Public Debate on Land Grabbing in Tanzania

Huu mradi kwa manufaa ya nani haswa?Hawa Viongozi wetu watatupeleka pabaya!,wamekuwa walafi mno kwa kujali matumbo yao binafsi na kuwaacha wananchi wa kawaida maskini!.Hivi kweli tumefikia wakati wa kuhitaji Green Ethanol?kwa magari gani tuliyonayo?Hapo kuna pesa za nje nje na sasa viongozi wetu walafi akina Karamagi wameanza kutolea macho.Tumeshindwa kutoa huduma muhimu kwa wanachi kama matibabu na Elimu,sasa tunataka kuwapokonya na Ardhi?
Wanavijiji wa huko Bagamoyo na Rufiji ni vigumu kuwaelewesha hili jambo wakalijua vizuri(walio wengi upeo wao wa uelewa ni mdogo),bali watakubali kupewa pesa kidogo na kutafutiwa sehemu kame wakaishi.
Ni wakati sasa wa kuwapigia kelele Viongozi wetu waache kufikiri kuwa kila uwekezaji utainufaisha Nchi.Hakuna kosa baya tutakalofanya kama hilo la kuuza ardhi yetu!Hao wawekezaji wawaelimishe wananchi na kuwaelekeza kilimo hicho cha miwa ili Wana-Rufiji na Bagamoyo wapate pesa kwa kuuza zao hilo kwa hao wawekezaji.
Kwa mara nyingine nakupongeza Mzee Moshi kwa Taarifa hii.Kuna kila sababu ya kuzungumza na Magufuli kuhusu mradi huo haramu.
 
Mwawado Good points,

Nafikiri bwana Moshi ameleta point ya maana hapa na jamaa wanafuatilia kuona wasomi JF wanasemaje. Kama tutalaza damu jamaa watawahamisha wandengereko na kujichukulia 40,000 hecters. Kama kweli ni mainvestor then wawafungulie wananchi mashamba na kuwapa impliments then wanunue kutoka kwao. Mimi nafikiri jamaa wameshajua kuna mafuta. Hivi hakua mageologist humu ambao wanakuwa nao field wakati wa exploration watuambie hau huwa wanafungwa midomo kwa kitu kidogo!!!!!
 
Wajameni, huu ndiyo wakati wa kuwatetea watu wa Rufiji na Bagamoyo before it is too late. Wakati MKJJ anaomba marehemu AC awe freed watu mlikuwa busy mnatafuta majungu kama Bro Z alifanya mavitu leo amekufa mnaanza kumtafuta mchawi mpaka evidence za picha JK alikuwa wapi. Sasa kesho mkisikia Rufiji na Bagamoyo zimeuzwa then msilalamike because the time to stop this is now. Please work up guys!!!!
 
I am concerned, very concerned, about the bones of my ancestors. It so happens that my ancestors are buried on the slopes of Mount Kilimanjaro, and there is every possibility that the government will one day either rent out or sell the whole area, to an investor. It would appear that they are already in the process of renting out most of the Lake Eyasi area to some hunting company from the UAE. I have attached below an article that alludes to just that.

At one level, I am mightily amused. Why lease out that land to a hunting firm while it is already inhabited by the Hadzabe, who are great hunters? The Lake Eyas area is already full of hunters, namely the Hadzabe people. Why lease it out to a foreign hunting firm?

Now, once Lake Eyas is leased off (or sold off, whichever comes first), what will they sell next? I am afraid that it will be Mt. Kilimanjaro. That would be awfully attractive to any investor. But then, what would such an investor do to the bones of our many ancestors who are buried there?

Augustine Moshi
=============================================
The article below is taken from http://www.arushatimes.co.tz/mailbag.htm

Plight of the Hadzabe Tribe of northern Tanzania
Dear Editor

I am writing regarding the reported effort by members of the United Arab Emirates' royal family to purchase rights to land in the Lake Eyasi region of northern Tanzania. I am greatly concerned that this deal will adversely affect members of the Hadzabe (Hadza, Watindiga) tribe who make their homes
in the area.

