Radi iliyopiga juzi Dar imeacha hasara ya kutosha

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
11,248
15,432
Juzi jumamosi mida ya asubuhi mvua ilinyesha Dar na around saa tatu hivi ikapiga radi moja kubwa sana kwa wanaokaa pande za goba, mbezi,tegeta A, Msumi, Makabe etc. wataelewa ninachosema.

Radi ambayo ilipelekea umeme kukatika kwa dakika chache tu ila tayari ilikua imeshafanya uharibifu kwenye vifaa vya umeme nikiwemo mimi na majirani kadhaa tuliounguliwa TV. Binafsi natumiaga fridge guard kwenye TV lakini ngoma haikusaidia sababu haikua low voltage.

Nimekaa Dar muda sijakutana na hali hii maana ilikua ni radi ya level ya zile konki za kanda ya kigoma, katavi na Rukwa.

Nimetoka dukani kwa mangi mitaa ya huku nimekuta jamaa wengine nao wanaongelea kuunguliwa TV sababu ya ile radi. Kuna muhanga mwingine humu?
 
Kiongozi naomba elimu kidogo katika hili.
Kwa kawaida kama ilivyo kwa binadamu, umeme unataka kupita katika njia fupi na rahisi kupitika. Umeme hupita katika njia iliyo rahisi kwake kurudi ardhini. Njia pekee inayotumiwa na umeme kurudi ardhini bila madhara yote ni kupitia katika waya ambao kwa lugha ya kiingereza unaitwa Earth Wire na kisha Earth Rod. Mchakato mzima wa kukamilisha ufanyaji kazi wa huu mfumo unaitwa Grounding.

Ikiwa kutatokea tatizo katika waya unaobeba umeme baada ya matumizi(neutral wire), au tatizo lolote la kiufundi ambalo litasababisha ongezeko la ghafla la umeme kutokana na radi kwa mfano, basi earth wire itaubeba umeme huu wa ziada kwenda ardhini. Kwa muunganiko huu wa earth wire na earth rod, ardhi inafikika kirahisi sana na umeme. Maana yake ni kwamba mfumo huu wa grounding una wajibu wa kumlinda mtumiaji wa umeme inapotokea tatizo la umeme.

Ikiwa radi ingepiga katika nyumba yako ingeweza kusababisha hatari katika mfumo wako wa umeme na madhara mengine.

Lakini kama mfumo huo umeunganishwa ipasavyo na mfumo wa earth(Grounding) kiasi chote cha umeme wenye madhara kwa mtumiaji au vifaa vya umeme kitaishia ardhini badala ya kuunguza kila kitu kilichounganishwa katika umeme kwa wakati huo au kumdhuru binadamu.

Sote tunafahamu kwamba ardhi ni kipitisha umeme kizuri kwa asili yake. Na kama nilivyosema awali umeme unapenda kupita katika njia rahisi na fupi, kwa hivyo ku-ground mfumo wako wa umeme ni kuufanya umeme wenye madhara kwako kupata mahali pa kupita kwa urahisi badala ya kwenda ardhini kupitia mwili wako. Hivyo kwa kifupi kabisa, Earthing au Grounding ni kuunganisha vifaa vyako vinavyotumia umeme katika ardhi ya dunia kwa kutumia waya(Earth wire) na fimbo(Earth rod) mara nyingi ya shaba ambayo huzikwa katika ardhi yenye unyevu wa kutosha.
 
Oh nimekuuliza
Kwa kawaida kama ilivyo kwa binadamu, umeme unataka kupita katika njia fupi na rahisi kupitika. Umeme hupita katika njia iliyo rahisi kwake kurudi ardhini. Njia pekee inayotumiwa na umeme kurudi ardhini bila madhara yote ni kupitia katika waya ambao kwa lugha ya kiingereza unaitwa Earth Wire na kisha Earth Rod. Mchakato mzima wa kukamilisha ufanyaji kazi wa huu mfumo unaitwa Grounding. Ikiwa kutatokea tatizo katika waya unaobeba umeme baada ya matumizi(neutral wire), au tatizo lolote la kiufundi ambalo litasababisha ongezeko la ghafla la umeme kutokana na radi kwa mfano, basi earth wire itaubeba umeme huu wa ziada kwenda ardhini. Kwa muunganiko huu wa earth wire na earth rod, ardhi inafikika kirahisi sana na umeme. Maana yake ni kwamba mfumo huu wa grounding una wajibu wa kumlinda mtumiaji wa umeme inapotokea tatizo la umeme.

Ikiwa radi ingepiga katika nyumba yako ingeweza kusababisha hatari katika mfumo wako wa umeme na madhara mengine

Oh nimekuuliza swali kabla sijaona haya maelezo. Ngoja niyapitie
 
Udongo

Umesema Udongo ni kipitishi kizuri cha umeme. Ukitumia tofali za kuchoma kama nyaya za umeme,taa itawaka?

Mfano ukaunganisha betri mbili na tofali moja la kuchoma kisha glopu ukakamilisha circuit,glopu itawaka? Circuit yenye glopu,waya,betri mbili. Ukaamua ufanye tofali kama betri la tatu. Umeme utapita na glopu kuwaka?
 
Kwa kawaida kama ilivyo kwa binadamu, umeme unataka kupita katika njia fupi na rahisi kupitika. Umeme hupita katika njia iliyo rahisi kwake kurudi ardhini. Njia pekee inayotumiwa na umeme kurudi ardhini bila madhara yote ni kupitia katika waya ambao kwa lugha ya kiingereza unaitwa Earth Wire na kisha Earth Rod. Mchakato mzima wa kukamilisha ufanyaji kazi wa huu mfumo unaitwa Grounding. Ikiwa kutatokea tatizo katika waya unaobeba umeme baada ya matumizi(neutral wire), au tatizo lolote la kiufundi ambalo litasababisha ongezeko la ghafla la umeme kutokana na radi kwa mfano, basi earth wire itaubeba umeme huu wa ziada kwenda ardhini. Kwa muunganiko huu wa earth wire na earth rod, ardhi inafikika kirahisi sana na umeme. Maana yake ni kwamba mfumo huu wa grounding una wajibu wa kumlinda mtumiaji wa umeme inapotokea tatizo la umeme.

Ikiwa radi ingepiga katika nyumba yako ingeweza kusababisha hatari katika mfumo wako wa umeme na madhara mengine
Lakini kama mfumo huo umeunganishwa ipasavyo na mfumo wa earth(Grounding) kiasi chote cha umeme wenye madhara kwa mtumiaji au vifaa vya umeme kitaishia ardhini badala ya kuunguza kila kitu kilichounganishwa katika umeme kwa wakati huo au kumdhuru binadamu.

Sote tunafahamu kwamba ardhi ni kipitisha umeme kizuri kwa asili yake. Na kama nilivyosema awali umeme unapenda kupita katika njia rahisi na fupi, kwa hivyo ku-ground mfumo wako wa umeme ni kuufanya umeme wenye madhara kwako kupata mahali pa kupita kwa urahisi badala ya kwenda ardhini kupitia mwili wako. Hivyo kwa kifupi kabisa, Earthing au Grounding ni kuunganisha vifaa vyako vinavyotumia umeme katika ardhi ya dunia kwa kutumia waya(Earth wire) na fimbo(Earth rod) mara nyingi ya shaba ambayo huzikwa katika ardhi yenye unyevu wa kutosha.
Asante Sana kwa elimu kiongozi
 
Back
Top Bottom