- Hawajajipanga kiuongozi; huwezi kuwa na viongozi wote wa kitaifa wanagombea ubunge halafu mkatarajia kushinda Urais!
- Hawajajipanga katika kutengeneza taasisi inayotegemea mfumo badala ya watu. Matokeo yake tatizo lile la watu kuhusu watu lililoko CCM (kwa kidogo) linaikuta CDM kwa kiasi kikubwa
- Hawajajipanga katika kuelezea mabadiliko ya mfumo ambao wao waataka kuujenga; je wanataka kuja kutawala nchi chini ya mfumo huu huu na vyombo hivi hivi vilivyoshindwa? au watafikiria kuvibadilisha wakishashika madaraka?
- Hawajajipanga katika kubadilisha sheria ambazo zinatusumbua leo hii; ukiondoa wakati ule Zitto ameleta mswada wa mabadiliko ya sheria ya maadili hatujasikia shinikizo lolote la kuleta mswada mbadala; haikuwa kwenye sheria ya katiba, sheria ya takukuru wala sheria nyingine;
- Hawajajipanga katika kutengeneza chama ambacho kinatoka chini kwenda juu badala ya kutoka juu kwenda chini. Matokeo yake madudu ya Arusha, Mwanza yametokea na tunaendelea kuona jinsi ambavyo bila viongozi wa juu kushuka chini ni vigumu sana kwa CDM chini kuweza kufanya kazi yake vizuri. CDM inategemea mno nguvu ya viongozi wa kitaifa zaidi ..
- Hawajajipanga katika kutengeneza mfumo mzuri wa kuhamasisha watu kujiletea maendeleo. Wao wamekuwa kama CCM wanatoa zaidi na kufurahia misaada ya kujenga visima! Hatujawaona wakihamasisha wananchi kwenda kuchimba visima wao wenyewe. Leo tunawaona wakihangaika kutoa misaada kwa wananchi wakati wanadai wana 'nguvu ya umma'. Nguvu ya umma si maandamano! ni mjumuisho wa uwezo wao, nguvu kazi, elimu, raslimali na muda. Ni kwa kiasi gani hivi vimeletwa kujiletea maendeleo?
- Hawajajipanga katika kutoa changamoto dhidi ya vyombo vya usalama. Tangu mauaji ya Arusha hadi haya ya juzi watu wale wale wanashikilia nafasi zao . Mwema, Chagonja, n.k
- Hawajajipanga katika kukosoa kisomi sera zilizoshindwa za CCM licha ya kuwa CDM inakusanya wasomi wengi na inakubalika sana na wasomi. Leo hii mwaka wa tatu hakuna hotuba hata moja nzito yenye kufanya contrast ya sera za CCM na zile za CDM na kuonesha kwanini za CDM ni bora!
... inaendelea...
Ni kwamba una ID mbili au umeamua mjibia huku ukiacha wengine hewani kwa tuliyoongea mwanzoni?Naomba ukajibu mkuu ili tuyafunge.
Anyway ngoja nipitie nadharia ambazo kwa kiasi kikubwa ni mawazo yako tuu:
-Kwanini unadhani ukiwa kiongozi wa kitaifa ktk chama cha upinzania huwezi kugombea ubunge?
-Wewe ni mshabiki na mshauri wa Zitto km unavyoonekana ktk postings zako.Pengine ndipo kulikokufanya umshauri apandishe kicha ukidhani kuwa ni tegemeo.Basi subiri akianguka ndipo utakuw aproved wrong.Hujamuuliza Sitta kwa nini alikula kona?kwa vile aliona kanuni za chama hazimruhusu kudandia na kuingia ktik list ya kugombea.Nadhani hata wewe somewhere ktk pitapita utakuwa umeonja hiyo shubiri ya CDM.
-Huo mfumo unaoutaka wautangaze kwani una deadline?What is huu mfumo ni safi tuu ila CCM ndio wame abuse kwa uchafu na udhaifu wao?
-Hawajajipanga kubadili sheria?Hujamiskia Tundu Lissu na Mnyika?Umemwona Zitto tuu.Kwani Ziito yupo wapi?Au mmeshaambiana kuwa si mwana CDM?
-hawajipanga kutengeza chama kutoea chini ila kutokea juu?umesoma ulichoandika mwanzoni?Kuwa haupo tayari kuwasaidi kushinda ubunge bila kushika uraisi.Hiyo kauli haijakutoka bure,ni influence ya CDM walipotangaza mika kadhaa nyuma kuwa wanajenga chama kuanzia chini,wakipanda hadi kufika pa kugombea urais.
-Kuhamasisha watu ,unajua mbowe kawambia nini jimboni kwake?Kuna miradi mingi tuu kawaambia wakichnga kiasi wanachoweza yeye atatoa mara mbili yake?Lema kila mara ana harambee.Sijui kama umepima kw amakini ulichoandika hapa.Kule kaskazini watu wanajiletea maendeleo wenyewe,watu wanajenga makanisa,shulem, dispensary, kurekebisha barabara kwa kujituma na kuongozana.Pengine ndio maana hujasikia sana ktk TV.Hiyo mikoa yenu ndio inahiaji pewa kitu kamili bure.CDM wanafanya hiyo kazi sana hadi nashangaa mwanakijiji gani hujaona haya.
-tehe tehe.changamoto za vyombo vya usalama?pamoja na kwamba tanzania hakuna mtu anayeweza jiengua mwenye hata kwa nini na akienguliwa huanza uadui wa kufa mtu.bado CDM wamesema, na wamesema,wamewapa ultimatum,wamewabana mbele ya mataifa.Na serikali imeshuhudia ikipewa Live.Usalama wa Taifa wamepewa live majukwaani na ktk kura.Sasa sijui ulitaka nini?wafanya vurugu za kipuuzi kama za CUF ili muwahukumu kwa hilo?
-jamani wasomi,wanawakilisha fikra makini, na si lazima waende kwa kutumia conventional ways,conventional ways za nini?ili CCM wazijue na kuziaharibu?CDM wamekuwa wakiendelea kwa kuwa unpredictable wa adui CCM(CCm ni adui kwa vile anapambana kuia CDM na raia).Sasa majukwaani kote CDM waliposimama wameyasema yote,sasa sumary ya nini?Majukwaa wanahiataji kuongea localized problems.Hata makampuni makubwa kama Google huwa na localized contents.Nadhani hii ni idea mpay kwako na wengine waliomshangaa Mbowe alipoongela mapato ya mlima Kilimanjaro akiwa Rombo.Sasa ya nini kuelezea kwa kina makosa 4000 ya CCM ktk hotuba moja?Huo muda utakuwa wapi?Kusema tuu kuwa CDM 1 ni sawa na gamba 30,huku wakiweka mifano hai ya magamba hakutoshi tuu?
Duh..nakushauri kurudia ulichoandika kwanza kabla ya kuendelea.Nimekujibu haraka haraka tuu ili uweze tumia umahiri wako kufikiri zaidi.Hivi kulikuwa na haja ya kuuliza haya maswali bado ukasema unaijua CDM?Sijui Jmushi1 yupo wapi achangie hapa.