Prof. Janabi: Kitu hatari zaidi ni sukari na wanga. Ataka watu kula wakihisi njaa kwani mwili hauendeshwi na ratiba ya chakula

Mzee baba hapo kwenye red sijakupata.

Ipo hivi,

ukila wanga mwili unautumia kupata nguvu katika mfumo wa glucose, ukisindilia sana mwili unakusaidia kuhifadhi huo wanga/glucose kwenye liver katika mfumo wa glycogen ambayo ndio mafuta sasa kwa namna nyingne,

Pindi mwili ukiishiwa nguvu/mfano umechelewa kula au hujala, ile glycogen inatolewa kwenye liver kwa kutumia hormone ya glucagon kuileta kwenye mfumo wa glucose ambao ndio unatumiwa na mwili kupata nguvu.

Kwa nini mtu anazidi kunenepa? Kwa kula wanga,

Sbb ni kwamba kila siku anakula wanga iliyozidi kiasi kinachohitajika, matokeo yake inaendelea kuhifadhiwa/jaa kama mafuta kwenye mwili...

Kumbuka, tunapozungumzia wanga tunazungumzia Sukari/sugar na ukizungumzia sukari unazungumzia glucose na ukizungumzia glucose unazungumzia Nguvu.

maelezo mazuri.
 
Wabongo kwa ujuaji🫡🫡 .
Kwahiyo mtu mpaka amekuwa profesa ina maana hajui tofauti ya wanga na sukari.
We nawe rubish kabisa, maprofesa wako ndio hao hao wanaotoa maboko kila siku....?, wanaomuita binadamu Mheshimiwa Mungu? Ona walipotufikisha..

Nyie ndio mkiambiwa mtu ni professor mnaamini anajua kila kitu, akija kijijini mnamuoshea barabara.
 
Prof naye ana upuuzi mwingi. Kusoma sana si kuwa na uelewa. Kula kuna ratiba zake na mwili unataka kula.
Mwisho wa siku kufa kupo tu, and it is only once in life time and for all, haijalishi ulikulaje. Nijitese niwe na shingo kama ya huyo Janabi... ya nini!!?

Mm nakula hadi kitambi kinatoka, ila likizo huwa naenda kijijini na kufanya kazi shambani hadi mwili unakaa sawa.

Ngoja nishushie huu uzi kwa mirinda ya buku..
 
Mzee baba hapo kwenye red sijakupata.

Ipo hivi,

ukila wanga mwili unautumia kupata nguvu katika mfumo wa glucose, ukisindilia sana mwili unakusaidia kuhifadhi huo wanga/glucose kwenye liver katika mfumo wa glycogen ambayo ndio mafuta sasa kwa namna nyingne,

Pindi mwili ukiishiwa nguvu/mfano umechelewa kula au hujala, ile glycogen inatolewa kwenye liver kwa kutumia hormone ya glucagon kuileta kwenye mfumo wa glucose ambao ndio unatumiwa na mwili kupata nguvu.

Kwa nini mtu anazidi kunenepa? Kwa kula wanga,

Sbb ni kwamba kila siku anakula wanga iliyozidi kiasi kinachohitajika, matokeo yake inaendelea kuhifadhiwa/jaa kama mafuta kwenye mwili...

Kumbuka, tunapozungumzia wanga tunazungumzia Sukari/sugar na ukizungumzia sukari unazungumzia glucose na ukizungumzia glucose unazungumzia Nguvu.
Semenya wa ukaldayo kumbe huko deep sana mgerasi wangu. Umeshusha Nondo kali maamae na madini yaliyojitosheleza.
 
Kulakula hovyo hovyo tutakula tuu na kunya tutakunya tuuu na kufa tutakufa tuu. Hakuna wa kutuzuia.
 
Mkurugenzi wa hospitali ya Muhimbili, Profesa Mohammed Janabi amesema mpaka sasa wanawake 100 wamewekewa puto na wanaume wachache. Prof ameongeza kuwa puto ni kitu kimoja lakini nidhamu kwenye chakula ni kitu kingine.

Janabi amesema kitu hatari zaidi kwenye mwili ni sukari na wanga na wala si mafuta kwasababu mwili hautunzi wanga wala sukari bali huvibadilisha kuwa mafuta. Ametaka watu kupunguza matumizi ya vitu vyenye sukari, utamu mkubwa na sukari yenyewe.

Prof Janabi amesema matatizo ya kushindwa kupata watoto, moyo, kiharusi, magonjwa ya kupumua, vifo vya ghafla asilimia mkubwa vinachangiwa na uzito usio sahihi na kula mara kwa mara. Profesa amesisitiza kutopeleka mwili kwa utaratibu wa chakula bali wale chakula wanapohisi njaa.
Huyu jamaa very ni Cheap ....ushauri wangu wana JF someni wenyewe mambo haya kuliko kumsikiliza huyu mjanja mjanja otherwise mtaumia.
 
Mwisho wa siku kufa kupo tu, and it is only once in life time and for all, haijalishi ulikulaje. Nijitese niwe na shingo kama ya huyo Janabi... ya nini!!?

Mm nakula hadi kitambi kinatoka, ila likizo huwa naenda kijijini na kufanya kazi shambani hadi mwili unakaa sawa.

Ngoja nishushie huu uzi kwa mirinda ya buku..
famchezo nini,?
 
Back
Top Bottom