Proper recording: Nini kilimbadili Mzee Mwanakijiji?

Proper recording: Nini kilimbadili Mzee Mwanakijiji?

Ukweli husemwa:



Mkuu, hayo maneno kwenye red yana maana gani au ulikuwa una maana ya cartography na stenography.


jaribu kuya google hayo ya kwangu kama yalivyo...kisha ya kwako......usichanganye
 
Wakuu, binafsi nilikuwa shabiki wa huyu mkongwe wa JF. Nikagundua kwamba MMK amechanganya fani mbili tofauti na hivyo kujichanganya na kuchanganya wasomaji wa posts/makalazake. Nikaacha kufuatilia na kusoma anachokiandika.

MMK amechanganya SIASA na UANDISHI wa habari.........


kama umeacha kumsoma ni wewe wengine humu ni mentor wao!!.....unafikiri wote wanaoandika kwenye magazeti ni waandishi wa habari??...usicheze na mtu aliyebobea kwenye Intensive course in Nationalism & Espionage halafu akachanganya na madude mawili niliyokwisha kuyataja!!.....juzi humu ndani mlimpoke kwa mbwembwe kibao dada mmoja kisa ametoa speech kali huko nkurumah....wengine wakamwita jembe na wengine mpini na wengine wakataka awe mwenyekiti wa bawacha....sasa mnaona huyu mmk anasema alimkubali kikwete 2005 kisa wengi walimpenda!!!!....ni mzee wangu tu ndiye alimkataa mapema kabisa maana alimfahamu viuzir akasema kwa kimombo...''the country is going to have the president who cannot think beyond the next meal'' .........na hakumpa kura

jaribuni kuwa na jicho la ndege katika kutathmini watu...speech moja haimpi mtu ushindi wa sunami hadi mnataka awe mwenyekti wa bawacha..mkiendelea hivi mtachanganywa sana...
 
mi nasema ivi let there be hapa tanzania wanakijiji kam 100 ivi, watu tuelimike... mwanakijiji ni mfano wa manyerere waliobaki wasiofungamana na upande wowote....tutasonga.
 
sidhani kama nimesema kuna umimi; CDM ndicho chama pekee sasa hivi kinachoweza kujipanga na kuchukua madaraka ya nchi. Kumbuka kina mtaji mkubwa sana wa mapenzi ya watu wengi. Wapo watu wengi ambao wamejitolea na wanaendelea kujitolea hali na mali kukijenga. Lakini hili peke yake la kupendwa halitoshi kufanya wawe wanastahili. Fikiria hapa ninachokisema vizuri.

Mkuu MMM,
Hoja yako kuu ni kuwa CDM haijajipanga, hujaelezea kuhusu M4C inayoendelea kama sehemu ya kujipanga! Pia unalalamikia migawanyko iliyopo CDM huku ukisahau kuwa CCM ni chanzo kikuu cha migawanyiko kwenye vyama vya upinzani! Nakuona kama mtu wa kukata tamaa haraka sana japokuwa unataka kujiaminisha kuwa "hushabikii matukio" bali fikra! Ukisoma between the lines kwenye hoja zako zimejaa matukio zaidi kuliko kile unachokiita fikra, ndio maana umeanza na kabla ya uchaguzi na baada ya hapo, huku ukionesha kuchanganyikiwa kuwa ubaki CCM au CDM! Sijui kama wewe ni mtu wa msimamo kama ulivyofanikiwa kuwaaminisha wengi! Mada yako kwa ufupi imenishangza sana, unatumiwa na CCM kama ilivyo kwa akina Zitto Kabwe, usitudanganye, huwezi kuwatumikia mabwana wawili (CCM vs CDM)!
 
Mzee Mwanakijiji,nimeitafuta nakala ya "Pembe tatu ya ushindi",sijaweza kuipata.Nimeifuata hiyo linki uliyoiweka, lakini sijaona hiyo makala yako.Kama kuna uwezekano,naomba utuwekee hapa ili tuweze kuendelea na mjadala tukiwa na nakala zote.

However,umesema kwamba ulishiriki kuandika ilani ya uchaguzi wa 2010.So hapo labda hakuna tatizo kwa upande wako.Pia inaonekana sera na itikadi siyo tatizo kwa chadema.

