Prof. Maghembe amekalia kuti kavu

Prof. Maghembe amekalia kuti kavu

Prof. Maghembe Mbunge wa Wilaya ya Mwanga nilipozaliwa, nikakulia na nitazikwa hapo wilaya ya Mwanga
 
Arudishwe baba aunt Ezekiel aendelee kuongoza Wizara ya maliasili na utalii
 
mmmh kumbe ccm kuna majipu lizaboni???kumbe ccm kuna mafisadi mimi nilijua magufuli ni malaika hakosei kuchagua
Yapo bado, hayaishi hivi karibuni. Ila sasa yakishatumbuliwa tu mnaanza kuyatetea na kuyakaribisha kwenu mtaa wa ufipa.
Hapa ndipo napopata wasiwasi na lengo la chama hiki cha mtaa huo.
 
Kwa kweli Maghembe ni tatizo sana hata jimboni kwake naona kuna matatizo sana tangu alipata Ubunge hakuna la maana alilofanya.
Uharibifu mazingira ni mkubwa sana kila sehemu.
Miradi ya maji jimboni kwake haionekani. Yote imekufa na mabomba hayato maji. Na kwa woga wa wananchi hakuna anaye hoji .

Maeneo ya Kagera hasa wilaya ya Biharamulo na kwingineko kuna uharibifu mkubwa sana wa Mazingira unaosababishwa na wakulima na wayfugaji wanaovamia maeneo ya hifadhi. Hata hivyo hatukuona waziri akichukua.
Miaka 20 ijayo wilaya ya Biharamulo itakua jangwa kama tutaendelea kuwa na waziri Maghembe kwenye wizara ya maliasili.
Ni vizuri Mh. Rais akambadilishia wizara. Apewe wizara nyepesi au apumzike kabisa.
Lakini si yeye tu bali mawaziri wengi hawana kasi ya kutosha kuendana na Rais aliyepo. Hawana ubunifu. Bila ubunifu nchi haitasonga mbele zaidi ya kufukuzana na kutiana hofu tu.
 
Kwa hilo la Biharamulo nakuunga mkono naifahamu misitu ya Biharamulo enzi hizo haijaharibiwa, ukiiona sasa.....
Binadamu anagombana ile mbaya na misitu badala ya kuwa rafiki wa misitu.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Binafsi nilikuwa ni miongoni mwa watu ambao tulionesha wasiwasi wetu mara tu baada ya Prof Maghembe kuteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Wasiwasi wangu haukutokana na location ambayo Prof Maghembe anatoka bali ni kutokana na ugumu wa Wizara hiyo na uwezo wa Maghembe kukabiliana na changamoto za Wizara.

Hakika nilikuwa sahihi kumjudge negatively. Huko Kagera, Mhifadhi Mkuu wa Pori amefukuzwa kazi kutokana na kuwaondoa watu waliovamia pori hilo kwa kukata miti na kuingiza mifugo mingi. Mhifadhi huyo amefukuzwa kutokana na amri ya Mamlaka ya Juu ya Wizara.

Kama hiyo haitoshi, kuna operesheni inayoendelea ya kuwakamata vibompa wa Meno ya Tembo. Operesheni hiyo imeanza juzi. Hata hivyo, mamlaka ya Juu ya Wizara ya Maliasili na Utalii ikaingilia kati ili wanaohusika na biashara hiyo akiwemo jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Mpemba asikamatwe. Bahati nzuri Mheshimiwa Rais aliinyaka hiyo hewani na akasimama yeye mwenyewe kuongoza Operesheni hiyo. Hivi tunavyozungumza hali ni mbaya sana kwa hao jamaa ambao walidhani kuwa kwa nguvu ya pesa waliyonayo hawawezi kukamatwa.

Kwa mifano hii michache, sioni wapi ataponea Prof Maghembe. Jipu tayari limeiva na litatumbuliwa soon.
Wewe umekalia kigogo
 
Back
Top Bottom