Reports are that the Hadza were not consulted on this issue and that they will effectively lose their right to subsistence hunt. Media reports have further painted the Hadza as primitive or savage in an effort to culturally excuse the effort by the UAE and Tanzanian government to deny
the Hadza their traditional homeland. I find it ironic that these governments would invoke the same language of cultural division used by every conquering society throughout history as justification for taking
tribal land away from native people. I would ask if members of either government (UAE or Tanzanian) see any connection at all with their current behavior toward the Hadza and the Arab expansion, conflict and slave trade across East Africa in the 15th and 16th centuries.

The Hadza want nothing more than to continue their traditional cultural practices within their traditional homeland. The efforts of the rich to seek their own pleasure at the expense of those wishing only to practice their traditional culture amounts to a human rights tragedy of epic proportions.

This travesty has not gone unnoticed amongst the internet blogging community and word is spreading worldwide quickly. I implore both the UAE and Tanzanian governments to cease further consideration of selling or leasing Eyasi region land instead take legal steps to insure that the Hadza may continue their cultural traditions without interference.

Concerned Human Rights Activist
 
Kuhusu Balozi aliyesema tunahitaji ethanol naomba nijibu hivi:

Hatukatai kulima miwa. Ila tuilime kwenye ardhi yetu. Mwekezaji anachohitaji ni miwa au ardhi? Kama ni miwa basi tushirikiane naye tulime miwa, na tuwekeane mkataba wa kumuuzia yote. Tutampa vile vile sehemu kidogo ya kujenga kiwanda chake, na viekari vichache vya kwake vya kulima mboga kidogo kwa ajili ya chakula chake na watoto wake (ili asiwe amekosa kabisa ardhi).

Mabalozi wanatetea maslahi ya wananchi wao. Balozi wa Sweden lazima atatetea maslahi ya mwekezaji toka Sweden. Nani anatetea maslahi yetu?

Augustine Moshi
 
Hapa chini nimeambatanisha makala inayosema amekuja mwekezaji toka Uingereza ambaye anataka apewe ardhi kiasi cha hekta 20,000. Serikali tayari imempangia ardhi kiasi cha hekta 9,000. Ni ardhi kubwa ajabu.

Swali ni hili: hawa wanataka ardhi au wanataka jatropha? Kama ni jatropha, basi kwa nini wasishirikiane na wananchi waioteshe kwenye ardhi yao, hata hekta laki nzima, na wainunue kwa bei ambayo watakubaliana kwanza?

Ukimpa mtu hekta 20,000 toka Kisarawe zitakuwa zake milele! Na atakachofanya ni kuajiri watu wa Kisarawe wawe manamba wake milele, wawe wanakaa pemebeni pembeni mwa ardhi yake na kupata makombo toka kwake.

Mbona tunakuwa wepesi hivyo kugawa urithi wetu wa ardhi? Bei ya hekta 20,000 za ardhi nzuri ya Kisarawe itakuwa ipi miaka 20 ijayo?

Tusipoangalia, wazee wetu wenye heshima zao na mali nyingi ya ardhi sasa watakuwa tu ni vibabu manamba wa masetla miaka michache jayo.

Augustine Moshi
========================================

Kisarawe land compensation `stalls` Jatropha project

2007-08-08 14:39:35
By Patrick Kisembo

Tanzania Investment Centre (TIC) has said there was still a long way to go before they allocated investors with land at Kisarawe, in Coast Region, for the Jatropha project.

TIC director general Emmanuel Ole Naiko told The Guardian on Monday while responding to a question on allegations that the amount set for compensation was too small for the ten villages in the area.

Ole Naiko dismissed the claims, saying it would take time before they completed procedures for the project.

He said villages and the council had done their part and what remained was for the TIC and other responsible authorities to send the proposals to the minister for Lands, Housing and Human settlement.