Hivyo basi,baada ya kupitia makala zako,na kusoma bandiko lako,nimegunduwa kwamba mzizi haswa wa fitina wa chadema kutokuwa tayari kushika madaraka ya nchi,kunaweza kuwa summerized kwa kutumia maneno yako hayo hapo chini,kama niko wrong unaweza kunisahihisha,na kama kuna nyongeza,basi unaweza kufanya hivyo(kuongeza),ebu tuanzie hapo kama ikiwezekana...
Mzee Mwanakijiji said:
Kilichobadilika zaidi ni kuwa ninaelewa zaidi kuwa wanasiasa wanataka mabadaraka zaidi kwa ajili ya madaraka. Ni kama Kikwete alivyoutaka Urais kwa ajili ya Urais. Mbowe bado hajaonesha uongozi na kipimo cha kushindwa kwake kilionekana 2010; viongozi wengine ndani ya CDM nao wanapata shida ya kuonesha uongozi na badala yake kuelekea 2015 CDM inaweza kwenda ikiwa imegawanyika kuliko CCM!

Wanaofikiri kuwa ati itakuja kujipanga baadaye wanajidanganya. CDM ilitakiwa iwe imeshajipanga sasa hivi kuelekea uchaguzi wa 2014 na ule wa 2015. Badala yake mwaka huu tumeshuhudia malumbano ya ajabu sana na visa vya ajabu vikitokea. Utagundua kuwa sijawahi kwa mwaka huu kutoa maoni yangu kuhusu hili kabisa na labda nitalitolea maoni lakini naendelea kukata tamaa na inakatisha tamaa! Nilisema wakati wa uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki ningekuwa na uwezo ningewatia bakora viongozi wa CDM na nilimaanisha! Na nilisema wangepoteza Arumeru Mashariki Mbowe na uongozi wote wa juu wangetakiwa kujiuzulu; na hata sasa labda kesi inaweza kujengwa ya kwanini wajiuzulu mapema zaidi (bado sijamaliza kuijenga hii hoja, inshallah).


Bado siamini kuwa CDM ilivyo sasa iko tayari kushika hatamu za uongozi wa taifa letu. Ndio maana utaona kuwa mimi pia siyo muumini wa "tuiondoe kwanza CCM halafu tutajua mbele ya safari". Siamini katika kuiondoa CCM ili tuingize chama kingine alimradi turidhike kuwa tumeiondoa CCM. Ninaamini yatupasa tuiondoe CCM kwa sababu kuna chama kingine kina sera na dira nzuri kwa taifa; kina viongozi wenye busara, na kinasimamia kanuni za msingi zilizojenga taifa letu.
Umesema kipimo cha kushindwa kwa mwenyekiti wa chadema ni 2010.Kukweli mwaka huo,chadema walikuwa na matumaini makubwa,na hata waliamini kwamba uchaguzi ulichakachuliwa.

Lakini kwa maelezo yako hapo juu,ni wazi kwamba wewe unaamini tatizo lilikuwa ni uongozi na specifically wa mwenyekiti wa chadema.

Binafsi nikiangalia matatizo ya mwaka huo,ni ukweli kabisa kwamba kulikuwepo na matatizo kwa viongozi,kuna kiongozi/viongozi ambao hawakuridhia hata mgombea urais wa chadema mwaka huo.

Kuna rumours(naomba kuelezwa kama ni kweli),ya kwamba kiongozi wa chadema alitokea kumsapoti mgombea wa ccm,na kwamba hakushiriki kwenye kampeni za mgombea wa chama chake!

Hilo lilinishtua sana,kwangu mimi ccm na chadema ni kama kiza na mwanga,ama hata usiku na mchana ukipenda.Ndivyo ninavyoona utofauti huo,kiasi cha kwamba pale niliposikia hayo,nilishangazwa sana.

Unayosema yalitokea 2010 na maybe beyond that,bado yapo(msisitizo kwenye uongozi kama nilivyosema hapo awali),the buck stops at the top with the chairman,hilo sikatai.

Kwasababu uwepo wa hizo zinazoonekana kuwa kambi,kwa namna moja ama nyingine,kunahatarisha uhai na maendeleo ya chama hicho kwenye kuelekea kuitaka ridhaa ya wananchi ya kuliongoza taifa letu.

