Proper recording: Nini kilimbadili Mzee Mwanakijiji?

Proper recording: Nini kilimbadili Mzee Mwanakijiji?

  • Hawajajipanga kiuongozi; huwezi kuwa na viongozi wote wa kitaifa wanagombea ubunge halafu mkatarajia kushinda Urais!
  • Hawajajipanga katika kutengeneza taasisi inayotegemea mfumo badala ya watu. Matokeo yake tatizo lile la watu kuhusu watu lililoko CCM (kwa kidogo) linaikuta CDM kwa kiasi kikubwa
  • Hawajajipanga katika kuelezea mabadiliko ya mfumo ambao wao waataka kuujenga; je wanataka kuja kutawala nchi chini ya mfumo huu huu na vyombo hivi hivi vilivyoshindwa? au watafikiria kuvibadilisha wakishashika madaraka?
  • Hawajajipanga katika kubadilisha sheria ambazo zinatusumbua leo hii; ukiondoa wakati ule Zitto ameleta mswada wa mabadiliko ya sheria ya maadili hatujasikia shinikizo lolote la kuleta mswada mbadala; haikuwa kwenye sheria ya katiba, sheria ya takukuru wala sheria nyingine;
  • Hawajajipanga katika kutengeneza chama ambacho kinatoka chini kwenda juu badala ya kutoka juu kwenda chini. Matokeo yake madudu ya Arusha, Mwanza yametokea na tunaendelea kuona jinsi ambavyo bila viongozi wa juu kushuka chini ni vigumu sana kwa CDM chini kuweza kufanya kazi yake vizuri. CDM inategemea mno nguvu ya viongozi wa kitaifa zaidi ..
  • Hawajajipanga katika kutengeneza mfumo mzuri wa kuhamasisha watu kujiletea maendeleo. Wao wamekuwa kama CCM wanatoa zaidi na kufurahia misaada ya kujenga visima! Hatujawaona wakihamasisha wananchi kwenda kuchimba visima wao wenyewe. Leo tunawaona wakihangaika kutoa misaada kwa wananchi wakati wanadai wana 'nguvu ya umma'. Nguvu ya umma si maandamano! ni mjumuisho wa uwezo wao, nguvu kazi, elimu, raslimali na muda. Ni kwa kiasi gani hivi vimeletwa kujiletea maendeleo?
  • Hawajajipanga katika kutoa changamoto dhidi ya vyombo vya usalama. Tangu mauaji ya Arusha hadi haya ya juzi watu wale wale wanashikilia nafasi zao . Mwema, Chagonja, n.k
  • Hawajajipanga katika kukosoa kisomi sera zilizoshindwa za CCM licha ya kuwa CDM inakusanya wasomi wengi na inakubalika sana na wasomi. Leo hii mwaka wa tatu hakuna hotuba hata moja nzito yenye kufanya contrast ya sera za CCM na zile za CDM na kuonesha kwanini za CDM ni bora!
... inaendelea...


Naam sasa umenena!! mimi sio discussant lakini mara nyingi natumia mbinu tu nilizoiga toka kwa wanazuoni kuchokoza fikra na mawazo yaliyofichika! ukweli ni kwamba aliyetoa hii thread amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kumtoa MM undani na kumleta nje kweupeee!

Naamini sasa umeweka bayana mapungufu ambayo mimi naona ni changamoto ambazo cdm wanapaswa kuziwekea mikakati thabiti ili kuvuka katika duru hili. Siamini ndani ya kapu la cdm hawajayaona haya.. wameyaona na pengine wengine yanawatesa namna ya kuyakabili LAKINI pia tukubali ni pagumu sana unapofikia level hii kichama.. Tukumbuke chama ni muunganiko wa watu wenye nia na kusudio na dhamira yakutaka kuchukua madaraka ya dola.. WATU hawa wanahulka na tofauti zao ambazo KIUKWELI inahitajika mfumo thabiti kuweza kuweka mambo sawa ili kuleta consistency,stability na reliability miongoni mwa wanachama na wafuasi pia.

Nakubaliana na wewe kwamba kuna changamoto lakini napingana na wewe unapoweka neno HAWAJAJIPANGA.. ndugu, unajua lugha inaweza leta maana pana ya mambo.. neno KUTOKUJIPANGA sio kwa watu makini, umeshasema cdm ina wasomi na watu mahiri ambao bado unaamini wana nafasi ya kuweka mambo sawa.. sasa unaaminije HAWAJAJIPANGA?? kwanini usiamini kwamba wapo kwenye mapambano ya aina mbalimbali.. Kumbuka cdm wapo kwenye kona ngumu sana kiutendaji maana ni chama kichanga bado hakiwezi jifananisha na chama tawala ambacho kina experience na ukongwe tangu enzi na enzi! ni lazima hapo pana added advantage (haipingiki) na kukiondoa hakutaonekana kwa macho... tuchukulie mfano majirani zetu kenya na KANU yao.. ilikuwa ngumu sana kuwaondoa mpaka wakaresolve kudesolve chama na kuunda chama ndani ya chama!!! haukujifunza pale?? ipo mifano mingi sana, hata south africa hilo lipo, nenda uganda yanaendelea hayo hayo, zimbabwe nk... Kukiondoa chama kikongwe kama chetu ni ngumu... CDM wanastahili pongezi maana ni chama pekee cha upinzani ktk ukanda wetu ambacho kimeweza kufurukuta nje ya chama tawala chenyewe!!!

JAPO nakubali changamoto zipo na kwa mawazo kama yako watayaangalia kwa jicho pana na matumaini yapo tele kwamba watayarekebisha kwa kuwasaidia mawazo na kuwapa nafasi yakutekeleza mawazo hayo kwa nia njema... swala la kimfumo ndugu yangu bado ni tata maana sometime inafikia mahala unashindwa kuelewa tupo katika mfumo gani na ni mfumo gani kiuhalali unahitajika ili nchi hii iweze kurealize potential zake!! kama chama kikongwe kimeshindwa tusiamini haraka haraka kwamba kuna mambumbu hawakujua kuset up mambo vizuri lakini tujaribu kufikiri nje ya box pia kwamba ni aina gani ya mifumo midogo midogo tuliyo nayo inayounda mfumo mzima!! aina ya watu pia na tulipoanzia mpaka tulipo kuna yapi tulikosea... yapo mengi yakutazama ambayo nadiriki kusema ianzishwe thread madhubuti itakayo jadili kwa kina na wachangiaji mahiri wachangie ni mfumo gani unatufaa watz na upimwe kwa undani wake... sio kutamka tu!

