Mbunge Simon Lusengikile: Gari ya Milioni 120 Yauzwa Milioni 8

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

Mbunge Simon Lusengikile: Gari ya Milioni 120 Yauzwa Milioni 8

MBUNGE wa Jimbo la Busega, Simon Lusengikile ameitaka Wizara ya Fedha kuja na mpango utakaoonesha ni namna gani uthaminishaji wa magari ya Serikali unafuata bei ya soko kabla ya kuuza magari hayo.

Akichangia hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Lusengikile amesema kuwa lipo tatizo kubwa katika mchakato wa kuthaminisha magari ya Serikali kabla ya kuyauza.

Ametoa mfano wa gari la Serikali aina ya V8 lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 120 lililokuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya ambalo liliuzwa shilingi milioni nane baada ya kufanya kazi miaka kumi tu na bado likiwa katika hali nzuri.

Aidha, ameongeza kuwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa imeona kuna changamoto ya kutokuwa na uwazi wakati wa kuuza magari ya umma.

Amesema taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) inaonesha kuwa katika taasisi nane zilizokaguliwa, sita kati ya hizo hazikuwa na uwazi katika kuuziana magari.
 
Attachments

  • Untitlednjuy.jpg
    Untitlednjuy.jpg
    8.9 KB · Views: 1

View: https://m.youtube.com/watch?v=Kt2cRzvcbEk&embeds_referring_euri=https%3A%2F%2Fwww.jamiiforums.com%2F&source_ve_path=MjM4NTE&feature=emb_title

Hivi wangapi mmesikiliza ili wasilisho la kamati.

Huo ufisadi unaoongelea wa millioni kulinganisha na watu wanavyo tafuna huko kwengine ni sawa na kikombe kumwaga kikombe cha maji baharini.

Personal baada ya kusikiliza hiyo report na reaction ndogo ya watanzania ndio nimekubali siasa za Tanzania kwa mtu unaejielewa ni sawa na utaratibu wa mbugani. Camera man wanaona simba dume wale wanaenda uwa watoto wasio wao mama mtu anajaribu kila mbinu kuokoa maisha ‘binadamu’ unaambiwa acha usiingilie huo ndio utaratibu wa nature wazungu wanabaki wanaangalia tu vitoto vinavyouliwa.

Ndio siasa za Tanzania kama kweli Unafahamu kanuni za maendeleo hiyo nchi aiwezi toka kwenye umaskini mpaka mwisho wa dunia kwa siasa za leo na hakuna hao wanasiasa waliopikwa kulisogeza mbele ukiwasikiliza vijana wenye nyadhifa ambao ndio wakuu wa nchi kesho.

Change will never happen in Tanzania itabaki maskini for a long time; huo ndio ukweli wenyewe.
 
Tuibienii Tena mtuibie haswa maana wananchi tumejiweka kizezeta tuibienii nkasema waachwe waibeee...
Shangaa nchi leo anasifika makonda kwa maigizo yake ya kugawa hela nakukumbatia wabibi eti anajidai kuikosoa serikali,ajabu anakosoa serikali na anataka tuichagie hiyohiyo serkali na haohao mawaziri na rais anayekosea kuchagua wasaidizi.
Shangaa wakati wananchi wanalia kwa huyo kijana kiongozi wanchi anaalikwa mahafla huko ulaya... nabado wenyenjaa huku gizani wanamsifu na kumshangilia kwakugalagala
Nkasema Tena ibeniiiii
 
Mbunge Simon Lusengikile: Gari ya Milioni 120 Yauzwa Milioni 8

MBUNGE wa Jimbo la Busega, Simon Lusengikile ameitaka Wizara ya Fedha kuja na mpango utakaoonesha ni namna gani uthaminishaji wa magari ya Serikali unafuata bei ya soko kabla ya kuuza magari hayo.

Akichangia hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Lusengikile amesema kuwa lipo tatizo kubwa katika mchakato wa kuthaminisha magari ya Serikali kabla ya kuyauza.

Ametoa mfano wa gari la Serikali aina ya V8 lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 120 lililokuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya ambalo liliuzwa shilingi milioni nane baada ya kufanya kazi miaka kumi tu na bado likiwa katika hali nzuri.

