Prophet IPM anahubiri injili gani?

Ni kama muislam fulani aliyejibanza ndani ya ukristo! Si kwa shombo zile anazozitoa dhidi ya wakristo huku akiwasifu waislamu! Mahubiri yake yamejaa utata na mashaka mengi kwa wanaoijua injili
 
Dini ya kikristo ni ya amani sana! Ingekuwa ni dini ya kiislam huyu asingethubutu kuwasemasema waislam na imani yao kuwa wanaamini abrakadabra tu, waislam wangemuijia juu na kumtembezea bakora kama si majambia. Sijawahi kuona muislam akiwanangananga waislam wenzake kwa kile wanachokiabudu na kukiamini ndani ya uislam huku waislam wakimuangalia tu! Huyu mmbaba amezidi kuwasema wakristo sana, anawaona ni mbulula kila nyanja
 
Asee ili ukilipigia malengo kwa mwaka ukawa na mikutano yako 10 au 5 kwa kiingilio cha 50k na ukawa na uhakika wa kuwadaka wanyantuzu 500 assee unaweza ipangia bajeti halmashauri yako
Na hii ndio hasa idea ya huyo nabii, alifikiria hivi hivi. Akifanikiwa hapo atakuja na huku mikoani. Kmmk waliohudhuria
 
hiyo haijalishi we ni kobazi au muebrania, jamii nzima imekumbwa na hofu hiyo na wanavaa wote, sio waebrania hata kobazi wanavaa
Jamii imekuwa ikishabikia mambo ya kijinga
 
Tupunguze ushauri.

Mawazo yake yaheshimiwe
 
Huyu ana tofauto gani na kiboko ya wachawi? Wapumbavu kama hawa ndio wanasababisha ukristo utadharauliwe.
 
Watu wanataka mijadala wajadili masuala ya uchumi,siasa,teknolojia
Huyu anatuletea mambo ya wanaume na wanawake kudinyana,umbeambea udaku

Ova
cha ajabu wanaume wamejazana kumsikiliza, niliwashanga wanaume wale kama wana akili timamu na hawana kazi za kufanya. Muda wa kwenda kumsikiliza huyu mmbaba wanaupata wapi?
 
cha ajabu wanaume wamejazana kumsikiliza, niliwashanga wanaume wale kama wana akili timamu na hawana kazi za kufanya. Muda wa kwenda kumsikiliza huyu mmbaba wanaupata wapi?
Yaani mwanaume unashona sare ati unaenda kwenye kikao cha wanaume na mnaenda kuambiwa mambo ya kawaida mno
Mara usilale ukutani, ati mkeo akuombe ruhusu
 
Nimecheka kwa nguvu hadi watu wamenishangaa,eti usikubali kulala ukutani"
Ila ndugu usipaniki sana chukulia tu kwamba ile ni miradi ya watu maana kuna mazuzu ni kweli watahudhuria na kulipishwa michango
 
Hayo mambo ya utapeli wa dini yako kote kote:

Kuna Nabii wa Kiislamu Elyasi anaishi Kibaha:

Kuna Shehe wa Zanzibar aliyesema Mlevi wa Zanzibar ni Mbora mbele ya Allah kuliko Mashehe wote wa Bara:

Kuna Shehe anayesema kuwa Uislamu unategemea Majini ili ustawi:
Hata Mtume MUHAMADI alifunga Majini: by Shehe Dr. Sule:

Mashehe walio Mwombea Mfalme kwa Majini ili ashinde Uchaguzi:

Shehe Mkatavichwa wapinzani wa Chama nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…