Hayo mengine yana solutions maana ni changamoto na hayahitaji kukurupuka na kuanza kupanic nayo,, sometime ukimya pia ni kuonyesha ukomavu na umakini!! ukianza kupurukushana na vyombo vya usalama bila kuzingatia utaratibu na sheria zetu zilivyokaa utajikuta ya mbagala na iringa yanajirudia kila kukicha!! Au ukaanza kukojolea (samahani) manifesto ya chama kingine eti sera zimeshindwa utaoneka chizi wewe... kukimbizana na kichaa kunataka moyo na timing makini...!!

nimalizie tu kwa kusema mimi bado ni mchanga humu na bado naendelea kujifunza mengi, nikaribishwe kwa uamini wa nguvu ya hoja na sio hoja ya nguvu! kwako MM



 
  • Hawajajipanga kiuongozi; huwezi kuwa na viongozi wote wa kitaifa wanagombea ubunge halafu mkatarajia kushinda Urais!
  • Hawajajipanga katika kutengeneza taasisi inayotegemea mfumo badala ya watu. Matokeo yake tatizo lile la watu kuhusu watu lililoko CCM (kwa kidogo) linaikuta CDM kwa kiasi kikubwa
  • Hawajajipanga katika kuelezea mabadiliko ya mfumo ambao wao waataka kuujenga; je wanataka kuja kutawala nchi chini ya mfumo huu huu na vyombo hivi hivi vilivyoshindwa? au watafikiria kuvibadilisha wakishashika madaraka?
  • Hawajajipanga katika kubadilisha sheria ambazo zinatusumbua leo hii; ukiondoa wakati ule Zitto ameleta mswada wa mabadiliko ya sheria ya maadili hatujasikia shinikizo lolote la kuleta mswada mbadala; haikuwa kwenye sheria ya katiba, sheria ya takukuru wala sheria nyingine;
  • Hawajajipanga katika kutengeneza chama ambacho kinatoka chini kwenda juu badala ya kutoka juu kwenda chini. Matokeo yake madudu ya Arusha, Mwanza yametokea na tunaendelea kuona jinsi ambavyo bila viongozi wa juu kushuka chini ni vigumu sana kwa CDM chini kuweza kufanya kazi yake vizuri. CDM inategemea mno nguvu ya viongozi wa kitaifa zaidi ..
  • Hawajajipanga katika kutengeneza mfumo mzuri wa kuhamasisha watu kujiletea maendeleo. Wao wamekuwa kama CCM wanatoa zaidi na kufurahia misaada ya kujenga visima! Hatujawaona wakihamasisha wananchi kwenda kuchimba visima wao wenyewe. Leo tunawaona wakihangaika kutoa misaada kwa wananchi wakati wanadai wana 'nguvu ya umma'. Nguvu ya umma si maandamano! ni mjumuisho wa uwezo wao, nguvu kazi, elimu, raslimali na muda. Ni kwa kiasi gani hivi vimeletwa kujiletea maendeleo?
  • Hawajajipanga katika kutoa changamoto dhidi ya vyombo vya usalama. Tangu mauaji ya Arusha hadi haya ya juzi watu wale wale wanashikilia nafasi zao . Mwema, Chagonja, n.k
  • Hawajajipanga katika kukosoa kisomi sera zilizoshindwa za CCM licha ya kuwa CDM inakusanya wasomi wengi na inakubalika sana na wasomi. Leo hii mwaka wa tatu hakuna hotuba hata moja nzito yenye kufanya contrast ya sera za CCM na zile za CDM na kuonesha kwanini za CDM ni bora!
... inaendelea...

Hapo kwenye RED nadhani hayo (ya kuweka hadharani mikakati na jinsi ya kutawala) wanatakiwa kuyafanya baada ya kukabidhiwa madaraka although wanaweza kuyatumia kama general promise kwa wananchi kuwa watafanya mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutawala. Otherwise wakianza kuanika kila kitu ni kuwasaidia CCM ambao kwa kweli watayafanyia kazi na hivyo kuwajengea uhalali wa kuendelea kutawala zaidi. Kuanika kila kitu ni sawa na CDM kujihalalisha kuendelea kuwa chama cha upinzani cha kudumu.Yaani CDM itakuwa kama Think Tank ya CCM.

Huwa kuna technique kwenye siasa za ushindani ya kuchukua au kupoka uhodhi wa mikakati. Tumeliona hili likitumiwa kwenye vita dhidi ya ufisadi ambayo wengi tunajua iliasisiwa na upinzani (CDM ikiwemo) dhidi ya CCM.Kilichofuata ndani ya CCM ni kuundwa kundi la wapambanaji wa Ufisadi wakawa wanafanya kazi hiyohiyo ya upinzani ingawa kisanii.Na sasa tuna V4C ya CUF ikijaribu ku pre-empty M4C ya CDM.

Hata hivyo, CDM kupitia Idara yao ya Sera, Utafiti na Mipango (nakumbuka nilishawahi kuwashauri waianzishe sina hakika kama ipo) hawana budi kuendelea kujikita katika kukosoa sera, sheria na mipango iliyopo lakini wajikite pia katika kutengeneza mbadala wake bila kumwaga hadharani ikiwa ni sehemu ya kujiandaa kushika dola.
 
Mashabiki na wafuas wa CDM humu 2we wakweli CDM HAIJAJIPANGA KUCHUKUA DOLA NI LAZIMA IFIKE MAHALI 2KUBALI USHAUR UNAOTOLEWA NA KUKOSOLEWA NDIO CHANGAMOTO
 
Mashabiki na wafuas wa CDM humu 2we wakweli CDM HAIJAJIPANGA KUCHUKUA DOLA NI LAZIMA IFIKE MAHALI 2KUBALI USHAUR UNAOTOLEWA NA KUKOSOLEWA NDIO CHANGAMOTO
Mkuu Magesi, angalia usije nyooshewa kidole kuwa "Magesi ni pandikizi la CCM".

