Prof. Maghembe amekalia kuti kavu

Prof. Maghembe amekalia kuti kavu

Ni aibu sana kwa wote waliotaka kuikwamisha operesheni ya kuwadaka maharamia wa meno ya tembo....
Nilipokuwa nasikia Rais akisema kila siku aombewe mwanzoni sikumuelewa. Ila sasa namuelewa. Hali ilikuwa mbaya sana huko serikalini. Mijitu bado ipo kwenye hang over za kupiga deal. Sasa kweli hadi Rais aingilie si hatari sana hii. Waziri na wasaidizi wake walikuwa wapi au wamekuwa compromised? Wakuu wa vyombo vya usalama wapo wapi?
 
Tukijua mmiliki wa hao ng'ombe 400 Ni nani, tutapata jibu kuhusu hatua ya Maghembe
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Binafsi nilikuwa ni miongoni mwa watu ambao tulionesha wasiwasi wetu mara tu baada ya Prof Maghembe kuteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Wasiwasi wangu haukutokana na location ambayo Prof Maghembe anatoka bali ni kutokana na ugumu wa Wizara hiyo na uwezo wa Maghembe kukabiliana na changamoto za Wizara.

Hakika nilikuwa sahihi kumjudge negatively. Huko Kagera, Mhifadhi Mkuu wa Pori amefukuzwa kazi kutokana na kuwaondoa watu waliovamia pori hilo kwa kukata miti na kuingiza mifugo mingi. Mhifadhi huyo amefukuzwa kutokana na amri ya Mamlaka ya Juu ya Wizara.

Kama hiyo haitoshi, kuna operesheni inayoendelea ya kuwakamata vibompa wa Meno ya Tembo. Operesheni hiyo imeanza juzi. Hata hivyo, mamlaka ya Juu ya Wizara ya Maliasili na Utalii ikaingilia kati ili wanaohusika na biashara hiyo akiwemo jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Mpemba asikamatwe. Bahati nzuri Mheshimiwa Rais aliinyaka hiyo hewani na akasimama yeye mwenyewe kuongoza Operesheni hiyo. Hivi tunavyozungumza hali ni mbaya sana kwa hao jamaa ambao walidhani kuwa kwa nguvu ya pesa waliyonayo hawawezi kukamatwa.

Kwa mifano hii michache, sioni wapi ataponea Prof Maghembe. Jipu tayari limeiva na litatumbuliwa soon.
Nasikia walimpigia Diwani aue "muvu",mkuu kainyaka akataka kuwasha vx mwenyewe,wazee wakamwambia mzee lala kutakucha tu
 
Nasikia walimpigia Diwani aue "muvu",mkuu kainyaka akataka kuwasha vx mwenyewe,wazee wakamwambia mzee lala kutakucha tu
Duh!Kweli Mzee hana simile na wanaomwangusha
1477803373894.jpg
 
Kuna Msomali mmoja haguswi ila yeye ndiye kinara wa meno ya Tembo na ujangili mwingi umefanyika kupitia yeye
kibaya zaidi tulivyomuuliza abuu kwanin unamaliza ndovu zetu kajibu kwani mwawakatia majan
 
Sumaye anaingiaje hapa futeni hizo hati zake kwani mimi zinanihusu nini? Magufuri anaogelea kwenye tope kama anataka kuishinda hii vita aruhusu maoni ya katiba ya mzee Warioba ipitishwe bila hivyo kila siku atakuwa mtumbua majipu mwishowe aambukizwe hayo majipu
We upo dunia gani? Katiba ya warioba ilishasahaulika,tunasubiri katiba ya binge la katiba tuipigie kura,una haki ya kuikataa ili tuendelee na katiba hii
 
Bashe asingekuwa Team Lowassa angefaa sana kwa wizara hii!
 
Waziri huyu sijui end result yake - USHIROMBO MASHINE zinachana shehena ya magogo yaliyozuiwa ndani ya mji. Kusema kweli watendaji wake ndo wapiga deal
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Binafsi nilikuwa ni miongoni mwa watu ambao tulionesha wasiwasi wetu mara tu baada ya Prof Maghembe kuteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Wasiwasi wangu haukutokana na location ambayo Prof Maghembe anatoka bali ni kutokana na ugumu wa Wizara hiyo na uwezo wa Maghembe kukabiliana na changamoto za Wizara.

Hakika nilikuwa sahihi kumjudge negatively. Huko Kagera, Mhifadhi Mkuu wa Pori amefukuzwa kazi kutokana na kuwaondoa watu waliovamia pori hilo kwa kukata miti na kuingiza mifugo mingi. Mhifadhi huyo amefukuzwa kutokana na amri ya Mamlaka ya Juu ya Wizara.

Kama hiyo haitoshi, kuna operesheni inayoendelea ya kuwakamata vibompa wa Meno ya Tembo. Operesheni hiyo imeanza juzi. Hata hivyo, mamlaka ya Juu ya Wizara ya Maliasili na Utalii ikaingilia kati ili wanaohusika na biashara hiyo akiwemo jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Mpemba asikamatwe. Bahati nzuri Mheshimiwa Rais aliinyaka hiyo hewani na akasimama yeye mwenyewe kuongoza Operesheni hiyo. Hivi tunavyozungumza hali ni mbaya sana kwa hao jamaa ambao walidhani kuwa kwa nguvu ya pesa waliyonayo hawawezi kukamatwa.

Kwa mifano hii michache, sioni wapi ataponea Prof Maghembe. Jipu tayari limeiva na litatumbuliwa soon.
Ndio maana tumeanza na DCI
 
Tatizo ni chama cha ccm wala sio Maghembe, Magufuri atapata shida sana kwenye haya mapambano atajikuta anapambana na chama chake
Ni kweli kabisa bt aliapa kukisafisha nafikiri anaelekea huko, Kikubwa tumuombee huyu mkuu wa kaya maana kazi anayo mafisadi, majangili na wahujumu uchumu wamo ndani ya Chana chake.
 
Hizo chuki za kikabila peleka kwenu. Ng'ombe zilikuwa detained kwa kosa gani..?
Huna haja ya kuhamaki. Kutaja Watutsi ni sawa tu na kutaja jamii zingine za kifugaji kama Wamaasai au Wasukuma. kua na amani mkuu. Umeuliza ng'ombe wana kosa gani nadhani una maana hadi kukamatwa. Jibu: ng'ombe hawajaingia kwenye hifadhi wenyewe ila wamepelekwa na wachungaji. Wachungaji ndio wenye makosa. Tofauti na raia mwenye uhuru kwenda popote nchini ngombe sio raia.
 
  • Thanks
Reactions: WFM
Back
Top Bottom