulikana njaa kali na uwoga ila wenzetu wanajiamini. Jukumu hili la serikali kuwataarifu watu. South Africa wangeamua kukana na kukaa kimya ingekuwa ni balaa lakini walisema ili wangine wachukuwe tahadhari. Kuna mikataba ya kimataifa kuwa wa wazi katika mambo yanayoweza kuleta maafa kwa wengine. Hii itatucost sana huko mbele hakuna wakutuamini tena huko mbele.
 
Corona kweli ipo. Mnataka lockdown au? Huko walikofanya hivyo nini kimebadilika?
Hakuna mtu anataka lockdown kama hatua za mara ya kwanza hakukuwa na lockdown ila tuliambiwa tuvae barakoa, kuharisha sherehe nyingi tu, shule zilisimama kwa muda yako mambo yakufanya bila lockdown tatizo wanakana hakuna corona wakati huki mitaani hali tofauti hapo ndio shida.
 
Back
Top Bottom