Kwenye Issues za weaknesses, acceptance is the first step towards correction!.
p.
 
Ninaamini kama ingekuwa inaweza kujipanga inaweza kweli kuchukua madaraka ya nchi; lakini katika hilo siishi katika kuona potentiality tu nataka iwe katika nafasi ya kuweza kushika madaraka ya nchi. Ukifika mahali na kuona gari linatengenezwa na ukaona linavyoweza kuwa husifii tu na kuanza kuendesha. Unahitaji kuona likiwa limekamilika na kama una uwezo kusaidia kuona linakamilika.

Hii naona hujanijibu kabisa.Naona ni kama siku nyingine pasco anapoamua kufanya mizaha tuu.
 
Hapo kwenye RED nadhani hayo (ya kuweka hadharani mikakati na jinsi ya kutawala) wanatakiwa kuyafanya baada ya kukabidhiwa madaraka although wanaweza kuyatumia kama general promise kwa wananchi kuwa watafanya mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutawala. Otherwise wakianza kuanika kila kitu ni kuwasaidia CCM ambao kwa kweli watayafanyia kazi na hivyo kuwajengea uhalali wa kuendelea kutawala zaidi. Kuanika kila kitu ni sawa na CDM kujihalalisha kuendelea kuwa chama cha upinzani cha kudumu.Yaani CDM itakuwa kama Think Tank ya CCM.

Huwa kuna technique kwenye siasa za ushindani ya kuchukua au kupoka uhodhi wa mikakati. Tumeliona hili likitumiwa kwenye vita dhidi ya ufisadi ambayo wengi tunajua iliasisiwa na upinzani (CDM ikiwemo) dhidi ya CCM.Kilichofuata ndani ya CCM ni kuundwa kundi la wapambanaji wa Ufisadi wakawa wanafanya kazi hiyohiyo ya upinzani ingawa kisanii.Na sasa tuna V4C ya CUF ikijaribu ku pre-empty M4C ya CDM.

Hata hivyo, CDM kupitia Idara yao ya Sera, Utafiti na Mipango (nakumbuka nilishawahi kuwashauri waianzishe sina hakika kama ipo) hawana budi kuendelea kujikita katika kukosoa sera, sheria na mipango iliyopo lakini wajikite pia katika kutengeneza mbadala wake bila kumwaga hadharani ikiwa ni sehemu ya kujiandaa kushika dola.


Hapa WOWOWO nipo na wewe 100%. kwenye red hapo political scientists wanaita cooptation, na inakubalika kabisa kisiasa, na kinachofanyika ni kujaribu kuvunja nguvu ya upinzani kwa kuiga mipango mikakati na mawazo yao yenye mashiko na kwasababu wao bado wananguvu ya miundombinu na rasilimali inakua rahisi kuhalalisha mbele ya umma kwamba ni initiative zao!! sio tu mawazo hata watu (i mean potential leaders) wanakua coopted!! that how system works...

Bado naamini cdm hawajafanya vibaya kwa kutumia precautious publicity tactic maana wanajua upande wa pili kuna njaa kubwa ya ideas na mipango!! na mfano ndio huo wa V4C!!!!

kiukweli vita ndio hii... kuendeleza mapambano ya kukosoa na kuonyesha dhahiri namna sera na mifumo ya upande wa pili zilivyoshindwa na zinavyodidimiza azimio la kuondoa umasikini, ujinga na maradhi kwa mtz!! while at the same time wakiconstruct a model yanamna watakavyoweza kubadili na kuleta maendeleo. (without disclosing the contents)

 
Hapana nimeamua kujibu tu kwa sababu ni mimi niliyeweka assertion ya kutokujipanga.
Okay
Hapana; sikumaanisha kuwa mtu hawezi kugombea. Kama umesoma "KUtoka hapa mpaka kule" nilisema ni mkakati mbovu na nilieleza ubaya wake. CCM walichohitaji kufanya (na niliweka wazi hili miezi mitatu kabla ya uchaguzi mkuu) ni kuweka pressure kwenye majimbo ya viongozi wa upinzani ili kuhakikisha kuwa hawawezi kukutana na kusimamia kura za urais. Matokeo yake ni kuwa siku ya uchaguzi ile viongozi wote wa kitaifa ukiondoa Slaa walikuwa wamebanwa katika majimbo yao wakilinda "kura"! Ulikuwa ni mkakati mbaya na kwa vile kanuni hazijabadilika utakuwa ni mkakati mbaya 2015.

Hunajua kukosoa vitu vinavyo work kwa hoja rahisi ni ngumu sana kum convice mtu makini.CDM wana sera ya kuwa na watu wanaofanya kazi zote wanazohitajika bila kuhitaji mtu bila sababu.Na hii ndio maana waliamua resort ktk Helcopter.Hakuna haja na kuwa na luluki la viongozi wakati kuna kazi nyingi zinahitaji kufanayika kwa msimu.Ni kupoteza gharama bure ktk kipindi chote cha mwaka.Nadhani hujaangalia mislocation of resources unayo suggest.Hapo ndipo kwa mara nyingine unathibitisha kuwa Mbowe ni Kiboko na Zitto hatakiwi ajipime naye.Mbowe alipiga kampeni effective siku 2 za mwisho.Kwa vile alishajipanga vyema.Kipindi hicho CCM walikuwa wakipiga longolongo kama hizi,kuwa mbowe kaenda majimbo mengine wakati lake linaangamia.Then mwenye Jimbo akaja last minute CCM wakajikuta walipo.CDM wana lead CCM wanafuta symptoms na kivuli.
Naomba ufanye tafiti zaidi otherwise unazidi jibana katik akulimwengu kadogo kanakoumba mambo ya kufikirika kwa haraka sana na kujiweka busy sana ktk hizo.Napenda Science fiction movies kwani nyingi huweza kuwa reality(wanasayansi wamefanya na wanaendele fanya) kuliko hizi imaginations za CCM zisizoweza kuja na wazo jipya ambalo ni practical.

