PSPF hatarini kufa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PSPF hatarini kufa

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by shadhuly, Mar 26, 2011.

 1. s

  shadhuly Senior Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Saturday, 26 March 2011 09:56

  Exuper Kachenje

  KATIKA kinachoonekana serikali inachangia kuzorota kwa mifuko ya hifadhi ya jamii, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imelezwa kuwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Mashirika ya Umma (PSPF), unaidai serikali Sh3.1 trilioni.

  Maofisa wa PSPF walifika mbele ya kamati hiyo jana, walieleza kuwa taarifa zake za ukaguzi wa hesabu zinaonyesha mfuko huo upo hatarini kufa.Habari kutoka ndani ya mkutano huo, zinadai PSPF ililalamika kuwa deni hilo limechukua muda mrefu na kwamba, Serikali haikuwa imeonyesha juhudi zozote za kulipa.

  Hata hivyo, akitoa muhtasari wa kikao kati yake na PSPF, Mwenyekiti wa Kamati ya POAC, Zitto Kabwe, alisema uwapo wa mfuko huo unahatarishwa na deni lake kwa serikali.

  "Asubuhi tulikuwa na mkutano na PSPF na tulimwita pia Katibu Mkuu Wizara ya Fedha. Niseme, PSPF uwapo wake unahatarishwa na deni lake kwa Serikali," alisema Zitto na kuongeza:
  "Auditor (Mkaguzi wa hesabu) aliyekagua hesabu za PSPF anasema mfuo huo utakufa."
  Alithibitisha kuwa serikali inadaiwa fedha hizo na PSPF, lakini akasema kwamba kamati yake imechukua hatua kadhaa kurekebisha hali hiyo ili kuuokoa.

  "Serikali inadaiwa Sh3.1 trilioni, lakini Kaimu Katibu Mkuu Hazina alikuwapo naye akaeleza yake, sisi tukatoa maagizo yetu kama kamati," alisema Zitto.

  Alisema baada ya taarifa ya mfuko huo kwa kamati yake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk Servacius Likwelike, aliyekuwapo katika mkutano huo alieleza kuwa, jana serikali imeanza kulipa deni hilo.
  Kwa mujibu wa Zitto, Dk Likwelile aliiambia kamati yake kuwa, serikali imeandika hundi ya Sh5.9 bilioni kwa mfuko huo kama malipo ya awali.

  Kutokana na hali hiyo, Zitto alisema kamati yake imewaagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, kuchunguza ili kujua kama kweli fedha inayodaiwa serikali hiyo au zaidi.

  Katika hatua nyingine, kamati hiyo imetoa mwezi mmoja kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia Wizara ya Fedha, kufanya tathmini ya mchakato wa uuzaji Kampuni ya Zain kwa wamiliki wake wa sasa Airtel ya India ili kufahamu upungufu wa kisheria uliokosesha serikali fedha.

  Pia, kamati hiyo imetaka TRA kutuma timu ya wataalam nchini Nigeria, kujifunza ilivyofaidika na uuzaji wa Kampuni ya Zain wakati Tanzania ingeweza kunufaika na zaidi ya Sh308

  SOURCE MWANANCHI
   
 2. MduduWashawasha

  MduduWashawasha JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 1,568
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Trillioni zote hizi kwa serikali hii ! Watanzania tujiandae kwa disaster kubwa
   
 3. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sasa naanza kupata mwanga kwa nini nasumbuliwa na mafao yangu. Tangu mwezi june 2010 nimekuwa nikifuatilia mafao yangu mpaka niandikapo ni njoo kesho jaribu baada ya week 2 na hivi navile. Mara faili lako limekwama mahali fulani na huyo mhusika yuko safari mpaka arudi. Kumbe serikali imejichotea jasho letu na kutumia kwa manufaa yao.
  Serikali itaendelea kutesa wananchi wake hadi lini?
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hii mifuko ya hifadhi ya jamii ilishashauriwa kufanya kitu inaitwa acturial ili kujua uhai wake ukoje na wengi walipuuzia na matokeo yake ndio haya. wakati mwingine waendeshaji wa mifuko hii nao wanaingiza sana siasa. sasa inakuwa mpaka deni linafikia trilioni zote hizo na wao wapo tu wanaangalia? Kulalamika kwenye kamati ya bunge haliwezi kuwa suluhisho la mattaizo yao na hili wanalo. sasa wajiandae kukabiliana na hasira za wanachama wao
   
 5. Panga La Shaba

  Panga La Shaba JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2011
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 209
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwanza hii mifuko imekuwa mingi sana,sioni mantiki yakuwa na mifuko mingi hivyo,kwa mfano kwasasa hakuna tofauti kati ya PPF na NSSF wote wanagombea wateja hao hao........mimi nafikiri lingebaki fuko moja tu tena NSSF,ambayo linaonekana liko strong.
   