``The president has the mandate to declare the area as general land. The request is yet to go to him for processing, `` he said.

The TIC chief further declared that the Member of Parliament for Kisarawe, Athman Janguo, was still working on the issue.

``The investor requested for 20,000 ha but we have allocated him with 9000 for Jatropha citrus farming,`` said Kisarawe district council chairman Omari Dibibi.

For his part Ole Naiko said the amount of compensation was normally known after all the processes of acquiring land had been completed.

Recent reports had it that a foreign company, Sun Biofuels Tanzania Ltd, had set aside 826m/- for compensation for residents in the ten villages in Kisarawe District.

It was learnt that if 800m/- was to be given to the 4000 residents in the ten villages, assuming that each village had about 400 residents, each resident would get less than 200,000/- as compensation.

Kisarawe District Council chairman Omari Dibibi was quoted as saying that the company had set aside 826m/- as compensation.

He said 800m/- had been set aside to compensate residents while 26m/- would go to TIC and the district council.

``Payment of compensation would be made after evaluation of crops and land in the ten villages,`` he had said.

The villages in question are Mtamba, Chakenge, Mtakayo, and Kurui-Mzenga.

Others are Mitengwe, Mzenga, `A`, Kidugalo, Marumbo, Palaka and Muhaga.
  • SOURCE: Guardian
 
Hawa watu waambiwe hakuna ardhi inayouzwa tutawalimia hayo majetropa yao wao walete vifaa ambavyo vitalipwa na walima jetropa kwa bei ya makubaliano.

Ardhi ilichukuliwa 1967 sasa hawa viongozi vilaza wanafikiria matumbo yao.
 
I am confused! Hivi twaweza fanya nini zaidi kuhakikisha huu umafia wa ardhi yetu hautokei?

Hii inatisha sana! mbona kasi ya uuzaji/ugawaji imekuwa kubwa namna hii? na kwaninini maeneo makubwa kiasi hicho?
 
Kuna haja ya kuzungumzia pia ununuaji mkubwa wa ardhi unaofanywa na Wapemba na Waunguja hapa bara. Sidhani kama nalo lina mwisho mwema kwa vizazi vijavyo vya huku bara!
 
Kuna haja ya kuzungumzia pia ununuaji mkubwa wa ardhi unaofanywa na Wapemba na Waunguja hapa bara. Sidhani kama nalo lina mwisho mwema kwa vizazi vijavyo vya huku bara!

Hivi nini hasa Tatizo la Viongozi wetu jamani? Wanawaza ni vichwani mwao? Huwezi kuamini hata kidogo yanayotokea katika nchi yetu.?

Kama kuna mtu aliaminika sana klwa watanzania alikuwa Bw. JK lakini kwa kweli Tuendako, anaweza akawa ni rais mbaya tutakayoikuwa tumempata mpaka mwisho wa ulimwengu huu.

Yaani serikali hii na wananchi ni kama MBINGU na ARDHI.

Ee mungu tuepushie balaa hili
 
Waunguja na Wapemba ni Watanzania. Wana haki ya kuwa na ardhi (kiasi wanachoweza kuendeleza, si zaidi) popote Tanzania, kama ilivyo kwa Watanzania wengine.

Wapemba na Waunguja wanafanya shughuli za maduka, teksi na uvuvi bara, kama Watanzania wengine. Si vema tuwatazame tofauti na kusema hawa ni Waunguja au hawa ni Wapemba. Ni Watanzania kwanza, na Uunguja au Upemba ni baadaye sana.

Kama Mpemba akitaka ardhi mahali ilipo nyingi, basi apewe na kijiji, asiuziwe. Na popote pale, kama kuna mtu amejichukulia ardhi kubwa kiasi ambacho hawezi kuendeleza, basi ardhi ya ziada inarudi kijijini.