CCM yupi ataweka pressure wakati wapo hoi?Subiri uchaguzi ujao halafu uniambie nani wa CCM anajeuri hata ya kutoka nje ya jimbo kuzika kwa siku moja.
Si mshabiki wa watu mimi nashabikia anayefuata kanuni ambazo nimezianisha hapo juu. Lakini pia siyo mshauri wa Zitto so ulichosema hapo hakinihusu.

Okay, pengine ingawa kwa maelezo yako ya siku za nyuma ni wazi hujajibu kwa usahihi.Lets say imebaki kuwa ni rafiki yako tuu.Na ukiwa na msaada kwa CDM kama usemavyo ni wazi katika chat zenu somwhere utakuwa umeongea manen o yaliyomuinfluence kama si kushauri kisiasa.ndio maana kuna vitu mna sync.
Well, sijui kama unasema unaamini mfumo huu ni mzuri tatizo ni CCM. Kama unaamini hivyo basi tofauti yangu na wewe ni kubwa zaidi. Mimi ninaamini tatizo siyo chama tu bali na mfumo wenyewe. Chama kitakachoingia madarakani itabidi kifanye overhaul ya mfumo mzima!
teh tehe .Tofauti zinaweza kuwepo ila kwanini udhani hiyo tofauti inakusaidia wewe zaidi ya mimi?Sijui kama nimesema naamini.Ila nimetaka jua kama kwa kiasi flani inakuwa hivyo?Kuna mengi yaliyopo sasa kama CCM wangekuwa hata na kiasi fulani cha kuwajibika na uaminifu Nchi ingekwenda mbali zaidi.

Hiyo kufanya overhaul ni suala linahitaji real time decision baada ya CDM kuwa na mamlaka ya kukaa na makamanda wa Jeshi,TISS, Na wengine ili waweze kutoa the best information walizo nazo na analysis zao ili CDM wanapopanga hayo mambo waweze kujumuisha taaluma za wahusika na si siasa tuu.Vipi bwana naona watu wanakuhusisha na TISS ,hili halikuwa ktk somo moja?Anayway pengine ni zile elimu za kuungaunga na kuhama faculty na vyuo zinazofanywa na agents wetu ndio wanadhani unafafana huko?
Sijui kwanini unaniuliza mambo ya Zitto (soma jibu langu hapo juu). Usidhanie halafu ukaamini ni kweli na ukaanza kuzungumza kwa kudhania unazungumza ukiwa na msingi wa ukweli.

Hembu rudi katk posting zako uone jinsi gani ulivyojipambanua ktk mahusiano yako na Zitto?Unatakiwa uwe na mind inayoweza switch very rapidly ktk issue mbalimbali.
Ukinukuu jaribu kunukuu vizuri na kama hakijawa sawa nitaweka ili ieleweke. Mimi nimesema hivi: Hawajajipanga katika kutengeneza chama ambacho kinatoka chini kwenda juu badala ya kutoka juu kwenda chini.

Okay,lets say unachukua hiyo route.Ktk management Vitu vingi vinavyoanzia juu bila mpango na approach sahihi huwa vinapata upinzani sana kwa walengwa.Na mimi nimekutana nalo sana ktk training zangu.na hili ndilo linawatafuna CCM.Baada ya kuwafanya mabalaozi watu wabaya kwa raia,sasa hivi CCM wanajifanyia mambo yao pale juu wakati CDM wanawekeza kwa watu, sasa watu ndio wanawapa Nguvu CDM pale Juu.Ndcho unachotaka CDM wafuate?Mbona unaprove failure kabla hujaanza wala wazo lako kununuliwa?
Umethibitisha ninachokisema! Kwa hapo hawana tofauti na wabunge wa CCM sivyo? au hujasikia wabunge wa CCM wakifanya hivyo hivyo?
Yaani hujaona tofauti ya kuwahamasisha watu kuchanga kwa kuwapa motivation na hiyo ya CCM kumwaga hela na kuhonga watu chakula?Hiyo ya CDM kuhamasisha ni tofauti na kuwapa hela bure bila kuwawajibisha.Dont tell me you are nt that serious.Wamefanana wapi sasa?

Ouuuch!!! nahofia kuelewa unachokisema. Hili la Ukaskazini limetoka wapi tena? Ni kwamba kuna hisia ya superiority complex ya watu wa Kaskazini? Sitaki hata kudhania umesema ulichosema.
Unadhani sikujua ninachoandika?Niliweka huo mfano makusudi ili nijue ulivyo disperate kungoje hilo.Wato wa ameneo tofauti wana parameters fulani ambazo wana excell over others na wana haki ya kujivunia hilo.Yapo makabila mengine yana excell katika areas tofauti na wa kaskazini na hata kati ya wakaskazini pia wana tofauti zaidi katk hayo maeneo.Ila maeneo watu ni wavivu sidhani kama mtu yeyote anaweza nyimwa haki ya kuucheka uvivu.Haja mkulu ukimuuliza Suala la UVivu kule kwake atakuambia bila kusita.
Thats exactyl the weakness; wametoa hotuba ngapi? Wamezungumza mara ngapi kwa ukali. Wamehotubia mara ngapi majukwaani wakishika vichwa na kupiga mayowe? NIni kimebadilika?

