Ndugu zangu, kama nyinyi kwa mtazamo wenu mnaona wawekezaji wanachukua urithi wenu kwa wanakijiji sio hivyo. Kwa wanakijiji wa maeneo ya Kisarawe kulikotolewa ekari elfu tisa wanasumbuliwa sana na wadudu waaribifu wa mazao hasa nyani na nguruwe. Usipokaa kulinda shamba lako ndugu yangu utavuna mabua na mihogo utapata.
Kwa wakulima huyu akilima eneo hilo lote maana yake nyani na nguruwe wameamishiwa mbali na shamba lake, atapata mazao bila kulinda shamba. Kwa kipindi kirefu watu hawa hata kulima ilionekana ni kupoteza wakati maana yataliwa na nyani na nguruwe.
Ndugu zangu wana JF kilimo mumewachia wakulima, wakulima ambao kwa mtazamo wa wengi ni watu duni wasioenda shule, watu wanaolaliwa na wafanyabiashara na kuendelea kuwa duni miaka nenda miaka rudi.
Ndio maana mtu akitaka kusema ametoka kwenye familia maskini anaseme yeye mtoto wa mkulima, huo ndio mtazamo wetu na ndivyo tulivyowaweka wakulima wawe.
Wengi wetu tunajua kuwa mtu akistaafu anaenda kuanzisha shamba, nani aliyetupa mawazo haya kuwa wasio na nguvu wanaosubiri kufa ndio wakawe wakulima. Wengi wetu humu ni wafanyakazi na mawazo yetu yanaweza kuwa ya namana hiyo hiyo kuwa utakapostaafu ndio ukawe mkulima ukisubiri miaka yako michache iliyobaki kabla ya kufa shambani. Huu ndio ujinga nambari wani wa wafanyakazi wengi wa Tanzania. Yeyeto ambae alimi chakula na yupo hapa nchini aanze kutafuta shamba vijijini.
Ndugu zangu, unapokuwa na shamba kijijini na kwenda kulima uendi kulima tu bali unafundisha kwa wanakijiji kuona unafanya nini, kwa mazungumzo pamoja nao na hata kuwapa matumaini ya wapi wanapaswa kuangalia na kujua waendako na kupanga maisha yao.
Ndugu zangu, mnachopaswa kujua ni hili mtu mmoja maamuzi yako yanachukua muda mfupi kuliko serekali. ukiamua kulima leo, kesho utakuwa shambani. Sina kipimo cha serekali itachukua muda gani ila ni muda mrefu kuliko mtu binafsi. maana kuna kuandaa dokezo halafu kabrasha, halafu semina elekezi, hakafu kongamano, halafu uamasishaji wakati wanaanza kulima mtu bibafsi utakuwa umevuna mara tatu au hata mara tano.
Ndugu zangu kama kweli mnataka maendeleo ya nchi hii nendeni mkalime, sio kuchukua mapori na kutufugia nyani na nguruwe. Sina hakika ni darasa lipi kama si la tatu basi la nne wakati wetu kulikuwa na shairi "Karudi baba mmoja.........., watu wa enzi zangu mnakumbuka.
Ukweli ndio huu aridhi ya kilimo Tanzania ni kubwa tunachopaswa kufanya Watanzania wenyewe ni kwenda kulima, usipolima ndugu yangu watalima wazungu.
Unalalamika wanapewa ekari nyingi wewe una eka ngapi? Nashukuru kuna mtu ametupa moyo kuwa alikuwa anatafuta ekari mia mbili za kilimo, huyu hayupo mbali na ufalme wa Mungu.
Kama mnataka aridhi isuzwe kwa urahisi na nyinyi muwepo katika kundi la wanakijiji sio kuwaacha peke yao mtazamo usio mzuri, ukiwepo waweza kuwapa mtazamo sahihi. Chukua shamba lima ufukuze nyani na nguruwe ili tupumzike kushinda mashambani kulinda mazao yetu.