Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,025
- 132,770
Du!, inaelekea japo hatukuwa intake moja, ila inaonyesha wakati nikiwa UD pia Mzee Mwakijiji alikuwepo!. Humu jf wengi wetu tunakabiliwa na tatizo kubwa sana la kutoukubali ukweli kewa kutumia "negation" na baadhi ya wasema ukweli kuwazushia!. Kuna watu wanaamini kila anaikosoa CDM ni CCM!. Au kwa vile mtu kama mimi japo nasisitiza sina chama, lakini napigia debe sana EL au Membe ndie ateuliwe mgombea wa CCM, basi mimi ni CCM!, na kwa vile mimi ni CCM, hivyo support yangu kuunga mkono matumizi ya demokrasia ndani ya CDM kwa kumuunga mkono ZZK kunazishiwa "bad faith"!.Kilichoandikwa hapo juu kina ukweli fulani lakini si ukweli wote. Kwa hiyo hili ni kasa mnalishwa na Edson halafu nashangaa kuona MM hajalipinga.
Mimi nimesoma darasa moja na MM hapa Tanzania. Na alikuwa mwanamapinduzi wa dhati nilipokuwa naye. Hakusoma BA pale UDSM, bali alisoma kozi nyingine( kwa sasa naihifadhi). MM amesoma Masters ya Uchumi USA. Lakini sasa MM amebadilika. Tulipokuwa chuo kaka zetu waliotupika kuwa wazalendo ni kina Kitila Mkumbo ambaye wakati huo alikuwa Rais wa DARUSO. Jakaya Kikwete ni sisi tumechangia kwa kiasi kikubwa kumweka madarakani na ndio maana tunatamani tumtoe hata leo kwa jinsi alivyotusaliti. RIDHIWANI ANALIJUA VYEMA HILI. NCHIMBI NDIYO KINARA HASWA(MBA UDSM!!!!)
MMM alikuwa ni kiongozi wa DARUSO Kwenye wizara nyeti ( Naihifadhi kwa sasa). MM alifukuzwa pamoja nami kwenye mgomo wa mwaka ambao kulikuwa na uchaguzi wa Rais, Hivyo MM hakumaliza masomo yake TZ. Alipoenda marekani kwa jitihada za kuuza ng'ombe wa mama yake kijijini ndipo alipobadilisha masomo.
MM hakupitia Mbweni hivyo si mwajiriwa wa TISS hata kidogo! Huwezi kuwa Ofisa wa jeshi kwa kupitia kwa amiri jeshi mkuu bila kupita Monduli kwa JWTZ au Mbweni kwa kupitia TISS. Japo sikatai kuwa anaweza kutumiwa na TISS kama anavyotumiwa mgombea Urais wetu Zitto Zuberi Kabwe.( Sijui kama anakumbuka kiapo chetu pale nyumbani kwa mama yake Magomeni mwembechai- kwa sababu tume ya madini ya Kikwete ilimvuruga kabisa)
Kwa kifupi niseme tu hapa mnalishwa kasa na Edson, na jambo la pili ni kuwa kina MMM wana msemo wao huko wanakotumiwa kuwa 'every head has got a price tag on it'.
Ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania, utaweza kupatikana pale tuu tutakapo kubali kwa dhati kusimama kwenye ukweli, na ni ukweli ndio utatuset free toka madhila tuliyopo!. Kila siku napiga kelele humu. kuendelea kuiimbia Chadema nyimbo za sifa na mapambio!, hakuisaidii CDM. Mtakuja kukuta sisi tunaoipitisha kwenye tanuru la moto, ndio tunaisaidia zaidi kuliko hawa wanaiimbia mapambio kila kukicha!.
Tukubali, tukatae, Chadema bado haijajipanga kisawa sawa, na ikiendelea hivi hivi ilivyo, 2015 ni CCM tena!.
Nawaombeni tuukubali ukweli huu na kuufanyia kazi na sio kuukanusha tuu kwa "negation" na kuwazushia wasema ukweli kuwa ni "magamba", "wasaliti", "wametumwa", "wanafiki", "hawaitakii mema CDM" , etc, etc!.
P.