Umezungumzia kuhusu Arumeru,wakati ule kusema ukweli,tatizo ambalo nalikumbuka pia bado ni hilo la uongozi,kuna viongozi ama kiongozi aliyekuwa akitoa kauli ambazo wala haziendani na kile kilichokuwa kikifanyika(kumkampenia mgombea wa chadema),badala yake ni kutangaza nia ya kugombea urais,pia sikumbuki kama kiongozi huyo alishiriki kampeni hizo.

Kimsingi,umeonyesha kwamba kugawanyika kwa chadema ndiko kunakoonyesha kwamba hawako tayari kuchukuwa madaraka.Jambo ambalo nalipinga kabisa na ndiyo maana nikasema ni kama unawaonea.

Mkuu kuna chama kilichogawanyika kwenye uongozi kama ccm?Tulishuhudia sana hayo kuanzia kwenye kumpata mgombea wao mwaka 2005.Tena hayo hayakuanza mwaka huo.Unajuwa wazi kabisa kuwa kama si mwalimu Nyerere ambaye alitumia udikteta kiaina,basi hata mwaka 1995 waligawanyika sana.

Utofauti wa ccm ni kwasababu ni chama kikubwa na chenye rasilimali nyingi na ofcourse madaraka,ni chama chenye dola nk.Ndiyo chama kilichokuwa kikishika hatamu,yani ikiwa na maana kwamba hata katiba ya ccm ilikuwa juu ya katiba ya nchi!(madhara yake yanaonekana hadi sasa)

Hilo huoni kwamba lilieta utofauti?Sasa chadema wamekuwa nani hadi wasiwe na migawanyiko?

Mimi ninapopingana nao,ni namna wanavyohandle hiyo migawanyiko.Hawataki kuchukuwa maamuzi magumu kwa maslahi ya chama na kusonga mbele.Hilo litawacost,kwasababu nilishawaambia wasuke ama kunyoa,wangefanya hayo,basi ungekuta sasa hivi wana worry about kuendelea na ujenzi wa chama.

Ni bora kuwa na wananchama wachache wenye moyo wa kweli wa kukijenga chama,kuliko kuwa na wanachama wengi ambao ni wafuata upepo tu.

Kutokuchukuwa maamuzi magumu kwa chadema kutawacost.Hilo ndiyo bottomline kwa maoni yangu.Na nilishawaambia kwamba wasipoziba ufa watajenga ukuta.

Hatutaki wapate washindi wa kambi hii ama kambi ile,lakini mkuu kama haukionei chama hicho,na kwamba uko radhi ccm ibakie madarakani kwasababu ya mgawanyiko huo wa uongozi/kambi,je kuna chama chenye kambi kama ccm?

Wewe binafsi,inaelekea kuna tatizo ambalo chadema wanalo na hata wakifanya kitu gani hawataweza kulitatua.Uliamuwa kabisa kupeleka sapoti yako kwa ccj na huku ukiwa hujui chochote kuhusu chama kile.Ulisema ulifanya hivyo ili upepo wake ukisukume chadema!really?Na ulipoisapoti chadema ulitaka upepo wake ukisukume chama cha ccm?

Hapa unani confuse sana tu kama vile ambavyo wengine wako confused kwa kusema unabadilika badilika.Hilo siyo jambo la maana kabisa,you should be a person of conviction.Na problem solving(kwa madhumuni ya kujenga), haiendi hivyo.

Pia kwakukusoma katikati ya msitari,sioni kama una nia haswa ya kuwasaidia hao chadema waondokane na hilo tatizo la kutokuwa tayari kushika madaraka.Nina mashaka sana na hapo mkuu sikufichi,ebu niambie maana haswa ya kipengele hiko hapo chini...
Wanaofikiri kuwa ati itakuja kujipanga baadaye wanajidanganya. CDM ilitakiwa iwe imeshajipanga sasa hivi kuelekea uchaguzi wa 2014 na ule wa 2015.

Kwenye red,umeshatoa kabisa imani yako na chama hicho,so why bother?

Halafu unaposema ilitakiwa iwe imeshajipanga kabla ya sasa kuelekea uchaguzi wa 2014 na 2015,kwa kukusoma btn line,ina maana kwamba wameshachelewa,sasa kwanini usiwaambie wazi kabisa kwamba jitihada zao(kama wakijipanga sasa),basi zitakuwa ni kwasababu ya uchaguzi wa 2020 ama 2025?

