Cetshwayo Kampande
JF-Expert Member
- Nov 28, 2018
- 1,013
- 2,278
Kristo.
Kuhusu wapenzi wa jinsia Moja Papa anasemaje?
Ukweli uko hapa!
"Fiducia suplicans". Ni barua alioandika papa juu ya maana ya Baraka katika uchungaji.
"On the pastoral meaning of blessings"
Katika barua hiyo papa aliandika kujibu maswali ambayo watu wanauliza Sana Kanisa sasa, juu ya msimamo wa kanisa juu ya wapenzi wa jinsia Moja na ndoa za Jinsia Moja. Maana Kila papa katika kipindi chake analazimika kujibu maswali ya kijamii yanayogusa Imani.
Fiducia suplicans n kilatini maanake " n kwamba tusimamie wapi? "On the pastoral meaning of blessing"
Makuhani tusimamie wapi katika maana ya kichungaji ya kutoa Baraka? Papa hazungumzii katika hii barua habari za ndoa ya jinsia Moja, bali Kwa ujumla barua yote anaelezea hasa maana ya Baraka na mapadre watoeje Baraka katika kipindi hiki chenye mchanganyiko wa watu "wema" wenye bidii na pia kipindi chenye maovu yake mchanganyiko.
ANGALIZO
Kwenye hiyo barua papa anatatua changamoto Moja kwamba je mtu huyo mdhambi anaeishi ndoa ya jinsia Moja je anahaki yakubarikiwa?
Hapo hashughuliki hasa na swali eti kubariki ndoa ya jinsia Moja, ameweka wazi kabisa kuwa haifai na haiwezekani.
Kwenye barua anajibu swali kwamba je mtu Mmoja anastahili kubarikiwa? Haisemi abarikiwe kwasabab yeye ni shoga hapana ila kwasabab yeye n mtu.
Kwa maana nyingine je Kanisa liwatenge watu ambao ni mashoga?
Swali hilo limetokea wapi? Huku ulaya nduguzanguni watu hupenda mtu Mmoja Mmoja anakwenda Kwa Padre anamwambia Padre nibariki. Sisi pia huwa mtu unakuta anasafiri anakwenda Kwa Padre, "baba naomba Baraka nasafiri". Padre anambariki. Mtu anapeleka mbegu za kupanda baba naomba Baraka, mwanafunzi anakwenda Kwa Padre baba nimeleta vifaa vyangu vya shule naomba baraka, Padre anabariki.
Watu wakamuuliza papa je mtu mdhambi akimwambia Padre baba naomba Baraka je padre akatae? Aseme Baraka ni Kwa ajili ya watu wema?
Papa akasema Kama akija mtu yoyote akaomba kubarikiwa basi Padre anaweza kumbariki hata kama anaishi dhambi zake kama huyo wa jinsia Moja. Wasibaguliwe kwamba Baraka n ya watu fulan wema
Lakini wasibarikiwe wakiwa wawili kama vile ni wanandoa! Ametoa tahadhari kubwa kuzuia fikra zozote kwamba tunawabariki kama vile Kanisa linaruhusu maisha yao hapana! Ndugu zanguni Baraka sio sakramenti. Ndio maana Padre baada ya Misa anabariki wote hatengi wema zaidi na wakosefu Zaidi. Ila sakramenti sio Kila Mmoja anaruhusiwa. Watu wa ndoa ya jinsia Moja wao pia wamejifungia masakramenti.
Kwa waraka huo Padre anaweza kubariki watu wakiwa katika kundi kama kanisani au kikundi Cha Sala au wasafiri, pia mtu Mmoja Mmoja Padre anaweza kumbariki bila kumuuliza hali yake ya dhambi, hata kama anajua huyo mtu anaishi hali yake ya dhambi Padre ambariki tu. Kwanini maana kupitia Neema za Mungu mtu huweza kubadilishwa pia.
