Mwanakijiji ana mawazo yake mwenyewe ambayo kwa wengine 'wasio waangalifu' yana madhara makubwa. Wanaochagua kufuata fikra zake wanatakiwa kufuata kwa mbali na kwa tahadhari. Yeye anaunga mkono CCJ, anaunga mono CHADEMA na anaunga mkono na CCM. Kwake ni heri CCM iliyo kwenye mgawanyiko iendlee kushika dola kuliko jukumu hio kulipeleka kwa CHADEMA iliyogawanyika na isiyo na matarajio ya kujipanga kabla ya uchaguzi wa 2015. Nimuulize kipo chama kilichoko madarakani kinachotoa fursa kwa chama kinachotaka kuingia madarakani kufanya maandalizi yote anayopendekeza yafanywe na CHADEMA? Niliwahi kusema wakati fulani kuwa CHADEMA inao umma nyuma yake umma ambao umekerwa na yale yanayofanywa na CCM na ambayo wanaona hayawezi kubadilika. Hakuna chama (hata kiwe na mikakati mizuri kiasi gani) ambacho kitakataliwa na wananchi, kinachoweza kushinda kirahisi katika chaguzi. Kama nia yako ni kuitia shime CHADEMA isibweteke kwa mafanikio iliyoyapata njia unayoitumia inainufaisha zaidi CCM. CCM imeshindwa. Haina tena uhalali wa kuendlea kuitawala nchi hii. Itafanya hivyo kwa ujinga tu wa wananchi wake. Watu wenye nia safi ya kuleta mabadiliko wataendelea kuja CHADEMA au chama chochote chenye dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko. Sera bora zitaendelea kupatikana, na CCM itaondolewa madarakani. Yaliyofanywa na CCM (na yanayoendelea kufanywa yanakera kuliko upungufu wowote ulioonyeshwa na Chadema hadi sasa. Najua CCM itafanya kila lililo kwenye uwezo wake kung'ang'ania isitoke hata kama hakuna jema analowafanyia Watanzania (au niseme hata kama imeshindwa kuondoa kero zinazowaumiza watu zilizo kwenye uwezo wake) Siamini (mpaka hapo atakaponishawishi) kwamba kwa sasa Mwanakijiji anaona Tanzania isiyo na CCM ni jambo linalowezekana. Huenda angetamani kumuona Nyerere anafufuka na kuifufua CCM kuliko kumuona anafufuka na kuiimarisha chadema - maana kazi ya kuifufua CCM ni rahisi kuliko Chadema. Yeye kama mmoja wa watunga sera wa Chadema alitakiwa aje atuambie alipendekeza nini kuhusu maeneo anayoyatilia shaka kama polisi, usalama wa taifa n.k. Kama alishiriki kwa kiwango kikubwa kama hicho kuijenga Chadema anatokeaje kwa walio nje 'ya chama' na madai ya kukatisha tamaa kama haya. Niliwahi kumuuliza Zito kuwa ikiwa ndani ya Chadema kuna mambo hayaendi sawa kwa nini wasiyaseme kwa maslahi ya chama badala ya kuja na kauli zinazoashiria kuwa wameanza kumwagiana mboga na ugali. Mi naamini chadema ni ya umma uliochoka na ukandamizwaji, na ikiwa wenye matarajio hayo wamejidanganya kufikiri hivyo, watatafuta chombo kingine kitakachokidhi kiu yao, na chadema kitapoteza umaarufu wake. Maelezo yako kwa sehemu kubwa yameonyesha kukihurumia (kukibeba) CCM zaidi kuliko Chadema huku ukijua madhambi ya CCM hayawezi kabisa kulinganishwa na udhaifu wowote wa chadema. Nilishawahi kuona watu niliowaamini sana kwa kupanga hoja, nikatekwa nao na kuleweshwa nao. Lakini ulifika wakati walichukua msimamo tofauti kabisa. Nikaamini kuwa hakika hakuna asiyenunulika. Waandishi wa RAI kabla mkapa hajaingia madarakani walimpamba lakini aliposhika madaraka walimponda. Naomba usije ukawa miongoni mwa hao. Hata hivyo nitakuwa mwangalifu zaidi katika kufuatilia mawazo yako kuliko huko nyuma. Kwa mara ya kwanza hoja yako imeniacha na kiu.