Umenishangaza sana mkuu,sana tuu!Sidhani kama wewe ni mpinzani,kiukweli watu wanaodoubt wana sababu kubwa kabisa za kufanya hivyo.Wacha niishie hapa kabla sija drawa much conclusions kwasababu na wewe upo hapa na utajibu haya kama ukitaka.

Bado naendelea kuzipitia makala zako na kuzitafakari kuona kama una nia gani haswa.
 
Last edited by a moderator:
jmushi1 usifikiri mwanakijiji wakati anaisapoti CCJ lengo lake lilikuwa hilo ulilotaja(kuisukuma chadema) .lengo lilikuwa kinyume chake...na ukosoma jibu lake humu utaona kabisa bado hana nia ya kuisukuma chadema mbele... halafu huu usemi alioacha baba wa taifa...''ccm sio mama yangu'' ....kuna watu wanaingia kwenye vama fulani wanavuruga kisha wanaapply usemi huu na kusepa
 
Last edited by a moderator:
Vision ya chama haiwezi kua kuondoa chama tawala madarakani. That is merely a consequence of the take over. What is the vision of CDM concerning key areas ya utawala? I believe that is what Mzee Mwanakijiji meant: Sio CDM ishinde ili [tu] CCM itoke madarakani.
Unaposema "vision concerning key areas ya utawala" una maana gani?Unaweza kufafanua zaidi ili tukuelewe specifically kile unachomaanisha?
 
Mkuu MMM,
Hoja yako kuu ni kuwa CDM haijajipanga, hujaelezea kuhusu M4C inayoendelea kama sehemu ya kujipanga! Pia unalalamikia migawanyko iliyopo CDM huku ukisahau kuwa CCM ni chanzo kikuu cha migawanyiko kwenye vyama vya upinzani! Nakuona kama mtu wa kukata tamaa haraka sana japokuwa unataka kujiaminisha kuwa "hushabikii matukio" bali fikra! Ukisoma between the lines kwenye hoja zako zimejaa matukio zaidi kuliko kile unachokiita fikra, ndio maana umeanza na kabla ya uchaguzi na baada ya hapo, huku ukionesha kuchanganyikiwa kuwa ubaki CCM au CDM! Sijui kama wewe ni mtu wa msimamo kama ulivyofanikiwa kuwaaminisha wengi! Mada yako kwa ufupi imenishangza sana, unatumiwa na CCM kama ilivyo kwa akina Zitto Kabwe, usitudanganye, huwezi kuwatumikia mabwana wawili (CCM vs CDM)!

‘The Italian Strategy of Tension with False Flag' ndiyo njia anayoitumia mmkjj...
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji,ebu kuwa fair kwa chadema tafadhali,ni ombi tu mkuu!Ebu ona unavyojichanganya na kutuchanganya at the same time...Hapo chini ni kigezo kuhusu mgombea ama kiongozi wa chadema.

Mzee Mwanakijiji said:
Sivutwi na hotuba hewa, au na mivuto ya umaarufu wa watu. Sipimi watu kwa kuangalia nani anaungwa mkono zaidi au nani haungwi mkono. Ninapima watu kwa fikra zao na mambo wanayoyasimamia lakini kwa jinsi gani wanaongozwa na kanuni (principle oriented) kuliko wanaoongozwa na matukio (events-oriented). Watu wanaoongozwa na matukio huitikia matukio yanapotokea; wanaoongozwa na fikra huitikia hata wakati kuko kimya!

Na. M. M. Mwanakijiji
Lakini tena kipimo chako wakati wa JK kilikuwa hicho hapo chini...

Mzee Mwanakijiji said:
"Kikwete alipopitishwa na kuwa mgombea wa Urais mimi nilikuwa miongoni mwa watu ambao tulimuunga mkono kwa sababu mbalimbali. Ya kwangu ilikuwa ni sababu ya kisiasa zaidi. Kwamba, alionekana kupendwa na kukubaliwa na wananchi wengi sana."

