A
Anonymous
Guest
Majangili (kutoka Tanzania na Kenya) wamemuua faru ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti.
Faru huyo ameuawa wiki moja iliyopita, na nyara zake zimekamatwa Nairobi, Kenya.
Baada ya uchunguzi, imethibitika kuwa faru huyo aliuawa eneo la Moru ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Bado kuna maswali mengi juu ya kuuawa kwa mnyama huyo, hasa ikizingatiwa kuwa ulinzi wa aina hiyo ya wanyamapori umekuwa wa kiwango cha juu mno.
Duru za ndani zinasema siku ya kuuawa kwake, askari walinzi waliondolewa kwa namna ambayo bado inaibua maswali mengi.
Pamoja na Wakenya, kuna Watanzania kadhaa wametiwa mbaroni. Watu hao wanatoka vijiji vya Arash na Oroipil Wilayani Ngorongoro.
Inashangaza kuwa mamlaka za uhifadhi na za nchi zinalifanya tukio hili kuwa siri kubwa, ingawa vyanzo vya taarifa vimedokeza kuwa watuhumiwa walitarajiwa kufikishwa mahakamani kuanzia leo Aprili 8, 2025.
Ujangili umetajwa kuibuka kwa kasi kutokana na mamlaka za uhifadhi kuwa kwenye mkwamo wa fedha kutokana na utaratibu wa OC.
Wizara ya Maliasili na Utalii, viongozi wake wamejielekeza zaidi kwenye utalii na kuweka nguvu ndogo kwenye uhifadhi na ulinzi wa wanyamapori.