Weakness ya nini sasa?Ulitaka waongee mara ili ujue wameongea?Kushika kichwa na kupiga mayowe kila sehemu kuna maana yake ya timingi yake ktk events.Huwezi piga mayowe wakati watu wameshazikwa ha kuoza.Ndivyo huwezi piga mayowe wakati TISS,police na Akina Shimbo wanasema hayo wanayosema na kufanya.N ahiyo haiwezi kuwa agenda ya maisha.Hizo habari unazoongea ni kama AU na Arab League walivyokuw awakijidanganya kuwa Ghddafi na Bashir wanaweza leta mabadiliko just kwa mazungumzo na vikwazo.Kuna private na public approaches.
Are you serious? really? Kwamba mbinu zake ni unpredictable? Sasa hivi ukiangalia sana ni CCM imewageuka CDM na inawafanya CDM wafuate. CCM imefanya political triangulation na hadi sasa CDM hawajaweza kujibu.

wewe ndio unasema,utageuka nini sasa kama hujui mpinzania wako ambaye kwanza ni flexible anakwenda fanya nini next?Vifo vya watu na hujuma nyingine za CCM Morogoro,Iringa na mwingine ni matokeo ya CCM na vyombo vya usalama kutoweza predict sequence of events.Nashindwa elewa kwanini unafikiri weka theory nyingi,wakati vitu vya CCM vinalipuka prematurely kwa faida ya CDM.kwanini usidhani bado CDM anaweza endelea mtumia CCM kurahisisha kazi.Ujue kazi ndogo ya CDM ina faida kubwa+faida toka kwa CCM.
Sawa waendelee kuzungumza na kuhotubia. Kwani si walizungumza na kuhotubia 2005, 2006, 2007, 2008, 2009, 2010, 2011, na sasa ni 2012. Kama ni hotuba tu kwa kweli si utani zinatia moyo na kufurahisha. Zinavutia watu wengi sana na hili si dogo. Na sitoshangaa kikija kikao kijacho cha bunge tutasikia tena hotuba motomoto; na kikao kijacho cha bajeti nacho kitakuwa na hotuba nzuri vile vile.
Sijaelewa unataka sema nini ?napata tone ileile ya kususa tena.Hiyo milolonho ya miaka CDM hawakuwa na shida na urais.Au hukumbuki?Wewe hutaki watu watiwe moyo na kufurahishwa?Taifa lenye watu disperate na wasio na furaha lipo doomed kufa kama si mfu.mwanakijiji gani hujui vijiji vya ujamaa.Watu walihamasishwa kwa nyimbo na mengine ili wapate moyo wa kuvuka vikwazo.
Yoote haya umeandika kwa kuwa disperate kuiona CDM inafanya vitu vya kufikirika na kutojulikana.Yote uliyoaychukuliwa kama mzaha hapo juu ndipopalipo nguvu ya CDM ndipo panapowafanya wabunge wa CCM walie kuwa CDM wapo majimbo kwao, walie kuwa bunge lisionyeshwe live, sasa kama wewe unataka waongelea hata waathirika wa CCM kwa nguvu ya CDM ya umma.Ni wazi theory zake zinahitaji pewa lab ya kufanyia test.

Kwa taarifa yako agent wa TISS uchaguzi uliopita waliponea bahati sana ktk vituo vya kura,wakaponea mikoni mwa polisi.This time around sijui kama watapona wote wakiingia ktk vituo vya kura kama wataendelea ibuka vituoni kwa mtindo wenye makosa kama ule.Soon CCM wana exaust mbinu zote za kuchukua ushindi.Itabidi tuu wa resort katika style ya Mugabe.n ahata wakifanya hivyo wata collapse katikati.Sasa hivi ni yenyewe tuu ni Mungu anasaidia.Rais ajaye wa CCM itambidi awe akivunja Bunge kila siku na kurudia uchaguzi kwa hela isiyopo.Ipi njia bora kuliko hii?Sasa hivi CCM wameshabanwa sana,na wakipita uchochoroni na mafichoni watajikuwa wakiwa katk lion den.mengi tuu wanafanya mafichoni yanalipukia hadharani.
 
Nimeufutilia mjadala huu kwa makini sana, mwanzoni nilihisi kama nachanganyikiwa, lakini kwakadiri nilivyokuwa nasonga mbele,nilianza kuelewa taraaatiib!

Siko kinyume na MMM, Nicolas, Paco au JMushi na wengineo... wote mna hoja, lakini hamkubaliani either kukubaliana au kutokubaliana, ingawa ukweli utabaki kuwa ukweli kuwa CDM inahitaji mabadiliko chanya ndani ya chama,tuache ushabiki... mimi ni Mwanachama wa CDM kindakindaki, ila kwa kiasi fulani nina mtazamo tofauti.... na niliwahi kuandika humu nikichangia Uzi fulani kuwa CDM kwa mtindo huu tunachezea hazina yetu ya wingu la kupendwa na watu wengi humu nchini.

Nimehudhuria mikutano mingi ya Chama, lakini yote nikaishia kuwa disapointed,kwani kila siku mnaambiwa hamsikii TATIZO kubwa huwa tunatumia asilimia 90 ya muda wetu majukwaani kuchochea hasira ya wanataifa hili dhidi ya CCM, na muda kidogo sana kueleza tutafanya nini (MMM nakubaliana nawewe kabisa juu ya hili) tunaweza kujidanganya kuwa yameandikwa kwenye katiba ya Chama, lakini wananchi wengi tunataka tusikie majukwaani na ndio forum nzuri ya kupata uungwaji mkono mkubwa kama tutatumia jukwaa vizuri.

Muda Mwingi unatumikakueleza Maige ameiba,Lowasa fisadi, Mbunge wenu ......bla blah, blah..... Ingawa ni moja ya strategy majukwaani lakini STRATEGICALY kama CDM tunataka Dola tutumie muda mwingi kuwaeleza wanataifa juu ya sera mbadala....tutafanya nini!!! Kusema Elimu itakuwa bure haitoshi...semapia tutafanyafanyaje kuwa na elimu bure... MMM aliwahikusema kuwa CDM tuna sera za majimbo tueleze watu sera hizi tuanze kuzizoea.... Fikra endelevu hapa ni muhimu sana.