Mkuu hizo ni double standards zinazoonyesha uonevu wa wazi kabisa!
 
sidhani kama nimesema kuna umimi; CDM ndicho chama pekee sasa hivi kinachoweza kujipanga na kuchukua madaraka ya nchi. Kumbuka kina mtaji mkubwa sana wa mapenzi ya watu wengi. Wapo watu wengi ambao wamejitolea na wanaendelea kujitolea hali na mali kukijenga. Lakini hili peke yake la kupendwa halitoshi kufanya wawe wanastahili. Fikiria hapa ninachokisema vizuri.

Anyway wether umesema au lah si issue, kwani lengo langu ni kujadili na si kubishana.Sijui umekiri au ni lugha tuu kuwa na options chache kuwa CDM wanauwezo wa kujipanga kuchukua madaraka.Sijui kama wana uwezo na nia nini tena mnataka washauri?

Umekiri kuwa wana mtaji mkubwa wa mapenzi ya watu wengi.Ila ujue pia utakuwa na kipindi kigumu sana kukataa kuwa huo mtaji umejengwa kwa mipangilio na uongozi bora na si vinginevyo.Sasa hivi CDM ni envy kwa vyama vingine.Hizi blah blha kuwa CCM imechokwa ua inashindwa haiwezi explain kwa nini Si CUF ,NCCR au mwingine aliyekuwa juu ya CDm anaweza grab chochote.Kwa sasa CDM wanaonewa wivu mpaka na watu wasiojua wachukue njia ipi kujiingia katk siasa.Watu waliochelea ingia CDM na sasa wanajiuliza mswali ingia CCM sasa wanishia kupata hasir ana wivu.Kwa vile wanaona wamechelewa jiweka mahali pa kupata ubunge wa bwerere kama wa CCM.

Kama CDM wameweza beat all odds na kuweza vuta mapenzi ya watu wote hata wale wanaofundishwa ktk makundi yao kuwa CDM si ya kwao, bado wanaruka ukuta wakawe na mpenzi wao mpya CDM, wamekuwa na mipango inayowavunja hadi wapinzani kwanini unsema hawastahili?Kwangu naona kama vile wale watoto wa Dar, wanaoona kijana wa mkoani akipendwa na warembo kiasi cha kuwa na uhuru wa kuchagua wakati mabishoo wa wa mjini wakijituma sana kujaribu tumia fahari zao.Mwisho huishia sema kuwa huyu jamaa hastahili mchukua huyu demu.Huyu ni mrugaruga tuu...Hapo ndio unajiuliza nani wa kusema mwanamume anastahili au lah?Kama raia watapiga kura na CDM kushinda kwani utumie neno hash hivi kuwa "si wanastahili?"

Tupe maelezo.
 
1.MKJJ yuko katika payroll ya Serikali katika kazi ya usalama wa Taifa. Majukumu yake hayafuati muundo wa kawaida(organogram) uliopo.

2. MKJJ ni mhitimu wa shahada ya kwanza (BA in Political Science)- Tanzania na pia Shahada ya uzamili (MA in Mass Communication & Media Arts)- USA. Baadaye alifaulu vizuri sana mafunzo ya upelelezi (Intensive course in Nationalism & Espionage) – Cuba chini ya Mwalimu wake gwiji aliyempenda sana kwa jina Mosses Powel . Hii inaeleza sababu ya MKJJ kupewa nafasi ya kuwa muhudumu (Usher) mmojawapo katika mazishi ya Powell 22.01.2005. Alipelekwa pia Trinidad & Tobago kwa ajili ya mafunzo ya ukakamavu na ulinzi wa kujikinga chini ya kitivo cha Powell ambaye ndiye mwanzilishi wa mashambulizi ya Sanuces Ryu Jujutsu lakini bahati mbaya MKJJ hakuwa mzuri sana katika somo hili.

MKJJ baada ya kushauriwa , alichagua kuendelea zaidi kubobea katika mbinu za kipepelezi za steganografia (steganography), Saitografia (Cytography) na Utafiti (Research) siraha zilizompa nafasi kupata mazoezi kwa njia ya vitendo katika Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Ministry of Defence).


3. Kwa sasa MNKJJ anafanya kazi ya kunusa na kuwachanganya Watanzania kwa kuandika na kuongea kwa style ya kukandia Serikali kwa sana kupitia majamvi na majukwaa mbalimbali kama vile JF na magazeti mbalimbali yaliyo katika mtandao.

