Idhaa ya Kiswahili ya BBC London 1991

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,925
30,273
IDHAA YA KISWAHILI YA BBC 1991

Nimetanguliza picha ya Chama Omari Matata ambayo nimeipata kwenye Dira ya Dunia siku chache zilizopita.

Ilikuwa kwenye kipindi cha Dira ya Dunia ambacho Salim Kikeke alituaga wasikilizaji wake kuwa anaondoka BBC baada ya utumishi wa miaka 20.

Nilimjua Chama Omari Matata hapo BBC pamoja na watangazaji wengine kama Ali Saleh, Ali Attas, Suluma Kassim ambae na yeye ameacha BBC pamoja na Salum Kikeke, Ali Adnan huyu akipenda kunyoa kipara kila siku, Aisha Yahya, Eric Munene, Mohamed Abdillah huyu alikuwa kijana wa Kisomali akitangaza Idhaa ya Kiswahili na Idhaa ya Kisomali.

Mwenyeji wangu siku ya kwanza kufika Bush House ilipokuwa BBC alikuwa Ahmed Rajab.

Ahmed Rajab na Chama Omari Matata ni marafiki wakubwa sana na wakajakuwa wazungumzaji wangu na kwa hakika timu yote iliyokuwapo pale Idhaa ya Kiswahili.

Naamini kitu kilichowavutia hawa ndugu zangu ilikuwa namna ya mazungumzo yangu pale tukizungumza siasa za Tanzania.

Majibu ya maswali yao kwangu yalikuwa tofauti sana na yale waliyozoea kuyasikia pengine wakati mwingine wanapowahoji wanasiasa wakubwa wa Tanzania.

Hivi ndivyo nilivyokuja kukutanishwa na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Nelville Hermes (sijui kama napatia kuliandika jina hili).

Nikafanyiwa mahojiano na yeye bila mimi kutambua niko katika mahojiano ya labda kupata kazi ya kujishikiza.

Yote haya mipango ya Ahmed Rajab.
Kilichotokea.

Niliandika na kufanya kipindi katika studio za BBC Glasgow, Scotland.

Kipindi hiki kilipokwenda hewani niliporejea London na kwenda Bush House jamaa wakanisifia kuwa nina sauti ya utangazaji na kipindi changu kiliwavutia sana.

Aisha Yahya akaniuliza kama nimewahi kufanya kazi radio.
Msomaji wangu naamini ungependa kujua Mzee Nelville alisema nini.

Hakika miaka imekwenda.
344821031_548924570771025_600152776467774942_n.jpg

344789868_193749179729806_5126892174000910893_n.jpg

344773184_1016825799334916_6158467993513218676_n.jpg

344913127_246891334497660_2586840327363911620_n.jpg

344765628_1641625466265021_1866885321133364531_n.jpg



 

Similar Discussions

Back
Top Bottom