Aidha, ameongeza kuwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa imeona kuna changamoto ya kutokuwa na uwazi wakati wa kuuza magari ya umma.

Amesema taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) inaonesha kuwa katika taasisi nane zilizokaguliwa, sita kati ya hizo hazikuwa na uwazi katika kuuziana magari.
Huyo Mbunge ni mgonjwa!
Gari Ina zaidi ya miaka 10 anataka iuzwe ghali?
 
Wewe ndio mgonjwa. Gari za wakubwa tanzania ni latest model inaponunuliwa, pia servicing yake huwa ni ontime na ya ubora wa juu. Na umeshaambiwa iko katika hali nzuri. Hiyo gari ikipelekwa mtaani, itauzwa Mil hata 40.
 
Mbunge Simon Lusengikile: Gari ya Milioni 120 Yauzwa Milioni 8

MBUNGE wa Jimbo la Busega, Simon Lusengikile ameitaka Wizara ya Fedha kuja na mpango utakaoonesha ni namna gani uthaminishaji wa magari ya Serikali unafuata bei ya soko kabla ya kuuza magari hayo.

Akichangia hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Lusengikile amesema kuwa lipo tatizo kubwa katika mchakato wa kuthaminisha magari ya Serikali kabla ya kuyauza.

Ametoa mfano wa gari la Serikali aina ya V8 lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 120 lililokuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya ambalo liliuzwa shilingi milioni nane baada ya kufanya kazi miaka kumi tu na bado likiwa katika hali nzuri.

Aidha, ameongeza kuwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa imeona kuna changamoto ya kutokuwa na uwazi wakati wa kuuza magari ya umma.

Amesema taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) inaonesha kuwa katika taasisi nane zilizokaguliwa, sita kati ya hizo hazikuwa na uwazi katika kuuziana magari.
Bibi anaomba tumchague tena 2025🤭
 
Gari zote za serikali ziuzwe kwa mnada wa wazi mtandaoni. Kwa US kuna site inaitwa Gov deals. Humo wanapiga mnada kila aina ya bidhaa za serikali na walizotaifisha, hadi ndege zipo. Mtu yeyote mwenye account anaweza kubid bei. Unahitajika mfumo kama huo.
 
Mbunge Simon Lusengikile: Gari ya Milioni 120 Yauzwa Milioni 8

MBUNGE wa Jimbo la Busega, Simon Lusengikile ameitaka Wizara ya Fedha kuja na mpango utakaoonesha ni namna gani uthaminishaji wa magari ya Serikali unafuata bei ya soko kabla ya kuuza magari hayo.

Akichangia hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Lusengikile amesema kuwa lipo tatizo kubwa katika mchakato wa kuthaminisha magari ya Serikali kabla ya kuyauza.

Ametoa mfano wa gari la Serikali aina ya V8 lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 120 lililokuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya ambalo liliuzwa shilingi milioni nane baada ya kufanya kazi miaka kumi tu na bado likiwa katika hali nzuri.

Aidha, ameongeza kuwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa imeona kuna changamoto ya kutokuwa na uwazi wakati wa kuuza magari ya umma.

Amesema taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) inaonesha kuwa katika taasisi nane zilizokaguliwa, sita kati ya hizo hazikuwa na uwazi katika kuuziana magari.
Huyu anafikiri gari ni ardhi ambayo kila siku inaongezeka thamani? Gari nakumbuka kuna kitu kinaitwa depreciation value kila inavyotumika ndivyo thamani yake inapungua. Nafikiri sijakosea Sana. Miaka kumi ni muda mrefu mno. Kuna mtu aliwahi kunisimulia kule kwa wenzetu scania hutumika kwa miaka kumi tu baada ya hapo inatakiwa irudi kiwandani ikafanyiwe refublish ndio iruhusiwe kutumia tena au iuzwe nje ya nchi.
 
Huyo mbunge ana akili za vibwengo, 10years ankataa 8 million, hilo limeuzwa scrapper
 
Back
Top Bottom