JMushi nakuunga mkono Kamanda wangu kwa analysis yako juu ya mambo ambayo CDM inafanya...M4C inafanya vizuri sana kuwaamsha watu...ila kama ni yale ya Shutuma, shutuma Mkuu hatuna Chetu...Tukumbuke Muda si rafiki yetu... tunapotembea vijijini tuwaeleze na sera zetu...Siku m1 nilikuwa kijiji cha Vinile (Miliamani kabisa kule mgeta-Morogoro) niliwakuta Makamanda wanaeneza CDM, niliwadadisi wanakijiji wa pale walisema kwa mara ya kwanza waliona viongozi wa vyama vya upinzani katika historia ya kijiji chao, nilifurahi kuwa CDM walivunja mwiko ule, nilifurahi pia kusikia baadhi ya ajenda za mkutano ule zilikuwa kuwaeleza wananchi kuhusu CDM nini, bandera ya chama kwa nini inarangi zile na maana yake, (sikupata bahati ya kusikia nyingine),ila nilifurahi and this should be the way foward. ila pia we should go beyond this,MMM amesema kuwa sera za usalama, sera zakimataifa,sera za elimu ya juu nk zielezwe wakati huu muda si rafiki,natukumbuke M4C ni garama hatutawezakupata nafasi nyingine kuwaeleza raiya juu ya sera zetu.

JMushi uliniangusha pale MMM alipokuuliza ni lini na katika mkutano gani waliwahi kusema juu ya sera hizi...ukakumbuka kwa mbali sana elimu ya bure, cement buku 5.... dah....hata mini sijawahikusikia sera za chama zaidi ya kuzisoma kwenye katiba ya chama...uliza vijana wengi mashabiki na wanachama waCDM hawajui why CDM...tunapenda tu kwa sababu CCM ilituudhi!!!Tunatakiwa kwa kweli tukiulizwa popote tuweze kueleza kinagaubaga juu ya sera za chama. NA HUU NI UDHAIFU MKUBWA CDM TULIO NAO!! kweli ukweli unauma lakini lazima tuseme ili tupone. Tuhubiri sera na sio tu kuwa majibu rahisi kuwa tutakuwa na elimu bure nk...tuende mbele zaidi kusema HOW!!!!
 
Ninaamini kama ingekuwa inaweza kujipanga inaweza kweli kuchukua madaraka ya nchi; lakini katika hilo siishi katika kuona potentiality tu nataka iwe katika nafasi ya kuweza kushika madaraka ya nchi. Ukifika mahali na kuona gari linatengenezwa na ukaona linavyoweza kuwa husifii tu na kuanza kuendesha. Unahitaji kuona likiwa limekamilika na kama una uwezo kusaidia kuona linakamilika.

Mbona hujajibu chochote ndugu yangu?Hii potentiality ndio uliyosema imekuvuta.Nikakuleza umeiona kwa vile imefanyiwa kazi na uongozi makini ndi maana hukuona kwa CUF wala NCCR vyeama vyenye kila kitu cha kuvifanya vikubalike ila vinakosa uongozi.Nilifikia mahali nikata uthibitishe kuwa wewe si mmojawapo wa opportunistics around,ukala kona.Ukarukia kwa mwingine kumwambia kuwa hukuipenda CDM kwa umaarufu wake.Nikakueleza unipe tofauti sijasikia majibu.Ki ukweli kuna direct proportionalitie kati ya wingi wa watu na kupendwa, kupendwa na potentiality ya kuchaguliwa.
 
.Mkuu Nicholas, unataka tuendelee kuisema jinsi ambavyo Chadema haijajipanga kwenye kila thread?, au nikusaidie kukuelekeza thread zipi zimejikita kwenye hilo?. Hii ni mifano michache!, nakuomba kama una hoja, nenda kazijibu huko huko na tutakutana. Hii sio thread ya jinsi ambavyo Chadema hawajipanga!.
  1. CCM Imechokwa; CHADEMA Haijajipanga!
  2. Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM...
  3. Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...
  4. CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015

Hakuna ubishi kuwa humu jf wengi wetu ni wanachama, mashabiki na wafuasi wa Chadema. Ukitokea kuwa tofauti, basi unanyooshewa kidole "CCM", "Gamba" etc!. Hawa wafuasi wa Chadema, wengi wao wanakabiliwa na tatizo kubwa sana la kutoukubali ukweli kuwa "Chadema Haijajipanga", na kazi yao ni kukanusha kwa kutumia "negation" kwa kujifariji kuwa kila anae ikosoa CDM basi lazima ni CCM!.

Ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania, utaweza kupatikana pale tuu tutakapo kubali kwa dhati kusimama kwenye KWELI, na ni KWELI tuu ndio itatuweka HURU toka madhila haya tuliyopo!.

Mimi kila siku napiga kelele humu. kuendelea kuiimbia Chadema nyimbo za sifa na mapambio!, hakuisaidii CDM. Mtakuja kukuta sisi tunaoipitisha Chadema kwenye tanuru la moto kwa kuikosoa, ndio tunao isaidia zaidi kuliko hawa wanao iimbia nyimbo za sifa na mapambio kila uchao!.

Tukubali, tukatae, Chadema bado haijajipanga kisawa sawa, inao muda wa kujipanga vizuri!, ila ikiendelea hivi hivi ilivyo, 2015 ni CCM tena!.

P.
haya ndio maeneo CDM hawajajipanga?hembuudia tena kusoma halafu uone kinachoendelea.
 
Are you serious? una matumaini sana ndugu yangu. Ingekuwa umati unamaanisha kura tungekuwa mbali sana. Kutoka umati kwenda kura siyo rahisi kihivyo. HIvi unajua hata ni asilimia ngapi ya wanachama wa CDM wamejiandikisha kupiga kura?

very serious...Nina matumaini sana.kama wewe huna na huna kwa vitu serious then taabu kubwa ipo.Nimeshakudokezas sana tuu hili na wengine ila kwa vile hawakuwa na fikra mbadala wanakomaa tuu CDM haijajipanga.Wapi hawajajipaga hakuna,mpaka waliowatuma wapate fikra mbadala.Kwa muda huu wanabaki tuu na hiki kipande "kataeni msikatae ukweli ndio huo CDM hawajajipanga...".akina pasco,mkandara,mchambuazi na wewe pia.CDM wamekuwa wakifanya kazi ya kuufanya umati umaanishe kura na hilo limethibitika Arusha,Moshi, hai,Igunga, Mbeya,Mwanza,Ubungo ,Iringa etc.Na CCM wamethibitisha hilo kwa kubana daftari lisirekebishwe ktk chaguzi zinazoendelea, na hata kabla ya uchaguzi mkuu.Sasa kama bado una hizo fikra za enzi ya akina Mrema basi hata hiyo potentiality ya CDM unayoisema ni wazi huijui kabisa.Ungeijua basi ungejua kwani fikra zako,hofu yako na makeke mengine ni kwa vile wamefanya hilo.Huwezi sema watu walio tayari kufa kuliko kuwakosa mkutano wa CDM hawaendi piga kura.Mkuu naona sasa umeamua kwa dhati kufnaya mizaha ktk masuala yanayohitaji tafiti na good observations.kawaulize TISS kwanini agents wao wanakuwa very busy kuvamia vituo vya kura.game waliyopigia Arumeru watapigia zaidi nchi nzima.Kama ni mamluki CDM walio effective ndani ya CCM kwa ngazi zote kuliko kichume chake.Kama nguvu ya umma, CDM wanazo, kama ni wapiga kura wengi CDM inao kuliko, kama ni kuvurugana CCM wapo ICU.
 
