Public Debate on Land Grabbing in Tanzania

Public Debate on Land Grabbing in Tanzania

Babylon,

Sasa hiyo habari umeisoma? Wananchi hawataki ardhi yao ikodishwe kwa miaka 99. Unajua yaliyotokea Madagascar?Serikari inaytakiwa iwawezeshe wananchi kutumia ardhi yao sio kuwapa wageni ardhi kwa miaka 99 wakati wananchi wanabaki kuwa wafyeka majani katika nchini kwao.

Wewe unajua maana ya slave plantation?
 
Hivi kwa nini tulimwondoa Mkoloni ambaye alituletea maendeleo makubwa yenye kuonekana hadi leo? Nini haswa sababu ya kumwondoa Mkoloni maanake tuliambiwa alichukua ardhi yetu na kutunyonya...Je, alitunyonya vipi tofauti na huko tunakokwenda leo!
 
Mkuu nadhani tuliwahi sana kuudai kabla hatujaona machungu ya kweli ya ukoloni na sasa tunajaribu kuurudisha! Wasiwasi wangu ni kwamba waliodai uhuru walitumia sababu "kama ulivyozitaja hapo juu" kwa malengo yao binafsi. YANAYOFANYIKA SASA HIVI YANATHIBITISHA HILO!!!

Hushangai mtu kama Kalyalya anaweza kureason vizuri zaidi ya Mawaziri wetu?:angry:
 
Hii ni Good new kwa nchi na wananchi watapata ajira na maendeleo tatizo lipo wapi hapo ?
Watapata ajira based on what? Kwanini serikali isishirikiane na hao wananchi HIVI SASA na kuitumia vyema hiyo ardhi kujiletea hizo ajira na kuongeza kipato? Kaa serikali imeshindwa vitu basic kaa hivi KUNA HAJA GANI YA KUWA NA SERIKALI?
 
Hii ni Good new kwa nchi na wananchi watapata ajira na maendeleo tatizo lipo wapi hapo ?
Watanzania mungu atusamehe hatujui tulitendalo, mtu hujajua hata anakusudia kufanya nini na hiyo ardhi wewe unasema wananchi watapata ajira, hivi unafahamu asilimia kubwa ya maeneo ya vilivyokuwa viwanda vya umma vimebadilishiwa matumizi nje ya makubaliano ya awali na hakuna yeyote anayehoji?

Kiwanda cha ZZK (zana za kilimo kilichopo Iyunga mbeya sasa hivi ni godown la beer ya serengeti wakati hao wanaoitwa wawekezaji wakati wanapewa eneo hilo walisema wataendeleza utengenezaji wa zana za kilimo kwa ajili ya nyanda za juu kusini na nchi kwa ujumla. Mambo yanafanyika kwa uwazi bila kificho chochote.

Tatizo kubwa la nchi yetu ukiwa mzawa hupewi kipaumbele na kwamba sifa za uwekezaji ni lazima uwe mgeni dhana hii inatudhalilisha kama taifa. Kibaya zaidi nchi imejaa viongozi waongo ambao kwa maslahi na visenti wanavyopewa huwa hawahoji chochote mambo yanapokwenda nje ya mikataba iliyokubalika wakati wa kukabidhiana miradi mbalimbali.
 
hivi kwa nini tulimwondoa mkoloni ambaye alituletea maendeleo makubwa yenye kuonekana hadi leo? Nini haswa sababu ya kumwondoa mkoloni maanake tuliambiwa alichukua ardhi yetu na kutunyonya...je, alitunyonya vipi tofauti na huko tunakokwenda leo!

shule ya msingi kuna simulizi iliyosema brown ashika tama,yaani aliporudi bongo na kuona maendeleo tuliyoyapata ukilinganisha na yale aliyoyaacha alishangaa na kushika tama.
 
Hii ni Good new kwa nchi na wananchi watapata ajira na maendeleo tatizo lipo wapi hapo ?

Babylon! You are myopic.

Kwani hawana ajira? Au ukilipwa kila mwezi ndo unadhani ni ajira? Hao ni wakulima, ni wafugaji, ni wachimba madini, wakat mbao, etc. Hizo siyo ajira?

Naelewa sasa hivi tutauza kila kitu ili tupate Bilioni 50 za uchaguzi. Wafanya biashara tumeanza kulazimishwa kuchangia chama. Ukikataa TRA wanafika kuchunguza hesabu zako na kukulipisha kodi zisizoeleweka.

