Prof. Janabi: Kitu hatari zaidi ni sukari na wanga. Ataka watu kula wakihisi njaa kwani mwili hauendeshwi na ratiba ya chakula

We nawe rubish kabisa, maprofesa wako ndio hao hao wanaotoa maboko kila siku....?, wanaomuita binadamu Mheshimiwa Mungu? Ona walipotufikisha..

Nyie ndio mkiambiwa mtu ni professor mnaamini anajua kila kitu, akija kijijini mnamuoshea barabara.
Mheshimiwa Mungu!! Ila profesa macho nyoko kabisa
 
Nimewahi kufuatilia interviews zake mbili tatu aisee kwa anachokishauri unaweza jikuta unakufa kwa kufunga kama wafuasi wa Mackenzie. Jamaa anapinga kila kitu, mpaka matunda karibia yote yanayopatikanika kwa wingi humu Tz yeye yupo against. Sasa sijui anataka tuishije, haya mambo ya afya mimi nilimuachiaga Mungu tu afanye kazi yake. Nakula kila kitu lakini nahakikisha angalau siku 5 katika wiki nakata km 50 za kufukuza upepo (jogging) yaani angalau 10 kwa siku.
 
Huyu jamaa sijui familia yake inaishije.hapendi chakula kabisa yaani.sidhani kama kwake kuna jiko
 
Mkurugenzi wa hospitali ya Muhimbili, Profesa Mohammed Janabi amesema mpaka sasa wanawake 100 wamewekewa puto na wanaume wachache. Prof ameongeza kuwa puto ni kitu kimoja lakini nidhamu kwenye chakula ni kitu kingine.

Janabi amesema kitu hatari zaidi kwenye mwili ni sukari na wanga na wala si mafuta kwasababu mwili hautunzi wanga wala sukari bali huvibadilisha kuwa mafuta. Ametaka watu kupunguza matumizi ya vitu vyenye sukari, utamu mkubwa na sukari yenyewe.

Prof Janabi amesema matatizo ya kushindwa kupata watoto, moyo, kiharusi, magonjwa ya kupumua, vifo vya ghafla asilimia mkubwa vinachangiwa na uzito usio sahihi na kula mara kwa mara. Profesa amesisitiza kutopeleka mwili kwa utaratibu wa chakula bali wale chakula wanapohisi njaa.
Tulitarajia elimu kama hii na nyingine inayofanana na hii ndiyo iwe inawekwa kwenye mabasi wakati wa safari ili iyafikie makundi ya watu wengi wasiopata fursa ya kuingia mitandaoni kama hapa, lakini utashangaa 12hrs of travel time watu wameinua vichwa kutazama miziki ya vichupi na vitovu nje
 
😂😂😂😂🙌
Nimependa comments ila msosi si burudani pia au?
 
Kweli tunahitaji elimu me nilikuwa najua wanga inachakatwa kuwa lactose (glucose) iliyochangamka kumbe wanga kama makande bila marage na hayana kiini yanasababisha mafuta. ni hatari kwa kweli.

Kuna natamani kuuliza kwa idadi ya Tanzania wangapi wanakula wangu kwanini idadi ya wagonjwa ni chache. au kuna miili wakila wanga tatizo linatokea?
Yeah, wanga inatengeneza kitu inaitwa glycogen waliosoma biochemistry watufafanulie hapa!
 
Kweli tunahitaji elimu me nilikuwa najua wanga inachakatwa kuwa lactose (glucose) iliyochangamka kumbe wanga kama makande bila marage na hayana kiini yanasababisha mafuta. ni hatari kwa kweli.

Kuna natamani kuuliza kwa idadi ya Tanzania wangapi wanakula wangu kwanini idadi ya wagonjwa ni chache. au kuna miili wakila wanga tatizo linatokea?
Hapa kuna maelezo yanakosekana,kula wanga kama wewe ni mtu wa pilika pilika au mazoezi ya kutosha haina shida,shida iko kwa watu wanaokula wanga na maisha yao hayana mazoezi au shughuli zao ni za kukaa muda mwingi,Mfano mzuri watu wa kule vijijini wanatembea sana,unakuta mtu anatembea mpaka kilometer 10 kwa siku huo wanga au sukari vitamdhuru vipi..
 
Binadamu ni lazima tule sukari/wanga.Kutokula pia kunaleta maradhi.Huwezi wakati wote kusubiria mpaka ukihisi njaa ndipo ule.
Mfano umeamka asubuhi uhisi njaa.Mchana uhisi njaa.Utakula jioni tu ukihisi njaa.Hapana hii kiafya haifai.
Mwili ili ufanye kazi vizuri unahitaji upate virutubisho vyote muhimu kama mafuta,sukari,vitamins,minerals,amino acids nk.
Kwa mfano karibu chembechembe hai zote mwilini zinatengenezwa na mafuta aina ya cholesterol kwahiyo pamoja ya kwamba mafuta haya yana madhara mwilini kama kusababisha magonjwa ya moyo,hypertension,stroke nk lakini ni lazima yawepo(yatengenezwe)mwilini Kwani miili yetu(cells) inayahitaji ili ifanye kazi vizuri tuwe na afya njema na tuendelee kuishi.
Wengine ni wagonjwa tayari.Huwezi kumwambia kwa mfano mgonjwa wa kisukari ale pale anapohisi njaa tuu.
Wengine wanameza dawa mbalimbali kila siku,lazima wale Ili dawa zifanye kazi vizuri mwilini.
Kwa ujumla ni lazima tule,isipokuwa tule kwa kiwango stahiki(optimal amount),ama a balanced diet.
 
Mkurugenzi wa hospitali ya Muhimbili, Profesa Mohammed Janabi amesema mpaka sasa wanawake 100 wamewekewa puto na wanaume wachache. Prof ameongeza kuwa puto ni kitu kimoja lakini nidhamu kwenye chakula ni kitu kingine.

Janabi amesema kitu hatari zaidi kwenye mwili ni sukari na wanga na wala si mafuta kwasababu mwili hautunzi wanga wala sukari bali huvibadilisha kuwa mafuta. Ametaka watu kupunguza matumizi ya vitu vyenye sukari, utamu mkubwa na sukari yenyewe.

Prof Janabi amesema matatizo ya kushindwa kupata watoto, moyo, kiharusi, magonjwa ya kupumua, vifo vya ghafla asilimia mkubwa vinachangiwa na uzito usio sahihi na kula mara kwa mara. Profesa amesisitiza kutopeleka mwili kwa utaratibu wa chakula bali wale chakula wanapohisi njaa.
Ameshaona tumesahau ajenda yake, amekuja na ajenda ya kupunguza kula.

Sawa prof.
 
Back
Top Bottom