Unajua wanafanya kama mchezo wa karata tatu.. binafsi ningependa kuwajua hawa wenye mashamba wasioyaendeleza ni kina nani? Maana wanaweza kuwa walibinafsishana wenye in 1990s kwa bei chee halafu leo wana flip kwa bei ya juu na wanatoka bado winners..
Mzee umenena! Si unajua hata Sumaye na kale kamgogoro ka shamba kule Morogoro, na Mh BWM kule Mtibwa na Kilombero nako nasikia aligusagusa pia. Tena kule Kilombero alifanya kama huyu anavyotaka kufanya, walitangaza shamba likauzwa bahati mbaya sio kwa waliyemtaka. Sasa baadae wakamnyang'anya wakasema wanampa wananchi. Wapi bwana! akakatiwa Mh mmoja wa Ikulu ekari 500 na zingine zimebaki hivi tangu enzi hizo 1997 au hivyo. Huyu mwekezaji amekuwa akidai arejeshewe ile hela aliyolipia hilo shamba hadi leo, kesi iko mahakama kuu. Lakini huyu mkulu ndio supplier mkubwa wa miwa kule Kilo Sugar kwa sasa hivi, anaongoza outgrowers (oh ngoja nimeshanganya michuzi hapa! lakini ndio demokrasia na utawala bora wetu)
Mahali pengine kule Moshi, yuko njemba mmoja ilipewa sehemu ya shamba iwekeze mradi wa hotel, tangu 1992, lakini hadi leo hajalipa kodi kwa chama cha ushirika ambacho ndio mmiliki wa shamba lile, na zaidi ya hapo, serikali yenyewe kupitia waziri wakati ule Rita walifanya kila mbinu ili apewe hati amiliki kasehemu kale ka shamba, bila ridhaa ya wananchi wale. Bado hii ni kesi inayoendelea. CCM ndio wamekuwa watetezi wakubwa wa huyu mwekezaji. Mwekezaji anadai alikuwa analipa kodi, kwani kila mara viongozi walimletea shida zao kama ada za watoto wa shule na alilipa. Utawala bora hapa bado...
Nimetoka sana kwenye mada lakini watakaokuwa wanamiliki haya mashamba ni hao na watalipwa cha juu zaidi. Kama yule Bw pale Kilombero akiambiwa awaachie wananchi lile shamba afidiwe, atakuwa amefaidi sana maana kwa sasa hivi ni tajiri, na shamba lile likithaminiwa sio haba kwake hata kidogo.
MMJ nimekuunga mkono kwa kwenda kando, mbele, nyuma na mbele, ndio mwondoko wa siku hizi mzee!