TAMKO LANGU KWA UMMA JUU YA
UZUSHI UNAOENEZWA DHIDI
YANGU.PROF JUMA KAPUYA
Ndugu wanahabari, Baada ya
kumshukuru na kumtukuza
mwenyezi Mungu mwingi wa
rehema.
Natanguliza salamu zangu za pole
kwa familia ya marehemu
mwanazuoni na mwanaharakati
mwenzangu Dkt Sengondo Mvungi
aliyetangulia mbele ya Haki siku
chache zilizopita huko Afrika ya
kusini.
Ndugu zangu wanahabari,
Wengi mnanifahamu na kuifahamu
vema historia yangu katika utendaji
kazi na utumishi wa umma wa
Watanzania. Nimekuwa
nikiitumikia nchi yangu kwa kipindi
kirefu katika Nyanja na sekta mbali
mbali kuanzia Darasani mpaka
kwenye siasa.
Kwa msingi huo, mimi Profesa
Juma Kapuya, siku zote ninajikuta
mwenye wajibu endelevu wa
kuendelea kulitumikia Taifa langu
kila siku mpaka kufikia mwisho wa Nguvu zangu.
Ndugu wanahabari,
Hivi karibuni nikiwa huku jimboni
kuendelea na shuhuli za utekelezaji
wa ilani ya chama cha mapinduzi
kumezuka Tuhuma kadhaa
zilizoelekezwa dhidi yamgu
zikiasisiwa na wanasiasa wenzangu
wa ndani na nje ya chama changu
ili kudhoofisha juhudi na utendaji
wangu wa kila siku.
Tuhuma hizo zisizokuwa na kichwa
wala miguu na pia kutokuwa na
ukweli wowote, wamekuwa
wakizitoa kwa kumtumia msichana
anayedai amefanyiwa vitendo
visivyofaa na mimi. Mimi
simfahamu na sijui hizi shutuma
zinatokea wapi.
Ndugu wanahabari,
Kwa tamko hili ninapenda
kuwaambia kuwa nimefedheheshwa
sana na uwezo mdogo wa kisiasa
unaofanywa na hawa watu kwa
kuwa dhamira yao haitatimia.
Napenda niwakumbushe ndugu
zangu kwamba tunaelekea kwenye
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na
wapinzani wangu wameanza
kunichafua ili nionekane sifai.
Ninapenda kuwaambia watanzania
na wananchi wa jimbo langu kuwa
wanatakiwa wazipuuze taarifa hizi
kwa kuwa hazina ukweli wowote
na kwamba ni za kutungwa zenye
lengo la kunidharirisha na
kuniondolea heshima yangu
niliyojijengea kwenye jamii kwa
kipindi kirefu sasa.
Waswahili wanasema dawa ya
mjinga ni kumpuuza
Na hili linajidhihirisha zaidi kwa
habari hii kuandikwa na chombo
kimoja tu cha habari
kinachotumiwa na chama kimoja
cha siasa na baadhi ya wanasiasa
wa chama changu wasiokitakia heri
chama chetu, naomba kuwashukuru
na kuwapongeza vyombo vingine
vya habari kwa umakini wenu wa
kuwa na nauelewa wa kutoandika
kitu bila kukifanyia uchunguzi na
kubaini ukweli ulivyo.
Chombo hiki cha habari kiliwahi
kuripoti mwaka jana kuwa kuna
mitambo imeingizwa nchini
inayoweza kuandika ujumbe na
kisha kuufanya uonekane
umetoka kwenye namba Fulani,
kwa kipindi kile sikuwaelewa,
lakini sasa ninawaelewa na
nimewaona kuwa wako sahihi na
wao ndio waliouingiza mtambo
huu na sasa wameamua
kuutumia dhidi yangu kwa
kutengeneza meseji na
kuzihusianisha na mimi.
Ninaamini ukweli utawaumbua
muda si mrefu.
Ndugu wanahabari, Nimeijenga
heshima yangu na familia yangu
kwa jamii yangu kwa kipindi kirefu
mno, kwa hivyo siwezi kuruhusu
heshima niliyoijenga kwa miongo
kadhaa karibiwa na kupotezwa na
watu wachache tena kwa muda
mfupi namna hii.
Hivyop basi nimechukua hatua za
kisheria kuhakikisha heshima
yangu inaendelea kulindwa na utu
wangu unaheshimiwa.
Nimemwagiza mwanasheria wangu
afungue kesi na tayari
amewashitaki watu wote
wanaohusika kwenye mpango huu
na tayari wameshapokea taarifa ya
kuitwa mahakamani.
Nitaendelea kuwachukulia hatua
kali za kisheria watu wote
watakaoendelea kutaka kujipatia
umaarufu ama wa kisiasa au
wowote ule kwa kutumia jina
langu.
Hayo yote ni kwa kuzingatia ukweli
kwamba nchi yetu inaendeshwa
kwa misingi ya kisheria na kufuata
na kuheshimu haki na wajibu
wakila mmoja wetu.
Kwenye hilo ninawaambia janja
yao nimeigundua, na
hawatafanikiwa
Ninatoa Rai kwa yeyote mwenye
kuona hilo jambo lina ukweli
alipeleke kwenye vyombo husika ili
lishuhulikiwe kwa mujibu wa
sheria na sio kutumia vyombo vya
habari kuchafuana.
Mwisho ninasisitiza kuwa
nitaendelea kuilinda na kuitetea
heshima yangu niliyojijengea kwa
jamii kwa muda mrefu sasa na
sitaruhusukuiona ikiharibiwa na
wajanja wachache kwa maslahi yao
binafsi.
Tuendelee kuijenga nchi yetu,
Mungu Ibariki Tanzania
Imetolewa leo tarehe 15.11.2013
nami
Prof. Juma A.Kapuya
Mbunge urambo magharibi
S.L.P 45 Kaliua Tabora
Simu 0784993930