Tatizo ni hawa wageni wanaokuja na "KUTAJA" kiasi kikubwa cha fedha za uekezaji, na kwa njia hiyo kujichukulia ardhi kubwa sana ambayo vijiji havina mamlaka nayo tena. Na wanachagua sehemu ambazo zinaelekea kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta! Utampaje mtu hekta elfu 20 sehemu ambayo imegunduliwa gesi, na inaonyesha uwezekano wa kuwa na mafuta?

Augustine Moshi
 
A Norwegian cement company wants to evict an estimated 3,000 Tanzanian farmers it says are trespassing on its land.

The farmers say their families have lived there for generations, and that they were not consulted when the land was sold. After 16 years of conflict Tanzania's highest court is due to reach a verdict soon.

habari zaidi http://allafrica.com/stories/200804180421.html
 
A Norwegian cement company wants to evict an estimated 3,000 Tanzanian farmers it says are trespassing on its land.

The farmers say their families have lived there for generations, and that they were not consulted when the land was sold. After 16 years of conflict Tanzania's highest court is due to reach a verdict soon.

habari zaidi http://allafrica.com/stories/200804180421.html





Mama, I hope this is just a bad joke. I read the full story, but I'm still dumbfounded.
 
Magazeti ya leo yana taarifa kwamba makampuni ya nje kiasi cha arobaini yametaka kupata sehemu kubwa za ardhi katika bonde la Mto Rifiji, kwa ajili ya biofuel production.

Kampuni moja, SEKAB BioEnergy Tanzania, linataka hekta laki nne. Tayari limeshaendeleza hekta elfu ishirini, na zingine hekta elfu hamsini ziko kwenye matayarisho.

Sasa kampuni kama hizi huwa zinapewa ardhi (ownership) kabisa. Na ardhi ya bonde la Rufiji tayari imeshagundulika ina gesi, na uwezekano wa kuweko mafuta ni mkubwa. Sasa ukimmilikisha mtu hekta laki nne zenye mafuta au gesi ili aoteshe mazao ya kutoa mafuta ya kuendeshea magari ni busara? Kwa nini tusitumie gesi iliyoko chini ya ardhi, na ambayo ni mali yetu, kuendeshea magari?

Ukishammilikisha mgeni sehemu kubwa ya ardhi yako unadhani kukipatikana mafuta baadaye atakubaki kuirudisha? Kumbukeni hawa wawekezaji Tanzania wanahakikisha kuna kipengele kwenye mkataba kisemacho mahakama za Tanzania hazina uwezo juu ya mikataba yao. Ni mpaka London.

Wangejitokeza watu kulima mchele kwenye mashamaba ya hekta elfu kumi kumi singejali. Hawa wanaotaka kulima miwa kwa ajili ya biodiesel wakati chakula hatuna wananiogopesha.

Ardhi ni mali. Msiuze urithi wetu. Kama ni lazima kutoa ardhi, basi kiweko kikomo cha hekta elfu kumi. Kwa vingine, watoto wetu watakosa ardhi, na watakuwa manamba wanaolima miwa kwa wageni.

Tunauza future ya wanetu.
 
implication ya kuuza haya maeneo ni kubwa sana kwani ukishamuuzia mtu yeye ndo anayeamua alime nini, mkumbuke kuwa mabonde haya ndo yanazalisha 80% ya chakula cha watanzania lakini kuna mwekezaji mmoja wa bonde la kapunga aliuziwa ili alime mpunga lakini ameacha kulima mpunga analima Mibono.

Tutegemee njaa zaidi kwa kuwa priority zimebadilika
 
Augustine heshima mbele Mkuu.... Yaani sijui tunapoenda ni wapi? Rufiji nayo imo??? Molla atuepushe na haya maamuzi yasiyo bora.... Hebu imagine hii, juzi nilikuwa Manyara kujaribu tafuta kihamba cha kujifanyia kilimo.... Nilienda na kuongea na wenyeji wakasema yale mashamba makubwa ya zamani NAFCO etc yanauzwa/kugawanywa kwa watu wenye mitaji/madau makubwa.... Nikawaambia hata mimi nahitaji kihamba na ninazo pesa, wakasema ninataka heka ngapi nikasema 200..... Jamaa wakasema kule wanaoongea ni wale wenye kutaka heka kuanzia 10000 nikarudi zangu Dar manake kwa mtaji ule nadhani sisi wanyonge tubakie kuajiriwa tuu......

