Radio Free wakatisha matangazo ya BBC baada ya Padre kufunguka ukweli kuhusu Corona

Nkobe

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
2,162
3,162
Katika hali ambayo isiyo ya kawaida kwa sisi wasikilizaji wa BBC kipindi cha jioni. Radio Free wamekata ghafla matangazo ya BBC wakati Padre akielezea juu ya tahadhari ya Corona. Katika mahojiano hayo, Padre alisema kuwa kipindi cha nyuma wao kama viongozi wa dini walikuwa wakiitwa mara chache kuendesha ibada za mazishi, lakini sasa wamekuwa wakiitwa misiba mingi katika Parokia zao.

Baada ya kutamka neno hilo, ghafla Radio Free ikakatisha matangazo na kuwa kimya kwa muda, baada ya hapo wakaja na mada tofauti. Ikumbukwe kuwa Radio zote na Madaktari hawaruhusiwi kusema kuwa nchi ina Corona
 
Hao RFA siku sio nyingi wao ndio watakuwa wa kwanza kutangaza Corona ipo, ngoja imyumbishe mmoja wao watashika adabu.

Huyo Padre amekiri siku hizi misiba mingi lakini kuna viziwi bado hawataki kusikia.
 
Nilifahamu hivyo pale nilipofika ocean road hosp wagonjwa wanahimizwa wavae barakoa wakati madaktari hawavai na ukiingia ofisini unakaa mbali na dr kama una ukoma
 
Back
Top Bottom