Prof. Tibaijuka Kikaangoni, CCM Waitana

Prof. Tibaijuka Kikaangoni, CCM Waitana

Ila hawa jamaa kwa uongo isee ni bilaa lkn mdee jana alijiona harudii tena kuvuta msokoto wake ndio aingie bungeni.
 
nilikuwa naangalia bunge wizara yake I was disappointed hasa yale aliyoyafumua Mdee balaa tupu

kwenye upendeleo huyu mama ni balaa kuna ndugu yake mmoja alimpachika UN Habitat

Kenya wakati bado hajaja huku wakati hata sifa na vigezo hana acha hiyo TAWLAT sasa

Wahaaya siunawajua!
 
Pale kigamboni ni karibu na ofisi yake ndio maana.Huwa akiwa ofisini yeye nikuchungulia dirishani tuu na kupatolea macho kigamboni.
 
Katika hali ya kushangaza na ambalo ni jambo la kawaida kwa wanaccm, waziri wa ardhi prof Tibaijuka ameingia katika orodha ya mafisadi wanaoiteketeza nchi hii. Akizungumza kwa uchungu mbunge wa kawe mh. Mdee amesema katika kila mgogoro wa ardhi unaotokea hapa nchini, mkono wa prof Tibaijuka upo kwa matakwa yake binafsi.
Baadhi ya migogoro hiyo ni;
1. Bukoba mjini ambako prof Tibaijuka anadaiwa kumiliki ekari 100
2. Chasimba eneo la wazo hill, kuna nyongeza ya watu 404 katika tathmini, kitu kinachopelekea na kuhisiwa kuwa ni kwa ajili ya Tibaijuka.
3. Kigamboni ambako pia mkono wake haujapungua kwa kujimilikisha maelfu ya ekari.

Kitu alichonishangaza zaidi ni kuacha kujibu hoja na kuanza kuzungumzia elimu yake, alikofanya kazi, kitu kilichopelekea nianze kuuamini utani wa watu wasemao mhaya anapopewa nafasi ya kuzungumza haachi kujisifu. Spika wa bunge alifanya kila jitihada kumkumbusha ajielekeze kwenye kujibu hoja lakini aligonga mwamba mpaka muda ulipoisha.
Duuuuuh! Kweli ukweli unauma, prof Tibaijuka ni Fisadi.
 
CCM hakuna msafi.
Bahati mbaya saana tumekosa wapinzani makini.
 
ama kwa hakika hata Yesu angekuwa CCM lazima angekwiba. hicho ni chama cha mashetani, wezi, malaya,majangili wa wanyama na wauaji wakubwa wa raia.

Tafadhali sana mkuu, acha kabisa kumfananisha Yesu na uchafu kama huu.
Pls,apologize to Him.
 
Fuatilia hapa chini, kisha useme maneno.....

Early life and education


Born in Tanzania, Tibaijuka studied agricultural economics at the Swedish University of Agricultural Sciences in Uppsala and is fluent in English, Swahili, Swedish and French. She is the widow of the former Tanzanian ambassador Wilson Tibaijuka, who died in 2000. She is the second highest ranking African woman in the UN after Dr Asha-Rose Migiro, the deputy UN secretary general (who is also a Tanzanian) In October 2010 she became MP for CCM for Muleba District, Kagera Region, in the national election.
Academic career

From 1993 to 1998 Tibaijuka was associate professor of erconomics at the University of Dar es Salaam. During this period she was also a member of the Tanzanian government delegation to several United Nations summits including the United Nations Conference on Human Settlements (Istanbul, 1996); the World Food Summit (Rome 1996); the Fourth World Conference on Women (Beijing 1995) and the World Summit for Social Development (Copenhagen, 1995). At the World Food Summit in Rome, she was elected coordinator for Eastern Africa in the Network for Food Security, Trade and Sustainable Development (COASAD). zMrs. Tibaijuka has also been a board member of UNESCO's International Scientific Advisory Board since November 1997. She is a foreign member of the Royal Swedish Academy of Agriculture and Forestry.[SUP][2][/SUP]

Anna Tibaijuka ni Agricultural Economist tu, agrarian economy!!! Anatamba sana, Equity Financing & International Markets!! Kweli? Hapana!!
 