Mpaka tupate bilioni 50!
 
Kwa wale wan jiolojia watakubaliana na mimi kuwa wamarekani pamoja na wengineo wanajuwa "anything that is anywhere" and whatever move they make is definetly a strategic one,kama hatuna viongozi makini ndiyo hivyo...Kwishne!earth geology iko wazi,kila palipo na madini ya aina yoyote panajulikana....Pengine madini ambayo hata kazi yake sisi tunafichwa ama viongozi wetu hawawezi kujishughulisha ili wakati waki negotiate wa include potentiality ya whats below the ground etc,maana sheria ni zina govern tofauti on whats on the groud and whats beneath the ground....Je wametafanyia hayo kazi kabla yahiyo 99 years contract?
 
aliyekwambia kufanya hivi ndo kuuzanchi ninani? do you know what you are talking about?
 
Ala kumbe wewe unadhani kuuza nchi ndio kumeanza sasa?!. Nchi ilishauzwa zamani, mauzo yatakamilika baada ya kipindi kijacho cha 2010-2015 unless otherwise October sote kwa pamoja tuseme basi!.
 
kama tumeshindwa kutumia ardhi, wacheni waje wanaojua kuitumia waje watufunze. mnakula ardhi nyieee. wengi mnakumbuka walipinga sana hata kujengwa mlimani city pale, lakini sasahivi wao ndo wakwanza kwenda kusafisha majicho/macho weekend au kupigia picha wakati wa arusi zao.
 
Hivi kwa nini tulimwondoa Mkoloni ambaye alituletea maendeleo makubwa yenye kuonekana hadi leo? Nini haswa sababu ya kumwondoa Mkoloni maanake tuliambiwa alichukua ardhi yetu na kutunyonya...Je, alitunyonya vipi tofauti na huko tunakokwenda leo!
Mkandara,
Kwa bahati mbaya leo nimeamka asubuhi nikaanza kusoma kitabu cha Kwame Nkrumah: Neocolonialism- the last stage of imperialism.
Kilichonisononesha ni kwamba Nkrumah aliandika kitabu hicho 1965, lakini yanayotokea leo ni kama aliyaona wakati huo. Neo-colonialism is real, na yeyote yule anayefurahia ardhi yetu kukopeshwa wageni kwa miaka 99 eti watatuletea ajira mwambie akazungumze na Red Indians wa Marekani na kilichowasibu.
 
fikra za kiujamaa hazitatufikisha popote, tuingie kwenye full capitalism wajameni, nyerere alitumaliza na propaganda zake, ona hadi sasa bado tunahangaika na upupu aliotumwagia.
 
Mimi nina imani kubwa ndani ya hiyo miaka 99 lazima atatokea kiongozi kichaa kama Idd Amin na kuirudisha ardhi kwa wananchi, na wote waliohusika kufikishwa mbele ya Pilato.
 
Wakuu,
hata hivyo hii hapa-
“Tumepokea maombi kutoka kwa Agrisol na tumeanza kuyajadili kwenye vikao vyetu, kampuni hiyo imeomba pia muda wa kufanya utafiti ili ijue nini kinafaa kulimwa na utafiti huo utachukua miezi sita nadhani baada ya hilo tutajua ukodishaji uwe wa namna gani,” alisema.
Yaani kampuni ya kimarekani inunue eneo halafu lifanyie utafiti?
Kwa upande mwingine nimecheka kuona kichwa kinasema "CCM yaanza kuuza nchi Tanzania"-Samahani lakini sioni ni jinsi gani CCM ikahusishwa na utoaji wa ardhi katika hiyo habari.

CCM ni wakala wa ardhi? Au Siasa tu?
 
fikra za kiujamaa hazitatufikisha popote, tuingie kwenye full capitalism wajameni, nyerere alitumaliza na propaganda zake, ona hadi sasa bado tunahangaika na upupu aliotumwagia.
Hivi leo ukiwaambia Red Indians manufaa ya kuwaaacha wanaojua kuitumia ardhi waitumie watakuelewa? Hata hiyo kapitalizm unayoshabikia msingi wake ni accumulation of capital. Tanzania lini tumeanza kujilimbikizia kapital? Fedha zote zinaishia nchini kwa wawekezaji. Acha fikra za kitumwa.
 
kwa habari ya native Americans (usiseme redi Indians ni offensive kwao), kusema ukweli ni bora mara mia kama kuna watu watakao kuja kuiendeleza nchi hii iwe kama marekani hata kama watachukua ardhi yooooote. leo hii ukimkamata native American umwambie ahame America kwasababu walinyaang'anya ardhi yake hivyo aje hapa tz wewe utampa Kibaha yote iwe yake ailime au awinde etc, hatokubali, anaona modernization iliyofanyika na wageni kule america ni tamu.