Sikatai watu kuchukua mashamba makubwa lakini kama Mkuu Augustino na Jamco.... walivyosema hapo juu, hao so-called wawekezaji wakubwa wanaishia kulima bio-fuels na mibono, duuuh, chakula je??

Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.............
 
Augustine Moshi

Heshima mbele mkuu hii nafikiri ingeunganishwa na ile uliyoiweka mwaka jana kuhusu swala hili. nashangaa hata wabunge bado wako mabubu kwenye swala hili. Bunge linaanza hivi karibuni lazima kieleweke nini kinaendelea huko.
 
Dua, Moran75, BabaH, Jamco_za na wandugu wengne mnaojua kwamba ardhi ni mali. Tena niseme kabisa kwamba wamechukua Rufiji Delta, ambayo ndiyo sehemu nyeti kuliko zote ya Bonde la Rufiji.

Kama alivyodokeza BabaH, yuko mtu kapewa sehemu alime mpunga lakini badala yake kalima mibono (hivi mibono ni nini, BabaH?). Sasa nionavyo ni hivi: hawa wageni wanaotaka hekta 400,000 watalima kwa muda kidogo, kama changa la machoni. Baadaye watauza sehemu hizo kwa makampuni mengine kwa ajili ya shughuli mbalimbali. Tukumbuke ni wajanja hawa. Dunia imekuwa ndogo. Wanataka ownership ya sehemu nzuri nzuri za dunia kabla ya walioko huko hawajaamka.

Thamani ya hekta 400,000 za Rufiji Delta itakuwa kiasi gani miaka 20 au 50 ijayo?

Moran75 ametaka kihamba cha ekari 200 huko Manyara amekosa. Na hela ya kuzinunulia alikuwa nayo mfukoni. Kaja Mzungu kataka hekta 400,000 (yaani kama ekari 988,400) za sehemu nzuri sana ya Tanzania, yaani Rufiji Delta, kapewa. (Angalao tumeambiwa kwamba tayari hekta 70,000 za mwanzo anazishughulikia). Damn! wapeweje ekari milioni? Nijuavyo ni kwamba hata Bush hana 1% ya hiyo huko kwenye ranchi yake Texas!

Sasa tufanyeje? Mbona ukoloni unarudi? Itabidi tupiganie UHURU upya?
 
they "foreigners" can never own the land by law, its a lease...sioni tatizo kwa wawekezaji ku invest huko na siyo kubaki kulima mihogo tu, naungana na wewe on the point that some joint venture be formed ili kuwashirikisha wenzetu huko nao wajifunze biashara na kilimo cha kibiashara huko. kila mtanzania ana haki ya kukodisha ardhi yake au kumuuzia mtanzania kwa bei yake. kama inawauma, nendeni huko pwani mnunue hiyo ardhi kutoka kwa hao watu wa pwani ili kuwazuia hao investors. au nendeni mkawafundishe huko pros and cons of business.
 
Hivi hatujajifunza lolote ni kwa nini nchi kama vile Zimbabwe Namibia Afrika kusini zina tatizo la ardhi? Granted wazungu waliichukua hiyo ardhi kwa mabavu na kuwafukuza Waafrika. Lakini hili limeanza kujitokeza Tanzania ambako serikali inayoongozwa na Waafrika wenyewe inawaalika wazungu na kuwapa ardhi kwa visingizio vya uwekezaji.Hii imeshatokea kwenye maeneo ya madini na sasa inaanza katika bonde ma mto Rufiji ambalo ni kitovu cha uhai wa Tanzania. Miaka 100 ijayo vitukuu wetu watakuja kumlaumu nani?
 
Back
Top Bottom