Prof. Maghembe amekalia kuti kavu

Prof. Maghembe amekalia kuti kavu

Haina haja na sidhani kama atamtumbua... wakati anamteua alijua kabisa uwezo wake... na sio Maghembe tu... wapo wengi walioteuliwa kwa kigezo cha ukada...

Na usishangae akitolewa huyo akawekwa Lipumba..
Mapambano dhidi ya Majangili inahitaji kuongozwa na watu shupavu. Si legelege kama Prof Maghembe
 
Mapambano dhidi ya Majangili inahitaji kuongozwa na watu shupavu. Si legelege kama Prof Maghembe
Kilimo, mifugo na uvuvi ndio hatujui kabisa wapi tunatoka wapi tunakwenda...

Afya huyu anasema hivi huyu vile...

Miundombinu tangu JPM atoke imebaki nyang'anyang'a...

Unajua kwa utendaji wa Magufuli alipokuwa waziri nilitarajia kabisa anawajua watu wapiga kazi kama yeye... lakini katuwekea watu ambao hawasomeki!!!
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Binafsi nilikuwa ni miongoni mwa watu ambao tulionesha wasiwasi wetu mara tu baada ya Prof Maghembe kuteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Wasiwasi wangu haukutokana na location ambayo Prof Maghembe anatoka bali ni kutokana na ugumu wa Wizara hiyo na uwezo wa Maghembe kukabiliana na changamoto za Wizara.

Hakika nilikuwa sahihi kumjudge negatively. Huko Kagera, Mhifadhi Mkuu wa Pori amefukuzwa kazi kutokana na kuwaondoa watu waliovamia pori hilo kwa kukata miti na kuingiza mifugo mingi. Mhifadhi huyo amefukuzwa kutokana na amri ya Mamlaka ya Juu ya Wizara.

Kama hiyo haitoshi, kuna operesheni inayoendelea ya kuwakamata vibompa wa Meno ya Tembo. Operesheni hiyo imeanza juzi. Hata hivyo, mamlaka ya Juu ya Wizara ya Maliasili na Utalii ikaingilia kati ili wanaohusika na biashara hiyo akiwemo jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Mpemba asikamatwe. Bahati nzuri Mheshimiwa Rais aliinyaka hiyo hewani na akasimama yeye mwenyewe kuongoza Operesheni hiyo. Hivi tunavyozungumza hali ni mbaya sana kwa hao jamaa ambao walidhani kuwa kwa nguvu ya pesa waliyonayo hawawezi kukamatwa.

Kwa mifano hii michache, sioni wapi ataponea Prof Maghembe. Jipu tayari limeiva na litatumbuliwa soon.
Hivi wizara ya mifugo ipo? Naona Kama imekufa hivi.
 
binafsi sina tatizo na majariwa nlichomaanisha kma asingekuwepo majariwa angekaa huyu jamaa pia. ila huwez mlinganisha na pinda kabisa. lukuvi malezi yake ccm ndo si mazuri lakini kama asingekuwa amelelewa ccm ni mtu mzuri tu. ukikulia na kulelewa na ccm una pata matatizo katika ufikiri wako.unafikiri upande upande.


Kwa hiyo unaona Majaliwa hajiamini?
 
Nisieleweke vibaya, kwa timu iliyopo bungeni sasa hivi... Hakuna wa kuongoza hii wizara kiuadilifu. Labda akasajili kutoka nje ya bunge na achukue mtu mzoefu. Kama wasira, chiligati, etc. hawa wazee inasemekana ukiwahonga wanalia.
 
<<< ANAWACHOCHEA majangiri wazidi kuuwa TEMBO wetu MH. RAIS amemstukia MAPEMAAAAAAA >>> ila ANAOGOPA Atalivunja BARAZA la MAWAZIRI tena ....>>
 
Back
Top Bottom