Angalia wazimbabwe kama hawalii sasahivi kwamba wazungu wangerudi waendeleze mashamba kwasababu nchi ilikuwa inafaidika na watu walikuwa wanapata ajira, na hela yao ilikuwa inapaaa. Kuna faida gani kuwa na liardhi lote hili na hatulitumii, badala ya kuleta mtu mwenye profession na pesa afanye kilimo cha kisasa au ufugaji wa kisasa na kuweka viwanda kuprocess kile anachoproduce ili kuwapa ajira watz kwenye mashamba na viwanda na kutoa kodo kwenye selikali? na pengine technologia yake itakuwa transfered kwetu....tuache hii protectionism isiyo na faida...wacheni waje tu tena kwa wingi.

As long as kuna masharti kulingana na sheria kwani wakileta za kuleta si unawatimua tu kutumia sheria iliyowaleta hapa?
 
Wakuu,
hata hivyo hii hapa-Yaani kampuni ya kimarekani inunue eneo halafu lifanyie utafiti?
Kwa upande mwingine nimecheka kuona kichwa kinasema "CCM yaanza kuuza nchi Tanzania"-Samahani lakini sioni ni jinsi gani CCM ikahusishwa na utoaji wa ardhi katika hiyo habari.

CCM ni wakala wa ardhi? Au Siasa tu?

uyu mtoa mada inawezekana kasoma Russia, au alishawahi kuishi kule.
 
kwa habari ya native Americans (usiseme redi Indians ni offensive kwao), kusema ukweli ni bora mara mia kama kuna watu watakao kuja kuiendeleza nchi hii iwe kama marekani hata kama watachukua ardhi yooooote. leo hii ukimkamata native American umwambie ahame America kwasababu walinyaang'anya ardhi yake hivyo aje hapa tz wewe utampa Kibaha yote iwe yake ailime au awinde etc, hatokubali, anaona modernization iliyofanyika na wageni kule america ni tamu.

Angalia wazimbabwe kama hawalii sasahivi kwamba wazungu wangerudi waendeleze mashamba kwasababu nchi ilikuwa inafaidika na watu walikuwa wanapata ajira, na hela yao ilikuwa inapaaa. Kuna faida gani kuwa na liardhi lote hili na hatulitumii, badala ya kuleta mtu mwenye profession na pesa afanye kilimo cha kisasa au ufugaji wa kisasa na kuweka viwanda kuprocess kile anachoproduce ili kuwapa ajira watz kwenye mashamba na viwanda na kutoa kodo kwenye selikali? na pengine technologia yake itakuwa transfered kwetu....tuache hii protectionism isiyo na faida...wacheni waje tu tena kwa wingi.

As long as kuna masharti kulingana na sheria kwani wakileta za kuleta si unawatimua tu kutumia sheria iliyowaleta hapa?
Wee unayasema haya umewahi fika Marekani au unazungumza tu ili mradi kufurahisha baraza. Wee kweli unayafahamu maisha ya hao wahindi wekundu au? nakuonmba google kisha rudi tuendelee na mjadala.
 
Wee unayasema haya umewahi fika Marekani au unazungumza tu ili mradi kufurahisha baraza. Wee kweli unayafahamu maisha ya hao wahindi wekundu au? nakuonmba google kisha rudi tuendelee na mjadala.

saa hizi hapa ninapoandika Tanzania ni saa tisa za usiku, na mimi sijalala, unafikiri ningekuwa Tz ningekuwa macho mida hii? that means, niko kwenye nchi ambayo kwasasa watu hawajalala, sitakwambia nchi gani, ila siku tz...wewe tu ndo umefika marekani, and so what? kwani ndo mbinguni huko? watu tumetembelea hizo nchi hadi tumechoka... sijafika marekani, nimeishi marakani. unasemaje hapo?
 
Back
Top Bottom