Prof. amejibu mapigo ya Mdee; akimtuhumu kuwa amesema uongo na kuwashauri wananchi wa jimbo la kawe wasimchague tena Mdee akidai "itakula kwao".

Amedai Mdee amefikia hatua ya kuiba barua ya kiofisi ambayo alimwandikia waziri mkuu na kuiweka katika hotuba yake.
 
Kuhusu kigamboni premier alihitimisha,,mchakato unaanza upya ukishirisha wadau, kwahiyo kujenga, kuuza,kununua ruksa!
 
Tafadhali sana mkuu, acha kabisa kumfananisha Yesu na uchafu kama huu.
Pls,apologize to Him.
narudia kwa namna hii, hata mitume wa dini zote leo wangekuwepo na wangekuwa CCM wangekuwa wezi, namaanisha kabisa....
 
Report yenyewe ame copy barua ya professor kwenda kwa waziri mkuu halafu mnamsifia, halafu sauti inazidi kukauka tu mwambieni aache kunywa gongo na kutembea na viroba kwenye hand bag yake.

Haijalishi,cha msingi ni kua tibaijuka ni mwizi wa ardhi halali ya wananchi wa chasimba na kigamboni usikute na jk nae kapora maekari maelfu kwa wananchi wa msoga....nzi wanao fanana hutua kwenye kidonda kimoja.
 
Uprofesa ni chaka la maovu yote uyajuayo na hakuna wa kukuuliza.
 
Ukawa mnaangaika nyie kisauti Jana kamwaga ushuzi wake bungeni pale ila prof. Alimpatia fresh yake
/HIVI YULE MAMA TIBAIJUKA NI PROFESA?mbona baada ya kujibu hoja kisomi kamshambulia MDEE?kazi ipo, na sura yake komavu kapata shiiida sana mama wa watu.halafu eti ni president material wa 2015.
 
Hao ndio maprofesa na madaktari walio ndani ya sisiemu.Wezi watupu msomi wa kweli,aliyeelimika katu hawezi kuwa shabiki au mwanachama wa sisiemu kwani huko suala la kufikiri haliko kabisa bali ni mazingaombwe tu yaliyojaa.
 
Mtoa mada labda nikwambie hivi..kuna utaalamu wa aina moja tu ambao ufanisi wake unakuwaga ni dhahiri mahala pote ambao ni SAYANSi. Hapa namaanisha sayansi ngumu sio ile laini so called social sciences..Ukisikia daktari professor ujue huyo amefanya tafiti dhahiri kwenye mwili wa viumbe akagundua kitu na ameponya watu katika shida au mphamasia kagundua dawa kaelezea madhara yake na inatumika kutibu hao ni kweli maprofessor na wengine katika sayansi ya aina hii kama wale waliomfundisha panya kugundua mambukizo ya TB na kufukua mabomu ya ardhini nk.

Lakini Professor wa uchumi ama sheria sijui wakati uchumi wetu haukui mikataba mibovu yapitishwa na ufisadi unakuwa na kuenea mbaka kwa watoto wadogo alafu mnawaita wataalamu wamesoma Sweden, Norway, USA nk..hao ni wataalamu wa maandishi na maandiko. Wanaandika kupata hadhi ya kitaalam lakini buree kabisa hawawezi kugeuza elimu yao kuwa faida. Wengine huko huko Bungeni wanayakana machapisho yao kisa siasa za mlengo fulani. Wasomi wetu PhD holders etal..wamekuwa watumwa wa mfumo huu wa hovyo wa nchi yetu. Si watu wa kuwakimbilia kabisaa hawana msaaada.

Hivyo basi mtoa mada..hakuna usomi ninaouona katika wasomi wetu kwani wanashindwa kutumia machapisho yao ya kisomi kuibadili nchi yetu katika maeneo ya usomi wao. Pathetic...........
 
Back
Top Bottom