thats exactly my point...
Unajua watafanya nini kuhusu usalama wa taifa? watafanya nini kuhusu polisi? watafanya nini kuhusu elimu yajuu? hivi umesoma lini kweney hiyo mikutano ya majukwaani ambacho CDM watakifanya. Nitafutie mkutano mmoja wa karibuni ambapo CDM wamesema wao wakiingia madarakani watafanya nini kunipa mfano.
Nilishawahi kusikia kwamba elimu itakuwa bure licha ya kwamba sikumbuki vyema the details.Pia nilisikia issue kama mfuko wa sementi kuwa elfu tano.Kwa ujumla,walisema watalishghulikia pia tatizo la mfumuko wa bei.
Hayo ya polisi na mengineyo,nakubali kuwa wanaweza kuyazungumzia.Lakini kumbuka hata mwalimu alipochukuwa nchi,hakujuwa alifanyie nini jeshi hadi pale aliponusurika kupinduliwa.
Kiukweli mkuu,ninaamini kwamba hayo maeneo yote yanahitaji overhaull,na ninaamini kwamba kuiondoa ccm madarakani ni kama uhuru wetu wa pili.Only this time ni kutoka kwa mkoloni mweusi.
Ninachoweza kusema,ni kweli nakubaliana na wewe kwamba wanatakiwa waseme ni kwa kivipi wataoperate,licha ya kwamba wanajitofautisha na ccm,lakini ni vyema wakatanabaisha kuwa mabadiliko hayo yatakuwa ya namna gani.
Lakini ebu tuchukulie tu mfano mmoja wa serikali za majimbo,je hujui namna zinavyo operate ama mfumo huo unavyofanya kazi?
Je hujui namna serikali isiyokuwa na ufisadi namna inavyo operate?
Hujui ni namna gani mikataba ikiingiwa kwa manufaa ya taifa ni kwa namna gani wananchi watanufaika na mikataba hiyo?
Hayo tu yenyewe yanaweza kukupa mwangaza kwa mbali.Lakini hilo la kuwepo na details,nadhani ni suala ambalo wanahitaji kulifanyia kazi.
Pia unaposema hujui watafanya nini kuhusu usalama wa Taifa una maanisha kitu gani?Kwamba wataivunja hiyo taasisi?Ama una maana gani haswa kuhusu national security?
Ina maana una wasiwasi na chama hicho kuhusiana na kumaintain national security?
Ama unamanisha ni kivipi wataifanyia taasisi hiyo mabadiliko?