..........Mkuu Mzee Mwanakijiji, uwongo ukisemwa sana na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, mwishowe huonekana ni ukweli. Aliyesema wewe umesoma UD ni huyu na hukukanusha popote!...........
teh teh.imebidi nikiangalia hiki kwa makini...Ndio maana mnarudiarudia sana kuhusu CDM huo ujinga wenu?
 
Well, what can I say? Sijawahi kukimbia swali la mtu kwani hakuna swali lisilojibika. KUna maswali mengine ambayo siyajibu tu kwa sababu nitakuwa narudia majibu ambayo tayari yapo. Na kama ni uongozi hujui kitu kimoja - I hate politics! Siwezi kuwa kiongozi wa kisiasa; at least sivyo kama ilivyo sasa.

kweli?
 
Sijawahi kusoma UDSM; usiamini sana masimulizi yanayonihusu humu.

Mbona mengi yako pia hayaaminiki?Kwanini na hili nikuamini wewe na nisimuamni mwingine?Hembu liweke sawa hilo.Hata kama hujasoma pale simulizi zako nyingi zimejionyesha zipo influenced na nadharia za wasomi wa pale ambao wametokea kuwa public figure.
 
Mzee MM, nini maoni yako juu ya chaguzi zinazoendelea ndani ya chama tawala pamoja na madai ya baadhi ya wagombea kuwa kumekuwa na matumizi makubwa ya fedha. Je hii itaathiri uchaguzi mkuu 2015?
 
Mkuu umejitahidi sana kuelezea mitazamo yako. Ila kuna vitu vipo clear hapa, hiyo kambi nyingine inayotaka mabadiliko kwa CDM hawana sababua ya msingi kwanini wasitake mabadiliko kwa wengine. Na mabadiliko wanayotaka wakiambiwa wayaseme hawana cha kusema wanarudi ground zero kusema kuwa haijajipanga na junks nyingine.

Hakuna mtu kasema CDM wapo perfect na kuwa time inavyo-change hawatakiwi badilika. CDM wapo busy kufanya mabadiliko na mipango ya kina ili wasiwe wanahitajikahitajika kufanya marekebisho hovyo.

Sera za chama zimeelezwa sana na nyingine CCM wamelia nazo sana ila time inavyokwenda ndivyo wanavyozidi weweseka kwani zinazidi kuwa reality.

Kwanza mjue hakuna sera 100% applicable nchi nzima na hivyo sera ya majimbo is double plus. Majimbo mengi yatakuwa na mipangilio yao inayo-fit ktk mazingira yao. Na si hizi habari za CCM za ku-centralize kila kitu. Sasa hivi kuna wilaya zinapokea hela kipindi cha kufunga mahesabu, na hivyo kuishia rudisha hela hazina. Majiimbo yatakuwa na uhuru wa kujipangia mambo yao na kutumia hela yao bila kusubiri hela ya serikali kuu ambao itahitajika ktk mambo ya dharura na mipango ya kitaifa. Sioni sababu ya watu kukomaa na kila kitu ingawa CDM wanayo. Kwani bado watahitajika kuyaachia majimbo sehemu zao kumalizia yaliyobaki kwa kutumia wawakilishi wa CDM ktk hayo majimbo.
 
Hapa WOWOWO nipo na wewe 100%. kwenye red hapo political scientists wanaita cooptation, na inakubalika kabisa kisiasa, na kinachofanyika ni kujaribu kuvunja nguvu ya upinzani kwa kuiga mipango mikakati na mawazo yao yenye mashiko na kwasababu wao bado wananguvu ya miundombinu na rasilimali inakua rahisi kuhalalisha mbele ya umma kwamba ni initiative zao!! sio tu mawazo hata watu (i mean potential leaders) wanakua coopted!! that how system works...

Bado naamini cdm hawajafanya vibaya kwa kutumia precautious publicity tactic maana wanajua upande wa pili kuna njaa kubwa ya ideas na mipango!! na mfano ndio huo wa V4C!!!!

kiukweli vita ndio hii... kuendeleza mapambano ya kukosoa na kuonyesha dhahiri namna sera na mifumo ya upande wa pili zilivyoshindwa na zinavyodidimiza azimio la kuondoa umasikini, ujinga na maradhi kwa mtz!! while at the same time wakiconstruct a model yanamna watakavyoweza kubadili na kuleta maendeleo. (without disclosing the contents)


umemaliza kabisa mkuu.Ni jukumu la akina MMK kuonyesha ni wapi haya maelezo yako yanakataa.
 
Acha kuabudu watu wewe mtoto wa kiume, umezaliwa mkamilifu, una akili timamu, unapojidharau kanakwamba akili zako si lolote wala chochote mbele ya mzee mwanakijiji unausikitisha umma!

Nyinyi bado mnagombana na nadharia wenzenu cdm wanatia fikra zao vitendoni, nisubirini ninywe togwa niwashushie mistari.

Nipo proud kwa the way nipo,kama fikra zako zinakutuma kuamini kuwa mtu akikubaliana na mawazo ya mtu mwingine basi ni kumuabudu nadhani sijui fasiri sahihi ya lugha na hasa neno kuabudu.