4. Kwa kutumia utaalamu wake wa sanaa na fani ya uandishi na utangazaji, MKJJ anajificha ndani ya mbinu ya kijasusi ijulikanayo kama ‘The Italian Strategy of Tension with False Flag'. Ingawa ni mwanachama CCM lakini anapokuwa mtandaoni huvaa ngozi ya mbwa mwitu na kujiita Mkuu wa Taasisi ya Kitanzania ya Demokrasia, Maendeleo na Amani (TAKIDEMA). Kazi zake ni kama ifuatavyo:-

a. Kuanzisha mada chokozi (provocative topics) zenye kuleta hisia kali akisukuma makombora kwenye Serikali ikiwa ni namna ya kuwachokoza wananchi ili mnapoanza kusema au kuandika basi yeye anachukuwa notisi zake na kuwakabidhi waliomtuma kwa ajili ya kurekebisha panapotakiwa haraka iwezekanavyo mfano katika moja ya jibu lak leo humu katika thread hii amesema aliyependekeza IGP Mahita aondolewe na ndie alitoa pendekezo la kugawa Dar-es-Salaam kama mikoa ya polisi (kanda). Pendekezo hili lilichukuliwa mara moja.. Hadhira yake kusudiwa ni hasa Watanzania walioko nje na hususani wasomi ambao wanaweza kuleta upinzanina ndio hawa aliokwaruzana nao wakati anapinga swala la uraia wa nchi mbili. sababu iko wazi nayo ni "you are either with us or against us.....I'M out!!
 
Vision ya chama haiwezi kua kuondoa chama tawala madarakani. That is merely a consequence of the take over. What is the vision of CDM concerning key areas ya utawala? I believe that is what Mzee Mwanakijiji meant: Sio CDM ishinde ili [tu] CCM itoke madarakani.
CDM haiwezi uliza watu wenye loosing spirit chochote.kama wote hapa hamkuweza ona ilipoanzia CDM na vikwazo vilivyorukwa, ni vipi mnaweza elewa vision ya waanzilishi wa chama?Ni kama mazaramo anayefikiria kwenda mcheza ngoma binti yake akitaka mshauri mchaga kuhusu shule na biashara.

Jamani acheni ujinga na uzembe,hizi nafasi mnazojipa za ushauri wakati hakuna mlichoweza achieve ni kufuru na matusi.Kuna mwenye pilot chama aliweza kitoa hata hatua moja kwenda nyingine?My friend aliapa kutowatumia consultants wa kitanzania wanaoganga njaa halafu wanataka mshahuri mtu aliyetafuta hela from the scratch to somewhere ambapo kila mtu anawakubali.Atakushauri nini zaidi ya kukupa ma theory kibao ambayo hata wao hawajui kuyatumia.

Nimekuta mjinga mmoja anamshauri mtu afungue akaumti bank na kufuata sheria ili a qualify kwa mkopo.Huyu jama ambaye hajaenda shule alikuwa na dreamz za kuifanya bank ndio equalify kumpa mkopo, na kwanini akapoteze muda kupanga foloeni ktk bank kwa transaction zinazoweza pitia ktk M-Pesa?Wakati huyu msomi anapiga blah balah kuwa ni Impossible,jama akampa clue kuwa maafisa mauzo wa bank wanashinda ktk office yake kila siku,bado mshauri hakuanza ona kuwa demand imeshift kutoka kwa mfanyabiashara na kwenda kwa bank.Hivyo mfanya biashara sasa anweza weka conditions zake kwa bank.Jamaa yangu akampatia jamaa bia na pombe.na hela kidogo huku akimwambia kamkubali san aelimu yake.Ikawa misho.Hivyo hivyo CDM inaendelea waonyesha critics kwa vitendo ,wakati wao wakiwa busy kutoa plan kichaa nyingi, na kutafuta conspirancy theories nyingi za kuelezea mafanikio ya CDM kama by chance na sijui mapenzi ya watu, mara sijui mapungufu ya CCM.
 
Sawan mkuu Mwanakijiji. Nazikubali fikra zako. Natumaini sasa kwa ujumbe huu na hizo link kadhaa, tumekuelewa zaidi. Nachoomba utuwekee link ya maoni yako ya mgawanyo wa jiji la dar katika mikoa ya kipolisi.
 
Duu! kweli JF ni raha tupu....ahsante sana Edson kwa kutuletea za chini ya kapeti about MMKJJ
 
Back
Top Bottom