 6. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Asante sana Shadhuly This is my point mifuko yetu ya pension iko katika hali mbaya sana. Wanasiasa wanaiendesha, wakurugenzi wengine wanaifisadi, na kuwekeza kwa ajili ya serikali kutaua mifuko ya pension ya Tanzania. Ikifa mifuko hii uchumi wa Tanzania uko mbioni kuanguka kama sio kuteketea kabisa kwa kukosa pesa ya kujiendesha.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Inasikitisha sana.
  Nimechangia toka mwaka 2003, na hadi wa leo sijapewa namba yangu ya uanachama, na kwa masikitiko makubwa juzi nimeletewa fomu nyingine nijaze details zangu upya, wakati nilishajaza nikianza kazi mwaka 2003!...sijui ndo nitaanza kuwekewa akiba mwaka huu!??
  Kwa kweli, kama serikali imeamua hadi kuchukua hela za raia, yaani za mtu mmojammoja na kuzitumia kwa mambo ya chama hii inatisha!
   
 8. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Pole mkuu,

  Ndio Tanzania yetu hiyo ukija kuidai hela yako usisashangae sintofahamu nyingi!!!!
   
 9. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Serikali inadai 3.1trillion. Je ni deni la pesa ambazo serikali imechukua au ni michango ya civil servants ambazo serikali haikupeleka. Ufafanuzi tafadhali
   
 10. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  The financial situation in the current government is extremely grave.
   
 11. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Michango mkuu ya watumishi wa serikali ndiyo hiyo inatumika kifisadi namna hiyo. Wawabane basi wawekezaji hawataki kazi kucheka na kima tu matokeo yake ndiyo hayo.
   
 12. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ni kweli mkuu na hapo bado nahisi huo ni mwanzo wa uchungu tu, itafikia kipindi mambo yatagoma kwenda kabisa.
   
 13. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,576
  Likes Received: 1,670
  Trophy Points: 280

  Duhhhhhhh!!!!!
  sasa deni jumla la serekali ni shilingi ngapi?
  maana hiyo peke yake ni zaidi ya ROBO ya bajeti ya nchi hii!
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mashirika mengine ya hifadhi ya jamii yanaidai serikali kiasi chochote? Na ni kiasi gani kwa kila shirika?
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Mar 27, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mafuko kweli yamezidi.
  Lingebaki moja hata gharama za uendeshaji zingepungua kiasi.
   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Mar 27, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  khaaaa! Pole sana ila inawezekana wamemisplace details zako kwahiyo wanazihitaji tena.
  Anza mchakato wa kufatilia mapema.
   
 17. L

  Logician Senior Member

  #17
  Apr 1, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  It is very sad news ...... if political interferences continues as it is now the financial sustainability of public pension funds will be questionable with no future.

  Director Generals of these funds do not observe single borrower limits and risk concentration principles. Public pension funds' portfolios are not well diversified with too much government involvements. Of course, they always argue that doing business with government is safer because it is the guarantor but too much dependence on one customer does raise a question on their ability to survive shall this customer starts to dishonor s/he obligations timely. The obvious risk is the liquidity risk which may in further trigger other financial problems.

  It is time to play safe as any collapse of the fund in this sector has enormous impact in the financial system of the country.

  A caution:

  Government and political interferences will worsen financial sustainability of the PPFs which will, in turn, create necessary conditions for private pensions to come as an exit door and government's excuse.

  SSRA should take a bitter pills asap to arrest poor governance practices in this sector. Measures may include

  • harmonization of the pension formulas,
  • clear definition of what is a government to assist single borrower limit is observed once introduced
  • advise government to reduce unnecessary competition from public pension funds and allow private pension funds to come while these public pension funds are in sound financial situations.
  • etc as they see fit.....
   
 18. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #18
  Apr 4, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  PPF ndiyo Parastatal Pension Fund na PSPF Public Servants Pension Fund naomba ufafanuzi kuwa hizo trilion ni za PPF au PSPF? Lakini pia kamati ya zitto inashughulikia mashirika ya umma, tafadhali fafanua.
   
 19. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #19
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  PSPF siyo mfuko wa pensheni kwa mashirika ya umma labda kama ulimaanisha PPF
   
 20. s

  shadhuly Senior Member

  #20
  Apr 4, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  pole sana,ukweli ni kwamba kuhusu namba inawezekana hiyo fomu uliojaza wameimisplace.lakini nakupa matumaini kwamba pesa huwa hazipotei.michango yote ambayo inalipiwa bila namba huwa inawekwa katika acount maaum inayoitwa SUSPENSE ACCOUNT.then namba ikipatikana michango inakuwa posted ktk account/number ya mwanachama.nakushauri ujaze hiyo fomu ili upate namba ya uanachama.sababu itakuja kusumbua baadae.then washauri muwe mnateembelea ktk hizo ofisi ili mpate kujua balance ya michango yako mfano nssf wanatoa hiyo huduma bure pia itakusaidia kujua kama muajiri wako ana peleka hiyo michango sababu kuna problem baadhi ya waajiri wanawakata wafanyakazi wao lakini hawasubmit hiyo michango.
   
Loading...