Prof. Tibaijuka Kikaangoni, CCM Waitana

Prof. Tibaijuka Kikaangoni, CCM Waitana

Mhhhh!!!!!!!!!! Sijawahi fungua huku nikakukosa. Kila post iwe udaku wewe upo tu. CCM wamekupa tenda nn mamaa ili na mm nijiunge angalau naweza badilisha upepo wa maisha.
Kama vipi nawe mfuate kila anapokwenda kama CRDB inavyowafuata wateja wake (ulipo tupo) kwa maana naona una wivu wa kike.
 
Kama vipi nawe mfuate kila anapokwenda kama CRDB inavyowafuata wateja wake (ulipo tupo) kwa maana naona una wivu wa kike.
We vipi? mbona unaingia bila hodi? Ila ndo mdudu alivyo. Umejiunga juzi hata sheria za JF hujazijua unaanza kuparamia watu ovyo.
 
Huyu Mdee alikuwa anapiga kelele tu. Chukulia hoja ya Chasimba,pale Mahakama ya Rufaa ilishahukumu kuwa wananchi wahame pale, Ardhi yote ni mali ya Kiwanda.Alikuwa ni Mama Tibaijuka aliyesimama kidete kuwa wananchi hawawezi kuondoka bila fidia.Zoezi lenyewe ndo lilikuwa linaendelea na linaonekana kufanikiwa. Ajabu ni Mbunge huyohuyo anaanzisha chokochoko kupinga.Kama sio kelele maana yake nini?
 
Nadhani naweza kukubaliana na hoja ya watu kulipwa ili wawepo hapa masaa 24 na kupinga kila hoja yenye mwelekeo wa kukosoa utawala wetu. Huu ni umamluki na ukahaba wa aina yake. Haiwezekani kwa Mtanzania mwenye akili timamu asione jambo hata moja linalohitaji kurekebishwa ndani nchi hii. Kwani nchi inaongozwa na malaika? Mwalimu Nyerere mwenyewe pamoja na uongozi wake uliotukuka alifanya makosa na mara nyingi alikuwa wa kwanza kukiri makosa hayo. Leo hii eti kuna watu wanashinda hapa kupinga kila kinachoonekana kinakosoa uongozi! Umamluki huu hauisaidii nchi hii; badala yake unahatarisha mustakabali wake. Hii ni kwa sababu, kwa tafsiri ya kawaida mamluki hao siyo wananchi wa kawaida bali ni wababaishaji na wezi wa rasilmali za nchi.
 
Back
Top Bottom