WOWOWO
JF-Expert Member
- Aug 3, 2011
- 599
- 457
Wakuu naomba nisamehewe maana najua si sahihi hata kidogo kujadili watu lakini kwa hili nafsi imezidiwa nguvu, nimeona nifanye hivyo.
Kwanza nianze kukiri mapema kabisa Mzee Mwanakijiji japo simfahamu na hatujawahi kuonana ni mentor wangu na kwa kiasi kikubwa amenijenga katika ujenzi wa hoja na upanuzi wa uelewa wa masuala mbalimbali.
Nimekuwa nikifuatilia kila anachoandika humu JF na kwenye machapisho mbalimbali kuanzia magazeti ya Tanzania Daima, Mwanahalisi (Mungu asaidie lirudi maana nimeugua kwa kulikosa),Majarida ya Cheche, Kitabu cha Majeruhi wa Mapenzi na mara kadhaa nimeelezwa majina kama Lula Ndali Mwananzela yanayotumiwa kwenye magazeti ya Raia Mwema na Mwananchi ni yeye.Sina hakika katika hili la mwisho.
Hakika nimekuwa sikosi maandiko yake.Nimekuwa nikihangaika sana kuhakikisha sipitwi na anachoandika. Kila Jumatano nimekuwa nikinunua magazeti ya Tanz. Daima, Raia Mwema na Mwanahalisi na Jumapili nimekuwa siachi kununua gazeti la Mwananchi kwa sababu yake. Ninapokosa makala zake nimekuwa naumia sana.
Lakini katika upekuzi wangu humu Jamii Forums (Enzi hizo Jambo Forums) nimekumbana naThread iliyonishtua ya Mh. Freeman Aikael Mbowe (Mwenyekiti wa CDM) aliyoipost JF mwaka 2006 yenye kichwa cha 'The OnlyThing We Have To Fear……' mara baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa mkuu mwaka 2005.
Uzi huo wa Mh. Mbowe ambao ni wa kwanza na wa mwisho kwake unaweza kuusoma hapa https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/947-the-only-thing-we-have-to-fear.html
Kilichonishtua si Mbowe kupost thread JF, la hasha, ni msimamo aliokua nao Mzee Mwanakijiji dhidi ya upinzani na mageuzi kwa ujumla nchini. Katika kuchangia thread hii pamoja na akina Kitila Mkumbo, Mkandara, Nyani Ngabu, John Mnyika kujitahidi kumuelewesha MMM bado alikuwa na msimamo hasi dhidi ya upinzani na ama kwa hakika alikuwa ‘Real pro-CCM' na naweza kudiriki kusema aliuona upinzani kama uliopoteza dira na usio na uwezo wa kuleta mabadiliko na kuaminiwa na wananchi.Niko tayari kukosolewa.
Moja ya nukuu ya MM kwenye mjadala huo ni hii "Lazima tuwaone viongozi hawa wakiongoza ndipo tutavutiwa navyama vyao!! Nilikuwa nakiheshimu Chadema sana, lakini baada ya kampeni zamwaka jana na hadi leo wamenikatisha tamaa!! Sasa naanza kukiangalia kwa karibuCUF huku moyo wangu bado uko CCM!!"
Kwenye thread hiyo, MM aliitetea CCM dhidi ya maovu yote iliyokuwa ikitupiwa na wapinzani. MM alisimama kidete kupinga madai ya CCM kununua shahada za kupigia kura, kuwanunua viongozi wa upinzani, matumizi makubwa ya nguvu za dola dhidi ya upinzani nk. nk.
Hakika ukitazama michango ya MMM kwenye thread hiyo ya F. Mbowe hasa jinsi alivyokuwa supporter mzuri wa CCM na kuuponda upinzani na harakati za mageuzi huwezi kuamini nini hasa kilitokea Mzee Mwanakijiji akabadilika na kuwa huyu ninayemsoma leo.I mean kuwa against na CCM na doings zake zote.
Wazo moja lililonijia ni labda pengine MM alikuwa anapata maslahi fulani manono kutoka CCM na ndiyo yaliyokuwa yanamuweka kwenye huo msimamo hasi dhidi yamabadiliko na sasa maslahi hayo hayapati tena, yamezibwa na ndiyo sababau ya yeye kubadilika. Vinginevyo nini hasa kilimbadili Mzee Mwanakijiji?