Binafsi nina watu ambao kwa mawazo yao ama fikra zao chanya ama hasi wananijenga,nikufahamishe tu kuwa hata wewe kwa kauli yako umenijenga sana,kuruhusu fikra za wengine kuingia katika kichwa changu kuna nipa fursa ya mimi ya kufikiri kuanzia hapo anapoishia mwenzangu na kwenda mbali zaidi,Mzee Mwanakijiji amekuwa mwandishi na mchambuzi wa mambo ya kisiasa kwa muda mrefu labda karibuni ameingia ktk tasnia ya mahusiano{mapenzi} lakini nimejipa nafasi ya kujifunza atoka kwake,ninakubali kazi yake na hakika sijisikii vibaya kuendelea kujifunza toka kwake.

Huwezi jua labda kama nawe ni mwandishi mzuri ktk eneo lako fulani naweza kuwa nimekuweka miongoni mwa watu ninaojifunza toka kwao kama role model wangu.
Mkuu si vizuri sana kulazimisha watu wawaze uwazavyo kwa kwa kuwa tupo jamvini kwa mambo mbalimbali,but mie nipo hapa kujifunza what others think on different issues,sasa kama unadhani kukubali kazi ya mtu ni kuabudu basi kuna tatizo sehemu fulani.Kila mmoja apewe sifa anayostahili na kwangu kujifunza hakuna mipaka wala ukomo bali mauti yanitoe duniani.

Naheshimu mawazo yako mkuu na singependa kuharibu nia yako njema ya kinijenga,kumbukumbu zangu zinaonesha kuwa ili niwe mimi kuna watu wa aina mbali mbali walijitoa muda wao,maisha yao,rasilimali zao ili kunijenga mimi hivyo si busara kwangu kutoonesha kujali uwepo wao hata walau kuonesha kuwa nipo nyuma yao.
Inawezekana uwezo wako katika kujenga hoja ni mkubwa kiasi kuona kwamba mtu akitoa sifa kwa mtu mwingine na si kwako unaumia,si mbaya mkuu lakini jaribu kutizama mimi ni JF SENIOR EXPERT MEMBER,kuna watu wamenilea kuyajua mambo nje na ndani ya JF,nawashukuru na always niko pamoja nao ili wasiniache mbali wewe ukiwemo,So hakuna ubaya kama natambua mchango wako ktk kunifanya kuwa mimi wa sasa.

Labda niseme tu kuwa mkuu,napenda na nitaendelea kupenda mawazo yako mazuri yanayonisaidia kujua position yangu kiuelewa na kiuchambuzi.Naomba usichoke kunifundisha na labda siku moja nami nitageuka kuwa Role model wako na tukakaa sehemu tukagonga cheers!Uwe na wakati mzuri mkuu.
 
Mbona mengi yako pia hayaaminiki?Kwanini na hili nikuamini wewe na nisimuamni mwingine?Hembu liweke sawa hilo.Hata kama hujasoma pale simulizi zako nyingi zimejionyesha zipo influenced na nadharia za wasomi wa pale ambao wametokea kuwa public figure.

Sijawahi kumsoma mwanachuoni yeyote wa pale kwa kiwango cha kusema nimekuwa influenced nao au naye. Kwa hiyo sijui wasomi wenu hapo wakoje au wanasimamia nini. Kwa vile sijawahi kusoma hapo (na sikuwahi kufikiria kusoma hapo) siwezi kuzungumzia hayo ya UDSM.
 
teh teh.imebidi nikiangalia hiki kwa makini...Ndio maana mnarudiarudia sana kuhusu CDM huo ujinga wenu?
Ujinga wetu ni nini basi? Je una athari zaidi ya upuuzi wako na wa wenzako ambao mnataka watu wote waimbe sifa za CDM bila kukosoa au wakosoe sirini kana kwamba ni chama kisichostahili kukosolewa? Ujinga wetu ni nini kudai na kuonesha bila kuwiwa na mtu kuwa CDM kama ilivyo sasa ikishika madaraka tutakuwa na tatizo lile lile ambalo tunalo ndani ya CCM yaani siasa zenye kufuata watu, sera zisizoangaliwa na kuandaliwa vizuri na mfumo mzuri wa kutawala? Ama ujinga wetu nini hasa kulinganisha na upumbavu wa kushabikia chama ilimradi ni chama? Ama ujinga wetu hasa ni nini? Kwamba tunapenda CDM na tunaamini inahitaji kujengwa kujiandaa kushika madaraka ya kuliongoza taifa siyo kutawala? Au ni ujinga gani unaozungumzia ule wa kusema uongozi wa CDM ulivyo sasa umenata kwenye watu kiasi kwamba fikra za kutoka nje zinakutna na ukuta wa kukwamisha ambao ni mgumu kubadilika kama vile ilivyo CCM?

Ama ni ujinga gani ambao tumeudhihirisha zaidi ya kusema kile ambacho tunaamini na kukiweka bayana kwa kila mtu kukiona? Kwamba hatuamini umati wa watu; kwamba kwa vile watu wengi wanajitokeza kwenye mikutano na kuvaa nguo za rangi ya CDM haina maana ni wingi wa kura? Au ni ujinga upi huu?

Au ni huu wakusema kuwa miaka miwili baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 na mitatu kabla ya ule wa 2015 CDM bado ni chama kile kile? Kina katiba ile ile, kina mifumo ile ile, kina mwelekeo ule ule na dhana zile zile? Kwamba hakijajionesha kuwa kiko adaptive na adoptive wa siasa mamboleo (modern politics) na badala yake kimeendelea kutumia mifumo ile ile iliyoundwa na CCM. Leo hii bado Kamati Kuu ya CDM ina nguvu za kuinfluence local politics kama vile ilivyo kamati kuu ya CCM? Ama ni ujinga wa watu kusema CDM inahitaji kujipnga, kuboresha miundo mbinu yake, kusasaisha sera na mwelekeo wake, na kutengeneza taasisi zake ambazo zitahakikisha kinatoka kuwa chama cha upinzani wa kuduma na kuwa chama kinachoweza kushika utawala wa nchi.

Wakati mwingine ujinga wetu una hekima zaidi kuliko werevu wenu.
 
Back
Top Bottom