Luka 15:1. Siku moja, watozaushuru na wenye dhambi wengi walikwenda kumsikiliza Yesu. Mafarisayo na waalimu wa sheria wakaanza kunungunika: “Mtazameni mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi, na tena anakula nao.....
Ngoja tuone baadhi ya nukuu kwenye barua hiyo.
Maelezo hayo yapo kwenye barua hiyo "Fiducia suplicans". Sura ya III
"Blessings of Couples in Irregular Situations and of Couples of the same sex". Kiswahili. Baraka Kwa wanaoishi wawili/kama mume na mke katika mazingira yasiyokuwa ya kiutaratib (utaratib kulingana na Kanisa) na ya watu wanaoishi pamoja wa jinsia Moja kama vile ni mume na mke.
Sasa Kwa kichwa hicho Cha habari anasemea sio tu watu wa jinsia Moja bali hata wale ambao hawapo katika ndoa inayotambuliwa kikanisa. Mfano wachumba wasibariki ndoa, wengine wameolewa mitara wote wanahusishwa kwenye kundi hilo. Papa anasema wote Padre anaweza kumbariki tu mtu huyo mkosefu akija Padre ambariki lakin anatoa mkazo isifanyike Baraka rasmi kama vile n sakramenti. Wala wasijisikie kuwa wanahalalishwa hapana.
Nanakuu hiyo barua
No 31. Uwezekano wa kutoa Baraka Kwa watu kama hao......
32. "Indeed the grace of God works in the lives of those who do not claim to be righteous but who acknowledge themselves humbly as sinners, like everyone else.".
"Hakika Neema ya Mungu hufanya kazi katika maisha ya wale ambao hawajidai kuwa wenye haki, lakini wanaojikubali Kwa unyenyekevu wakosefu "
Papa anasema Baraka hiyo ni Neema ambayo Mungu ataitumia kuwaongoa lakini Neema ya Mungu hufanya kazi ndani ya mtu anaekubali Kwa unyenyekev kuwa yeye ni mdhambi. Watu hao wakubali kuwa wao n wakosefu wampe Mungu ushirikiano.
No 33 "This is a blessing that, although not included in any liturgical rite........, "Hii ni baraka ambayo, ingawa haijajumuishwa katika ibada yoyote ya kiliturujia,
No 36 In this sense, it is essential to grasp the Holy Father’s concern that these non-ritualized blessings "kwa maana hii ni muhimu kutambua mtazamo wa baba mtakatifu kwamba hizi baraka ambazo sio rasmi kama zingine za kwenye ibada........ hapa anaonyesha ni za kawaida sio rasmi kama za kwenye liturjia
39. In any case, precisely to avoid any form of confusion or scandal, when the prayer of blessing is requested by a couple in an irregular situation, even though it is expressed outside the rites prescribed by the liturgical books, this blessing should never be imparted in concurrence with the ceremonies of a civil union, and not even in connection with them. Nor can it be performed with any clothing, gestures, or words that are proper to a wedding
39. .......this blessing should never be imparted in concurrence with the ceremonies of a civil union, and not even in connection with them. Nor can it be performed with any clothing, gestures, or words that are proper to a wedding
Baraka hizi zisitolewe Kwa namna yoyote inayoendana na muunganiko kama ule wa ndoa na Wala hata Kwa mfanano zisiendane, Wala zisifanywe kama Kwa mavaz ya ndoa ama ishara au maneno ya kubariki ndoa.
Civil union n msamiati wanaotumia zaidi Kwa watu wa jinsia moja anasema Baraka hizo zisielekee Wala Kwa namna yoyote inayoashiria kitu kama hicho.
Anaependa uisome mwenyewe kwenye mtandao "Fiducia suplicans" kuanzia no 31. Itajitokeza Kwa kiitalianoa lakin mwanzo wa document kushoto kabisa wameorodhesha lugha ya kuchagua bofya " Testo in lingua linglese" itabadilika kuwa Kwa kiingereza.