Akizungumza kupitia kwa wakili wake, Yasin Memba, mbunge huyo alitishia kuliburuza gazeti hili mahakamani endapo halitamwomba msamaha ndani ya siku saba. Pamoja na kukataa kwake kumfahamu binti huyo, Kapuya amekiri kumiliki simu namba 0784993930 ambayo imekuwa ikitumiwa kuwasiliana naye ikiwemo kumtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) wa vitisho. Hata hivyo, katika namna ya kushangaza, Kapuya alidai kwamba simu hiyo aliishaigawa miezi sita iliyopita, na hivyo hausiki kwa namna moja ama nyingine na tuhuma alizopewa. Kweli njia ya MUONGO ni FUPI. Wakati wakili wa Prof. Kapuya, Yasini Memba anadai kwamba mobile No. 0784993930 ya Prof Kapuya alishaigawa simu na line yake MIEZI SITA iliyopita. Tamko la Prof Kapuya alilotoa kwa waandishi wa habari Jana 15/11/2013 linaosha kwamba Prof Kapuya bado anatumia namba hiyo. Yaani kesi hii hata akipewa mwanafunzi anayesoma sheria mwaka wa kwanza hawezi hata kutumia zaidi ya saa nzima kabla hajamfunga P